Kitu kilichowashinda Mkapa na Magufuli lakini kimewezwa na Kikwete na Rais Samia ni " Kukaa meza moja na Mpinzani wa Kweli na Kujadiliana"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,867
141,797
Hayati Mkapa na Magufuli waliamini katika kutumia nguvu kukabiliana na wapinzani wa kweli kwa wakati husika ndio utaona Mkapa hakuwahi kukaa na CUF bali aliwatwanga wakakimbilia Shimoni Mombasa.

Magufuli hakuwahi kukaa na Chadema bali aliwabomoa kwa kuchukua wabunge wake na viongozi muhimu kama Dr Slaa Lowassa na Sumaye.

Lakini mstaafu Kikwete aliwaalika Ikulu kwa mazungumzo viongozi wa Chadema wakati kikiwa chama kikuu cha upinzani.

Kadhalika Rais Samia ameweza kuzungumza na viongozi wakuu wa upinzani hapa Tanzania kwa sasa ambao ni mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe na makamu wake mh Tundu Lisu.

Mungu wa mbinguni mbariki Rais Samia!
 
Nilichojifunza ni kwamba mswahili ni kiongozi mwenye utu kuliko wale wa kule

Samahani sio ukabila ni halisi
Mimi ni mtu wa bara ndanindani kabisa tena kanda ile ya 'gang' lakini nakubaliana na wewe.

Nimeishi ughaibuni nchi nyingi na nimekuwa nikiona mabalozi wetu, mabalozi best na wenye treatment nzuri ukitembelea ubalozi huwa ni wale wa asili ya Zanzibar na kidogo wa pwani lakini ukute balozi mlugaluga amekulia mkoani huko vijijini huwa wana roho mbaya balaa, kama vile huwa wana chuki na watu wanaoishi ughaibuni(NB:huwa kuna exceptional cases chache).
 
Mbowe kaomba kushirikiana na serikali, kwa hiyo, rasmi Chadema sio chama Cha upinzani Bali mshirika wa ccm, karibuni sana Lumumba
20220305_101526.jpg
 
Hayati Mkapa na Magufuli waliamini katika kutumia nguvu kukabiliana na wapinzani wa kweli kwa wakati husika ndio utaona Mkapa hakuwahi kukaa na CUF bali aliwatwanga wakakimbilia Shimoni Mombasa...
Na technically hao wote wenye roho nzuri ni Waislam sasa ingia ndani ndaniiii ujue hua mnafundishwa nini mkiendaga Vatican. Usisahau Mwinyi pia muislam na yupo
 
J.K ndie alizungumza na upinzani lakini aliwazingua mfano mzuri issue ya katiba alipokea report ya warioba kwa bashasha na madoido tukajua mambo mazuri.

Alipoingia bungeni akazingua na ndio mwanzo wa zoezi lile kushindwa. Option aliyokubaliana na wakina cheyo nayo akaipiga chini. Hivyo ingawapo alikaa na wapinzani meza moja hakukuwa na matokeo ya maana. Hakuwa na political will ya kuleta mabadiliko.
 
Hayati Mkapa na Magufuli waliamini katika kutumia nguvu kukabiliana na wapinzani wa kweli kwa wakati husika ndio utaona Mkapa hakuwahi kukaa na CUF bali aliwatwanga wakakimbilia Shimoni Mombasa.

Magufuli hakuwahi kukaa na Chadema bali aliwabomoa kwa kuchukua wabunge wake na viongozi muhimu kama Dr Slaa Lowassa na Sumaye.

Lakini mstaafu Kikwete aliwaalika Ikulu kwa mazungumzo viongozi wa Chadema wakati kikiwa chama kikuu cha upinzani.

Kadhalika Rais Samia ameweza kuzungumza na viongozi wakuu wa upinzani hapa Tanzania kwa sasa ambao ni mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe na makamu wake mh Tundu Lisu.

Mungu wa mbinguni mbariki Rais Samia!
Samia ni rais wa hovyo sana kama Magufuli, mnafiki na anaendeshwa na mafisadi
 
Hayati Mkapa na Magufuli waliamini katika kutumia nguvu kukabiliana na wapinzani wa kweli kwa wakati husika ndio utaona Mkapa hakuwahi kukaa na CUF bali aliwatwanga wakakimbilia Shimoni Mombasa.

Magufuli hakuwahi kukaa na Chadema bali aliwabomoa kwa kuchukua wabunge wake na viongozi muhimu kama Dr Slaa Lowassa na Sumaye.

Lakini mstaafu Kikwete aliwaalika Ikulu kwa mazungumzo viongozi wa Chadema wakati kikiwa chama kikuu cha upinzani.

Kadhalika Rais Samia ameweza kuzungumza na viongozi wakuu wa upinzani hapa Tanzania kwa sasa ambao ni mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe na makamu wake mh Tundu Lisu.

