Isaiah 52: 13
13Behold, My servant will prosper,
He will be high and lifted up and greatly exalted.
14Just as many were astonished at you,
My people,
So His appearance was marred more than any man
And His form more than the sons of men.
15Thus He will sprinkle many nations,
Kings will shut their mouths on account of Him;
For what had not been told them they will see,
And what they had not heard they will understand.
Jaribu kufikir mateso aliyoyapata Yesu, alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, magonjwa yako yanaweza kupona kwa Jina la Yesu, Neno la Mungu linafafanua hapo juu kwamba, alipata matesi makali kupita kiasi kana kwamba sura yake iliharibiwa kabisa kwa mapigo yake, lakini wafalme na wakuu hawakujua ni nani wanamsulubisha, hawakujua kama wanamsulubisha mtumishi wa Mungu aliye hai, hawakujua kama yalikuwa ni mapenzi ya Mungu mtumishi wake afanywe hivyo, hawakujua kama anateswa vile kubeba dhambi zao wenyewe, hawakujua kama huyo anayeteswa alikuwepo tangu awali, ni Mungu aliyejigeuza kuva mwili wa mwanadamu ili ashuke kwetu afanane nasi abebe yote tunayopitia kwa ukombozi wetu, walijua Mungu anamtesa au amemtupa, kumbe ulikuwa mpango wa Mungu baba kwa ukombozi wetu, walipokuja kugundua siri hii walishangazwa mno.
Yesu Kristo alijeruhiwa kwa ajili yako, hauna sababu ya kutokuokoka, deni lote la dhambi limelipwa, shetani hana haki kwako tena kama ukikimbilia kwa Yesu, dunia na vyote vilivyomo vinapita, kuna maisha baada ya hapa, jiandae sasa ili upone. Mungu awabariki.