Umewahi jiuliza inakuaje -watu wanaofundisha wenzao kufanikiwa, maisha yao pia bado ni ya kuunga unga tu na pengine hiyo kazi ya kumotivate watu ndo chanzo cha mkate mezani kwake?
Mwalimu wa marketing na ujasiliamali hana hata kiosk cha mboga mboga!!!!
Basically, wanopaswa kufundisha watu namna ya kufanikiwa ni wale ambao wameshatusua ili wanachokifundisha kiwe ni zao la practical experience na sio merely theory
Ila katu matajiri hawatokaa hata siku moja wakuambie ukweli namna ya kufanikiwa na ni jinsi gani walipata pesa maishani mwao
A matter of fact, asilimia kubwa ya watu waliotoka kimaisha kuna game chafu walizozicheza na kujikuta kwenye direction waliopo Leo, wako:
waliodhurumu
Walioiba
Walioua
Waliotoa makafara
Wanaomiliki jini chuma ulete
Waliodanga na wenye nazo kisha wakawaua wapenzi wao ili walithi mali etc
Haya mambo, hakuna tajiri atakuambia aliyafanya, lnstead atakuhimiza Fanya kazi kwa bidii na weledi.
Mdau leta uzoefu wako ktk hili
Ndugu mtoa mada utajiri ni fumbo kubwa, ukweli ni kwamba wapo waliopata utajiri kwa njia halali waliopata kwa njia haramu pia wapo. sio kweli kwamba matajiri wote wamepata kwa njia haramu.
Utajiri ni roho, na umasikini ni roho.
Maana yake ni hii- mfano wapo matajiri wengi sana ambao ni masikini wa kutupwa, katika jamii yako lazima kuna mtu unaye mfahamu ambaye amewahi kumiliki mali nyingi na zote zilishapotea na sasa hv ni mtu wa kawaida, huyu ndio mwenye roho ya umaskini, umaskini una tabia zake na hata ukimpa fedha zote za benk just matter of time atakuwa bankrupt atarudi kwenye asili yake..
Vile vile wapo kwenye jamii watu waliokuwa maskini sana na sasa hv wanauwezo mkubwa kiuchumi.
SIRI ya utajiri (fedha) ni tabia, kuna tabia ambayo fedha zinakuja zenyewe na kuna tabia ambayo fedha zina kimbia. penye tabia/roho nzuri ya fedha utajiri hautaisha vizazi kwa vizazi. kinyume chake penye tabia/roho mbaya hata kama pana utajiri mkubwa hautadumu.
Utajiri wwt uliokuja kwa njia haramu kimsingi sio utajiri, kwa maana ya uhuru na manufaa ya utajiri. wengi tunaowaona kwa macho kama matajiri wanamateso makubwa sana ikiwemo masharti ya kula, kuvaa, unyumba, n.k n.k.
Wasaka utajiri wengi wanafeli kwa sababu wanataka kucopy mafanikio/ kazi au shughuli ya mwingine. anayefanikiwa kwa kuuza nyanya akatajirika ukimuiga itakula kwako na sababu ni rahisi utajiri ni tabia/roho ambayo ww hutaweza kuiga tabia ya mwingine.
Usitumie nguvu kusaka pesa, chochote unachofanya kupata fedha lengo liwe kutoa huduma na sio fedha, hapo fedha zitakuja zenyewe. Saikolojia ya fedha ukiifukuzia inakimbia, lakini ukijifanya kama huitaki itakuja yenyewe malengo yako yatatimia