Kitu kidogo kimewashinda?

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Nawasalimu wanajamvi wote.

Nimekuwa nafuatilia mara kwa mara siasa za hapa kwetu Tanzania hususani matamko ya wale wanaotuongoza.

Nikumbushe tu, moja kati ya vitu ambayo vilivaliwa njuga ni bei ya Sukari. Matamko yalitoka na kuambiwa kuwa bei elekezi ni 1,800/= kwa kilo moja.

Tena tukaaminishwa kuwa mfanyabiashara yeyote atakaye ficha sukari atanyang'anywa na watu kupewa bure. Mimi binafsi nilikuwa nikisikia tu sukari imekamatwa ila kupewa watu bure sijawahi sikia.

Mambo yalipokuwa magumu zaidi tukaambiwa uzalishaji wa ndani ukianza sukari itauzwa kwa hiyo bei elekezi.

Naombeni mnijuze wanajamvi,

1. Je uzalishaji wa ndani wa sukari haujaanza?. Huku kwetu sisi sukari inauzwa 2,400/= hadi 2,500/= zaidi ya bei elekezi.

2. Viongozi wetu wamesahau walichosema na kutuaminisha au?

3. Kama jambo dogo la sukari wameshindwa hayo mengine wataweza kweli?

Nawaomba wanajf wenzangu mtakapokuwa mnanijibu haya maswali au kuchangia wekeni na bei ya sukari huko ulipo.

Ahsanteni!

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom