Kitimtim Kipawa - JK azuiliwa kupita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitimtim Kipawa - JK azuiliwa kupita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WomanOfSubstance, Oct 15, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  HEBU TUJULISHENI MLIOKO KIPAWA...mabomu ya machozi huko...ni aje wamemzuia mkuu wa nchi asipite?
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ni kweli VC,

  Mabomu ya machozi yanaendelea kupigwa...

  Hii imesababisha hata nikate simu kwa mwakilishi wetu kwenye Press Conference ya Zitto ili kuongea na huyu aliye eneo la tukio.

  Hali si shwari
   
 3. K

  Kyachakiche JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 16, 2009
  Messages: 911
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  Kulikoni tena wakuu. Ni maswala ya upanuzi wa airport au ni nini?
   
 4. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Yeah,

  Wananchi hawataki kulipwa fidia kwa sheria ya mwaka 1967. Wanataka sheria mpya ndo itumike. Leo ndio siku iliyokuwa imepangwa kuanza kulipwa kwa wananchi hawa lakini walitoa tamko kuwa hawakubaliani na serikali na hivyo leo wakaamua kutanda barabarani kumzuia JK kwenda Airport.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Bila shaka ni masuala ya fidia.Wengi wanapinga kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya zamani wakati tayari ipo sheria mpya.

  Walioko uko tafadhali tupeni habari kamili
   
 6. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  HAli kidogo imetulia ila sie tulio jirani nao tumeyapata hayo machozi
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ngongo,

  Ndicho chanzo, kuna mtu yupo jirani na eneo hilo, nitakufahamisheni hatma ya wananchi hawa.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Great,

  Afadhali umetufahamisha walau kama hali imetulia. Ilikuwaje? Nani alikuwa anapiga mabomu hayo? Ili iweje? Kwanini wananchi watawanyishwe? Kwanini rais asiwasikilize kabla ya kuendelea na safari yake? Kipi muhimu kwake?
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  kwa hesabu za haraka haraka yamepigwa zaidi ya kumi tulikuwa tunawachungulia kwa dirishani tu vijana wa ukonga walivyokuwa wanakimbizana na wakazi hao waliogoma kulipwa pesa zao leo sababu kubwa ni huo mfumo wanaotaka kuutukia.

  Ila kuna bango moja limenifurahisha linasema "HATUDANGANYIKI NA VIJISENTI VYENU"
   
 10. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160  Mkuu si unajua tena hii sirikali yetu ikiamua kitu imeamua?
  Vijana wa hapa jirani na kipawa (FFU) ndio walikuwa na haka kajizoezi maana yamekaa muda mrefu kwenye ile stoo yao hayajatumika nao hawajafanya mazoezi ya kupiga na kukamata watu.

  Ili muheshimiwa apite asibughuziwe.

  Wameona hiyo ndio njia sahihi ya kuwatawanya wananchi but hali halisi walikuwa wafunge barabara wakatu mkuu anaporejea kutoka butihama ili wamweleze kilio chao kwanini serikali yake haiwatendei haki hao wakaazi wa huku Kipawa.

  Kwasababu amechoka anahitaji kupunzika

  Umuhimu wake ni kupita kwenda Ikulu .......

   
 11. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  >Kuna siku yaja lakini hatuijui, Inshallah<
   
 12. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  lakini watalipwaje kwa sheria mpya wakati uamuzi umefanyika kwa sheria ya zamani? wenye kufahamu sheria nifafanulieni tafadhali...
   
 13. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #13
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Ahsante kwa taarifa mkuu BornTown.

  Inasikitisha lakini ndivyo ilivyo! Tanzania zaidi ya unavyoijua
   
 14. M

  Msharika JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani wananchi msikubaliane na lolote , huyo bwana msanii, tumieni kura zenu vizuri 2010 kumadabisha, manyanyaso kwa wananchi yamezidi. Kwanini mlipwe kwa sheria ya 1967 na kunasheria mpya ya malipo 2002? Wizi mtu, wanatafuta hela za campaign 2010 wawanunulie kanga na kofia kwa hela zenu, zichukueni au ********** ila angalia ametoka safari hivyo amechoka.
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kusema ukweli hii nchi inamaudhi sana wakati mwingine unaweza kukasirishwa ukajiuliza hivi hii nchi yenye sifa kwa wenzetu wanayo yafanya hi ya haki. Mfano hawa jirani zangu hapa kipawa wanataka kuwalipa fidia ya mwaka 1967 !!!!! kweli hii hi haki maana wakati sheria ya mwaka 67 inatungwa laki moja ya pesa ilikuwa ni nyingi sana mtu waweza nunu hata na gari ukajenga nyumba yako na balance ikabaki kubwa tu ya kutunza heshima mtaani.

  Karne hii ya sasa mfuko mmoja wa simenti unauzwa sh. 14500/ ukitaka kujenga nyumba ya vyumba viwili vya kulala na kajisebule potelea mbali kule posta tukakuweka nje na kuzungushia magunia n kikawa cha passport size.
  uje upewe shilingi laki 5 utazifanya nini?
   
 16. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  pole SINKALA, kama nakuona vile unalia kuna bomu limeanguka mbele yako au nakufananisha?
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Mbeya, Mawe na Kuzomewa ....Leo tena kazuiwa

  I am Smelling French Revolution very soon than later, wananchi tumechoka!
   
 18. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  kwasababu walijafanyiwa tena tasmni upya nadhani ilikuwa mwaka jana mwanzoni na kama walikuwa wanlijua hilo kwania kipindi kile (awamu ya kwanza) waliposema wanataka kupanua kiwanja hawakuwalipa kipindi kilekile waje wawatese weeeee halafu waseme wanwalipa now hii sio haki.
  geuza upande wapili wa shilingi ungekuwa wewe ungefanyaje??
   
 19. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,447
  Likes Received: 7,187
  Trophy Points: 280
  msg sent na bado watanzania si mabwege tena
   
 20. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Yaani Afrika yatupasa kumwomba MUNGU sana atuponye na hii laana iliyoko juu la bara letu. Unyonyaji na dhuluma kila mahali. Maana kama kuna sheria mpya iweje wawalipe kwa sheria ya mwaka 1967 ambapo USD 1 ilikuwa sawa na Ths 1 kama si 2 Tshs. (mwenye takwimu sahihi anisahihishe). Ina maana watapunjwa kwa kama 650% hadi 1300 % hivi. Huu ni wizi mkubwa unaotaka kufanywa na serikali isiyojali watu wake. May GOD forbid.
   
Loading...