clion dismas
Senior Member
- Aug 6, 2017
- 185
- 169
NYAMA,NYAMA- TUIFAHAMU KWA UFUPI
Habari ndugu, pole na majukumu na mshukuru MUNGU kuiona siku na mwaka huu pia. naomba kwa ufupi nieleze machache juu ya nyama kama mboga, faida kadhalika na maudhi yake kwa mwanadamu. twende wote.
Kwa ufupi kabisa, nyama ni moja kati ya kundi la vyakula, ujulikana kama kitoweo na uliwa na watu wengi sana duniani. Chanzo chake ni wanyama tuwafugao katika makaazi yetu.
Haijalishi ni nyama nyekundu au nyeupe. Naongelea nyama yote kwa ujumla. Wengi tunapenda kitoweo hiki, hebu kwa ufupi tuelewe asili yake, ni namna gani tunaila hadi leo na kadhalika faida zake pamoja na maudhi yake katika mwili wa binadamu.
CHAKULA CHA ASILI CHA MWANADAMU NI KIPI?
JIBU: Matunda na nafaka nzima.
Tukisoma historia tutaelewa fika juu ya hili kwamba zama za wanadamu wa kale, zama za mawe watu waliishi kwa matunda na nafaka nzima.
Tukiichunguza BIBLIA, MWANZO 1: 29, MUNGU ASEMA HAYA KWA ADAMU NA HAWA: -
“tizama nimewapa kila mmea utoao mbegu ulio juu ya uso wa dunia, kila mtii wenye mbegu katika tunda lake ndivyo vitakua chakula kwenu.”
Naam, ndiyo mlo wa kwanza kabisa kutolewa na MUNGU kwa wanadamu kabla ya kuanguka katika dhambi.
Adamu aliishi kwa miaka 930 (mwanzo 5:5) kwa chakula elekezi toka kwa MUNGU, ingawaje, hakuna ajuaye, wasinge muasi MUNGU, yeye na mkewe, yumkini wangeishi milele. Kadhalika na kilembwekeze chake METHUSELA, kiliishi kwa miaka 965.
JE, MUNGU ALII HALALISHA NYAMA?
JIBU: NDIYO.
Katika ukoo wa ADAMU, maasi yalizidi kuwa mengi sana na MUNGU alinuia kuuondosha uzao wote wa uasi (MWANZO 6:7), kupitia kwa NUHU, mtoto wa LAMEKI, kitukuu cha ADAMU.
Mpango wa MUNGU kukiondosha kizazi cha uasi ulimwenguni ilikua kupitia MAFURIKO, maji ya mvua, iliyonyesha kwa muda wa siku 40, USIKU NA MCHANA (mwanzo 7:12). Ndege warukao, wanyama wa kila aina na binadamu wote waliokua na uasi mbele ya macho ya MUNGU walikufa kwa mafuriko yale (MWANZO 7:21-22). MUNGU aliipa kibali familia ya NUHU (jumla yao 8) kuwa hai, kwa maana walimpendeza MUNGU.
NAAM, BAADA YA GHARIKA ILO, MUNGU AKAONGEZA VYAKULA, AKARUHUSU UKOO WA NUHU KULA NYAMA. NYAMA IKAANZA KULIWA HAPA. (MWANZO 9:3), “… kama nilivyokupa mimea ya kijani, nimekupa kila kitu…. Kila kiishicho, chenye pumzi ya uhai kitakuwa chakula kwako.”
Kwa sababu MUNGU yu na akili kupita wanadamu na viumbe wote, alitupa muongozo wa ni manyama gani na ndege gani tule, kwa lugha nyingine, sisi hatuli kila kitu, bali twala kulingana na maelekezo ya MUNGU. (MAMBO YA WALAWI 11), AMEAINISHA VILE VYA KULIWA NA VISIVYO VYA KULIWA.
LAKINI, ONYO LILITANGAZWA: -
OLE ULITOLEWA NA MUNGU, MWANZO 9:4,
“USILE NYAMA NA UHAI WAKE, YAANI DAMU”.
SASA, TUNAANZA KUMUELEWA MUNGU YA KWAMBA SAYANSI ANAIJUA YOTE, MWANZO HADI MWISHO. Anajua ya kwamba nyama ina madhara, anajua ya kwamba wanadamu ni wakengeufu siku zote (yumkini ndio maana mwanzoni kabisa akuruhusu nyama kuliwa) na anajua fika ya kwamba MAGONJWA YOTE YA WANYAMA YAKO KWENYE DAMU ZAO.
KWANINI MUNGU ANASEMA TUSILE NYAMA NA DAMU YAKE?
JIBU: DAMU INABEBA VIMELEA VISABABISHAVYO MAGONJWA
Wataalamu wa afya na wanasayansi wote ulimwenguni tutakubaliana kwamba makuzi ya viumbe wadogo katika maabara zetu, mfano bakteria hufanyika katika damu. Asilimia kubwa uwa hivi.
