Kitu/ kifaa kipya ambacho hakikuwahi kuwepo

Centia2

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
1,018
1,621
Kuna mkuu mmoja aliwahi kuleta uzi wa kwamba ukipewa uwezo wa kubuni kifaa kipya utabuni nini?

Kutokana na utata mwingi ambao huisumbua jamii juu ya kubaini ukweli wa jambo au wa mtu hasa mahakamani.

Hivi kweli mzungu/Mchina na akili (maana tunaamini hivyo) yake yote kweli ameshindwa kupata kifaa hicho!

Yaani kiwe kinawekwa kifuani au kwenye ubongo au popote ili kisome mawazo ya mtu anayoyawaza, kituoneshe nia ya kuwaza hivyo na hata lengo la muhusika.

Haya sasa wadau wabunifu changamkieni fursa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kote mbali sana huko. Tafuta tech ya kifaa cha kuhakikisha mbu au inzi hakai eneo angalau mita 20 kukizunguka bila kutumia madawa.
 
Kote mbali sana huko. Tafuta tech ya kifaa cha kuhakikisha mbu au inzi hakai eneo angalau mita 20 kukizunguka bila kutumia madawa.
Kuna frequencies kali (> 20khz) ambazo zinampigia kelele mbu ila sisi hatuwezi kuzisikia, niliwahi kusanifu circuit ya kifaa hicho miaka 20 iliyopita, kufukizia mbu.
 
Mbona iyo technologia ipo kitambo ushawahi kusoma historia ya Steven Hawkins alikuwa hawezi kuongea au kuandika walimuunganisha mashine flani zinazosoma frequency kwenye ubongo wake na kuinterprate Nini anachowaza.wazungu wamefikabali eti ,mbali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna frequencies kali (> 20khz) ambazo zinampigia kelele mbu ila sisi hatuwezi kuzisikia, niliwahi kutengeneza circuit ya kifaa hicho miaka 20 iliyopita, kufukizia mbu.
Hiki kifaa naweza kukipata wapi kwa sasa mkuu. Mbu husumbua sana maeneo napokaa kila uchwao lazima nichome UDI wa mbuu na kupuliza sumu ya rungu angalau mara 3 kwa wiki.

Siku hizi kuna hizi mosquito repellent bracelet, wanauza kama $1 amazon.

Pia unaweza jaribu kutumia simu, tafuta app inayoweza kupiga makelele ya frequecy ya juu, yanayoweza kumfukuza mbu na wadudu wadogowadogo.
 
Kuna frequencies kali (> 20khz) ambazo zinampigia kelele mbu ila sisi hatuwezi kuzisikia, niliwahi kutengeneza circuit ya kifaa hicho miaka 20 iliyopita, kufukizia mbu.
Bei gani sokoni. Mi naona utapiga hela ndefu sana. Sasa hivi dawa uswahilini inayotumiwa sana ni ile ya kuchoma ambayo hata ukichoma inadumu sana sana dk 45 hivi, kama itaweza kudumu hata miaka 2 utapiga hela ndefu. Jaribu kuzifanyia kazi
 
Hicho kifaa nilitengeneza zamani sana (2000) ilikuwa ni project ya chuo. Kwa sasa simu janja inaweza kufanya hiyo kazi kwa ku broadcast 38-44 KHz.
 
Mbona iyo technologia ipo kitambo ushawahi kusoma historia ya Steven Hawkins alikuwa hawezi kuongea au kuandika walimuunganisha mashine flani zinazosoma frequency kwenye ubongo wake na kuinterprate Nini anachowaza.wazungu wamefikabali eti ,mbali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu mimi nipo huku Gongolamboto kama hiyo kitu ipo nielekeze iko wapi nitashukuru.

Ila naona huyo mkali amekalia fweza. Tech inatakiwa ipunguze kero fulani kwenye jamii.

Jana nimeliwa sana na mbu kuangalia movie kali ya zamani EXECITIVE DECISION. nimechoma vipande sita ili kumaliza movie.
 
Hicho kifaa nilitengeneza zamani sana (2000) ilikuwa ni project ya chuo. Kwa sasa simu janja inaweza kufanya hiyo kazi kwa ku broadcast 25KHz frequency.
Sasa mchoro si upo nadhani unaweza kuuboresha halafu tuujaribu niko bondeni hapa karibu na mto mbu hawakwepeki.
Inzi wana msimu lakino mbu ni balaa
 
Sasa mchoro si upo nadhani unaweza kuuboresha halafu tuujaribu niko bondeni hapa karibu na mto mbu hawakwepeki.
Inzi wana msimu lakino mbu ni balaa
Unachofanya ni kutengeneza pulse kwa kutumia 555 timer IC halafu una tune output kwa kutumia oscilloscope kupata frequecy inayotakiwa (38KHZ).
 
Good! Kwa kutumia kanuni "energy can neither be created nor destroyed but can be converted from one form to another" na kwa kuwa sound is a form of energy, I wish kingepatikana kifaa cha ku-trace sauti za manabii wa zamani. I wish ningeisikia sauti ya Jesus of Nazareth.
 
I wish kingepatikana kifaa cha ku-trace sauti za manabii wa zamani. I wish ningeisikia sauti ya Jesus of Nazareth.
Wow, I hypothesized about this when I was a teenager. I thought to myself, if energy is conserved then all images (people, buildings) of the past can be retrieved or translated.
 
Wow, I hypothesized about this when I was a teenager. I thought to myself, if energy is conserved then all images (people, buildings) of the past can be retrieved or translated.
... safi sana! Na maujinga mengine kama wizi ungeisha. Maana would be possible to trace back all events pertaining to a certain scenario. Kwa mfano ingeonesha mwizi alivyochukua silaha, kaiweka ndani ya koti, kawasha gari, kakaribia eneo la tukio, kavaa mask kuficha sura, kauwa mlinzi, kavunja mlango, kaiba, then huyoo kaondoka zake, kavua mask, kaendelea na shughuli zake nyingine n.k. kama sinema fulani hivi. Of course, hayo yatatakiwa kuwa under strict control ili kutoingilia faragha za watu, n.k.
 
Hiyo kitu watu wasiojulikana wakiipata, watakuwa wameokota dodo kwenye mnazi.
 
Unachofanya ni kutengeneza pulse kwa kutumia 555 timer IC halafu una tune output kwa kutumia oscilloscope kupata frequecy inayotakiwa (38KHZ).
Mi naona kama inawezekana vifanyie kazi ila tengeneza viwe vina expire baada ya miezi mitatu kwanza kwa bei ya majaribio. Vya majaribio unaweza kuuza au kugawa bure ili kuvitambulisha.

Baada ya hapo utapata mrejesho ndio ufanye kweli muda wa matumizi uzidi na bei.
 
Back
Top Bottom