Mungu wa mbinguni mbariki Rais Samia!
Siasa za Tanzania uongo uongo mtupu.Kwani aliyemfunga Mbowe na kumwambia ni Gaidi ni Magufuli au Samia?Huyu bibi kamfunga Mbowe ,Halafu ,Magufuli ndio mbaya.Unafiki wa kiwangp cha PhD.
 
Mimi ni mtu wa bara ndanindani kabisa tena kanda ile ya 'gang' lakini nakubaliana na wewe.
Nimeishi ughaibuni nchi nyingi na nimekuwa nikiona mabalozi wetu, mabalozi best na wenye treatment nzuri ukitembelea ubalozi huwa ni wale wa asili ya Zanzibar na kidogo wa pwani lakini ukute balozi mlugaluga amekulia mkoani huko vijijini huwa wana roho mbaya balaa, kama vile huwa wana chuki na watu wanaoishi ughaibuni(NB:huwa kuna exceptional cases chache).
We sio mtu wa bara.Ungekuwa mtu wa bara usingejitukana bhana.Kama ni mtu wa bara kweli una matatizo ya akili.
 
Nilichojifunza ni kwamba mswahili ni kiongozi mwenye utu kuliko wale wa kule

Samahani sio ukabila ni halisi

Nimekuelewa vizuri kabisa. Kwa hapa kwetu Mwinyi, JK na SSH wametenda haki nyingi kuliko WBM na JPM. Na sidhani ulikuwa unazungumzia uswahili. Ulikuwa unazungumzia imani. Hata uswahilini kuna wenye imani ya hawa wengine - sasa usiseme kusiko uswahilini hakuna hakuna utu! Au kinyume chake!!
 
Mimi ni mtu wa bara ndanindani kabisa tena kanda ile ya 'gang' lakini nakubaliana na wewe.
Nimeishi ughaibuni nchi nyingi na nimekuwa nikiona mabalozi wetu, mabalozi best na wenye treatment nzuri ukitembelea ubalozi huwa ni wale wa asili ya Zanzibar na kidogo wa pwani lakini ukute balozi mlugaluga amekulia mkoani huko vijijini huwa wana roho mbaya balaa, kama vile huwa wana chuki na watu wanaoishi ughaibuni(NB:huwa kuna exceptional cases chache).
Yaani ilifikia mahali tunatengana kwenye misiba kwamba kafa CCM hainihusu au kafa mpinzani hainihusu! Loo, hii hali haikuleta afya katika Taifa. Mwanzo Rais Samia alioonyesha kuliponya Taifa lakini chawa walioko CCM wakambadili mawazo, nashukuru kwa Sasa Rais Samia Yuko kwenye uhalisia wa tabia yake ya utu wa kuliponya Taifa, wale chawa wa CCM waendelee kununa Cha muhimu sisi Kama Taifa tuwe wamoja.
 
Mimi ni mtu wa bara kwa maana ya kabila langu, wazazi wangu wote wamezaliwa na kukulia bara lakini hilo halinizuii kusema ukweli kuhusu majority ya watu wa bara walivyo kitabia.
Sio ukweli.Kama ni mtu wa bara umekulia Pwani.Isitoshe si wote wenye tabia unazozisema.Aidha watu wa bara wamekuwa wakali ,kwa kuwa wanataka ukweli sio unafiki.Unaowasifia wamejaa unafiki na undumila kwiri.
 
Jana siku ya tarehe 4/03/2022 DPP Kupitia kifungu cha 91 Cha Sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai aliamua kufuta mashitaka ya Ugaidi dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema na wenzake watatu.

Kwa kupitia kifungu hicho tafsiri yake ni kwamba pale ambapo itaonekana inafaa DPP anaweza yarejesha mashitaka hayo.

Hiyo inamaana kwamba kesi iliondolewa mahakamani bila ya Mbowe kutoa utetezi wake mahakamani na hatimaye mahakama kutoa maamuzi kuhusiana na tuhuma hizo.

Kwakua hakuna hukumu yeyote ile ya mahakama iliyosema kwamba Mbowe hajafanya alichotuhumiwa nacho au kakifanya na kwakua bado DPP anaweza kurejesha tena kesi mahakamani basi kiufundi tunasema kwamba tuhuma dhidi ya Mbowe zinabakia pale pale.

Kwakua tuhuma bado zipo kwakua hakuna rekodi ya mahakama inayomsafisha Mbowe na tuhuma dhidi yake basi kwa manufaa mapana ya Chadema na Taifa kwa ujumla inampasa Mbowe kujiuzulu nafasi yake ya Uwenyekiti na kukaa mbali na siasa za kiushindani.

Inampasa Mbowe kujiuzulu kwani anakosa sifa muhimu ya uadilifu kwani tuhuma dhidi yake ni kubwa na hatarishi kwa ustawi wa Taifa lolote na haitakuwa afya kwa chama kuongozwa na kiongozi ambaye anaishi na tuhuma hizo.

#free Sabaya
 
Back
Top Bottom