Kuna baadhi ya nadharia ya kwamba, magonjwa ya ng`ombe hayawezi kuwapata binadamu, yaani, magonjwa ya specie moja hayawezi kwenda kwa specie mwingine. HUU NI UONGO, JIULIZE MASWALI MARAHISI, KWANINI NYAMA INAPIMWA NA BWANA MIFUGO KABLA YA KUUZWA.?
Kuna tafiti moja ilifanyika, Ng’ombe aliyekuwa na saratani ya leukemia alikamuliwa maziwa na kunyweshwa watoto wa sokwe kwa muda wa miezi 3, wale sokwe hawakuwa na saratani ya leukemia awali. Lakini baada ya kutumia maziwa yale kwa muda ule, walikutwa na maambukizi ya ile saratani.
Tutajiuliza maswali mengi, je si nyama kabla ya kwenda buchani, wataalamu wa afya si manaipima na kuigonga mihuri kwamba iko vizuri na haina shida, sasaje, kuna shida gani kula na damu yake?
JIBU NI JEPESI, “HEKIMA YA MWANADAMU NI UPUMBAVU KWA MUNGU”.( 1 wakorinto 3:19). MUNGU ni mwerevu kuliko kiumbe yeyote yule hapa chini ya jua, akikataza jambo au akisema usifanye hiki na ukafanya, mwisho ni aibu na kifo.
UMEWAHI KULA NYAMA BILA YA DAMU YAKE KAMA TULIVYOELEKEZWA NA MTABIBU MKUU.? Kwa lugha nyepesi, ukanunue mchanganyiko/steki kilo moja, ichemshe, mwaga maji, chemsha tena, mwaga maji, ongeza maji, chemsha tena, mwaga, mpaka nyama yako iwe nyeupena damu yote iishe. UMEWAHI FANYA IVYO.?
UMEWAHI JIULIZA KWANINI MLO WA MUNGU WA AWALI HAUKU USISHA NYAMA?
Yumkini kwa sababu zifuatazo hatuwezi jua, -
1. Hatuna meno ya kurarua(chonge), kama wanyama wengine walioumbwa kula nyama maisha yao yote. Kwani MUNGU angetaka kutuwekea chonge, angeshindwa? Tafakari.
2. Mate yetu wanadamu asili yake usaidia mmeng’enyo, lakini mate ya mbwa hayausiki na mmeng’enyo. Yaweza kuwa sababu nyingine pia. Kwa sababu, mmeng’enyo wa mwanadamu uanzia kinywani wa mbwa ni tumboni.
3. Utumbo mwembamba wa mwanadamu ni mrefu sana ukilinganisha na utumbo mwembamba wa viumbe wala nyama. Ifahamike wazi ya kwamba, nyama mmeng’enyo wake kwa mwanadamu sababu ya maumbile yake ufanyika baada ya masaa 48 hadi 72. Tofauti kabisa na viumbe wala nyama ambao wao ni kwa haraka na muda pungufu ya huo sababu ya jinsi walivyoumbwa.
JE, NYAMA INA VIRUTUBISHO GANI? AU INA NINI NDANI YAKE?
PROTINI, VITAMINI, MADINI MBALIMBALI,FATI
JE, NYAMA INA FAIDA GANI MWILINI?
1. Usaidia kukua kwa mwili, sanasana kwa watoto
2. Kujenga na kuulinda mwili na magonjwa
3. Kuupa joto mwili n.k
JE, NYAMA INA MAUDHI GANI MWILINI?
Katika nadharia za kiroho, nyama ina madhara katika hali kuu 3: -
1.Kimwili, mwili kushambuliwa na magonjwa mbalimbali. Mfano, kuvimba miguu(gout), magonjwa ya moyo na presha
2.Kiroho, kwa sababu na kuwa na viamsha hisia yaani stimulants, humfanya mtu kutenda matendo mengine yasiyompendeza MUNGU. Kwa mfano, ulevi, kutusi, kuona mambo maovu ni sawa na kadhalika.
Twaweza jifunza pia kwa wana wa IZRAELI, walipokua wakitoka katika nchi ya utumwa ya MISRI. Walipokua jangwani wakielekea nchi ya ahadi wali miss vitu vingi sana na vya ufahari walivyokua wakivipata nchi ya utumwa misri.
Walimnung’unikia MUSA, MUSA AKAMULIZA MUNGU, (“…NIPATE WAPI NYAMA MIMI YA KUWAPA MAKUTANO YOTE HII...? HESABU 11:13). (kama wewe ulizoea kunywa pombe na yumkini imepita mwezi hujaipata, wajisikieje? Hivi ndivyo vichocheo vilivyokua ndani ya mwili wa wana wa Israeli jangwani kwa sababu ya nyama waliyokuwa wakila misri). Musa alimnung’unikia MUNGU aliyekua amemfanya awe kiongozi wa msafara wa watu wake, na fika, MUNGU hakutaka kuwalisha nyama kwa sababu alijua Zaidi kuhusu nyama.
