Yani kwa watu walio andika utumbo we ni miongoni wao, unataka kutuaminisha kuwa mwanadamu anaijua sayansi zaidi ya Mungu? Hiyo tabia uliyo nayo ni ya ulafi jifunze kuwa na kiasi katika maisha yako.Clion Dismas, IQ yako na biological knowledge yako ni hafifu sana.Kwanza unachanganya mambo ya sayansi na mambo ya imani yaani dini ambavyo ni vitu viwili tofauti kabisa.Halafu hata uandishi wako ni duni sana kwani mara nyingi umeandika Kizaramo badala ya Kiswahili fasaha na hii inadhihirisha kuwa ikiwa hata Kiswahili tu lugha ya taifa inakupiga mweleka, mambo magumu ya sayansi utayaweza wapi? Elewa kwamba nyama na damu ni vyakula bora vinavyopatikana kwa urahisi duniani kote.Nyama itakuwa na madhara pale tu daktari atakaposema kuwa mgonjwa huyu anahitaji 'no or low protein diet katika matibabu yake.Kama ilivyo kwenye maziwa ambapo yametengenezwa kutokana na mahitaji ya miili ya watu hasa katika kimatibabu.Kuna maziwa ya 'no fat',au 'full creamed milk' nk.yote hii inatokana na mahitaji ya walaji kuzingatia afya zao kimatibabu.Nyama ya mnyama ni mbaya pale tu mnyama anapokuwa amepata maambukizi mbali mbali kama kimeta, TB, brucellosis, minyoo mbali mbali, nk. Damu ya mnyama pia ina virutubisho kibao kama calcium, magnesium, manganese, sodium, zinc, iron, fats, proteins,vitamins nk.Damu ni mbaya iwapo imetoka kwa mnyama ambae ana maambukizo ya magonjwa mbali mbali na haistahili kuliwa.Kulinganisha mifano ya makatazo kula nyama au damu kama ilivyobainishwa kwenye biblia au quran haiwezi kulandana na ukweli wa kusayansi.Kwenye biblia kuna kumbukumbu la Torati na Mambo ya Walawi ambamo humo ndo kuna makatazo hayo.Mambo ya Walawi ni typical historia ya watu wakale wa Walawi ambayo ili base kwenye utamaduni wao.Ni watu halisi walioishi kipindi hicho wakiwa 100% hawana elimu yeyote ya kusayansi.Walipokuwa wanaparamia vyakula vyenye matatizo ya mambukizi mbali mbali walikuwa wanapitisha katazo moja kwa moja kuwa ni haramu.Hata nyama ya nguruwe waliita haramu simply kwa sababu kila walipoparamia kula kwa pupa mwisho walijikuta wanahara ovyo kwa sababu ya mafuta mengi, hatimae wakubwa wa dini wakapitisha zuio kwa mgongo wa dini kuwa nguruwe ni haramu.Utamaduni wa watu wakale wajinga wa kabila la Walawi lina aksi nini na utamaduni wa makabila mengine duniani??.Nguruwe ana nyama tamu na bora kuliko nyama zingine nyingi ila nyama yake itakuwa mbaya pale tu mnyama yule atakapokuwa ameambukizwa na magonjwa mbali mbali kama nilivyobainisha awali na atakuwa hastahili kuliwa.Kwa sasa duniani kote kuna madaktari wa wanyama ambao hupima na kuthibitisha kuwa mnyama aliechinjwa anastahili kuliwa pamoja na kula kisusio kwa wale wanaopenda.Bwana Dismas pamoja na wasomaji wengine watakuwa wamepakua walau kile kidogo wanachostahili kupata.Imeletwa kwenu na Tyupa 0620229448.