Manung’uniko yalipozidi, MUNGU aligadhabika sana na akasema maneno haya kwa wale wana wa Israeli, HESABU 11: 19, “…hamtokula nyama siku 1,2,5,10 au 20 bali mtakula mwezi mzima mpaka zitoke kwenye miimo ya pua zenu…”. HAKIKA UTAONA NI KAULI YA UBAYA TOKA KWA MUNGU, NA HAKIKA, NYAMA ZINATUTOKEA PUANI LEO. TULIZILILIA, TUKAMPANGIA MUNGU TULE NINI, NI MAGONJWA YA AJABU YASABABISHWAYO NA NYAMA KILA KUKICHA.
( kwa siku kiafya yakupasa kula gramu 170 za nyama kwa afya-American Heart Association)
3.Kiakili, kuna baadhi ya tafiti zimeonyesha nyama uhafifisha uwezo wa kufikiria wa mwanadamu. Na utumiaji wa nyama kwa muda mrefu kwa watu wanaosoma, mara nyingi uwezo wa kumbukumbu uwa chini.
Kisayansi kadhalika yathibitisha: -
1. Matatizo ya kuongeza lehemu nyingi mwilini
2. Shinikizo la damu
3. Unene kupita kiasi
4. Gout
5. Saratani
6. Kisukari n.k
JE, NI KWELI HAKUNA MBADALA WA NYAMA?
Hapana, upo mbadala wa nyama: -
Mchanganyiko wa maharagwe ya soya na mchele. Protini inayopatikana hapa ni karibia asilimia 90 ya ile ipatikanayo kwenye nyama.
Kadhalika, mimea mingi jamii ya mikunde, protini zilizoko ndani yake haziulemei mwili na zinameng`enywa kwa wepesi
Kuna chakula maalum cha soya, mbadala wa nyama. Vyote hivi vinaweza kutumika sehemu ya nyama.
SHUHUDA NA MREJESHO KWA WAPOKEA SOMO
1. " MAMA YANGU NYAMA APIKAYO KATIKA MATUKIO YA SHEREHE ANANUNUA MACHINJIONI. NA HUA ANAWAAMBIA WASIIOSHE, NA IKIFIKA JIKONI, ANAIPIKA NA DAMU BILA KUIOSHA, ANASEMA WATEJA WANAPENDA ILE LADHA YA DAMU"
2. " MZEE WANGU KAVIMBA MIGUU NA DAKTARI KAMZUIA NYAMA KAMA ANATAKA KUISHI"
3." MDOGO WANGU ALIYE DARASA LA SITA KAZUIWA NA DAKTARI KULA NYAMA, INAMUUMA, NI MDOGO SANA, LAKINI, DAKTARI KASEMA UGONJWA ALIONAO, NYAMA ITAUFANYA UWE MKUBWA SANA NA WAWEZA PELEKEA KIFO"
waweza kua na shuhuda pia, twambie, wambie watu wajue kweli, kuna shida katika nyama. hao ni wachache kati ya wengi walionipa habari izo pindi nikiwa natoa mhadhara.
HITIMISHO
Wanyama tulao nyama zao ndugu kwani wao wala nini? Utamu wa nyama zao umejengeka katika virutubisho vipi? Kweli si majani? Sasaje, si bora ukifaidi utamu wa moja kwa moja kwa kula mbogamboga na nafaka walazo wanyama kuliko kula utamu huu katika hatua ya pili yani nyama?.
SIKUZUII KULA NYAMA NDUGU NA SINA UWEZO WA KUFANYA IVYO LAKINI NAKUELIMISHA, MAAMUZI NI YAKO MWENYEWE.
UMEWAHI AMBIWA NA TABIBU “ACHA NYAMA”? KAMA NDIYO, WAJUA UCHUNGU WAKE NA KAMA BADO, USINGOJE MPAKA TABIBU AKUELEKEZE, UTAKUA UMECHELEWA, MUOMBE MUNGU UKUSAIDIE USIITEGEMEE NYAMA KAMA CHANZO CHA UHAI WAKO.
Rejea
Meat analogue - Wikipedia
REUTERS
American dental association
VITABU
Biblia
your what you eat
ministry of healing by ellen g white
CLION ODHIAMBO
Email: odhiamboclion@gmail.com
Youtube: clion odhiambo
Simu: 0759154479
Ikikupendeza, tuungane kuhabarisha ulimwengu, kwa kudhamini masomo haya au kwa nam,na yeyote ile. watu wana shida, watu hawana elimu hizi. kama MUNGU kakufanya kuwa sehemu fulani, basi kuwa mbaraka kwa wengine pia.
vituo vingi vya tiba mbadala vyaanzishwa kila kuchwa na tiba zao ni matunda, nafaka na mbogamboga. tupaze sauti, atakaye sikia, akayaishi, aponywe.
MUNGU NA AKUBARIKI.