Kitilya, wenzake waendelea kusota rumande

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
kesi+pic.jpg

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na dhamana (Egma), Harry Kitilya na waliokuwa maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon bado wanaendelea kusota rumande kutokana na upelelezi wa kesi inayowakabili bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi ameeleza mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa leo Ijumaa kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Pia ameeleza kuwa bado wanasubiri awamu ya pili ya upelelezi kutoka nchini Uingereza, kutokana na hilo ameomba kesi hiyo ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya ombi hilo Hakimu Mwambapa ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 10, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Mwananchi
 
Msiwabolee watu wa Mwanza ndio walio nipa......
 
Uhujumu uchumi dhamana hakuna lakini tuangalie upya huyu alikuwa kamishna wa mamlaka t.r.a angetaka kuwa mwizi nafikiri ndo angekuwa mwizi nomber moja hawa walioko madarakani kuna kitu tunawafundisha tuwe makini tunapoweka watu ndani uadilifu utatoweka mzee mkapa na kikwete walimwamini sana huyu mzee kitilya nasema ukifikia kustaafu na ulikuwa mwadilifu ukikaa mtaani utajua vitu na utajuta ukisema ningejua mstaafu anakula mafao gerezani upelelezi ukamilike mzee muadilifu atoke ni maoni yangu hayo
 
Now its too much!!

Wanatia huruma nilifikiri walisha toka.
 
Tanzania buana, mtuhumiwa anakamatwa kwanza,upelelezi ndo unaanza akiwa jela... What if akija onekana hana kosa na mahakama kumwachia huru, will the Government pay the damage to rebuild their reputation???
Mtuhumiwa anafichwa eti ni ili asije kuharibu ushahidi!
 
Tanzania buana, mtuhumiwa anakamatwa kwanza,upelelezi ndo unaanza akiwa jela... What if akija onekana hana kosa na mahakama kumwachia huru, will the Government pay the damage to rebuild their reputation???
Kukaa rumande ni kwa usalama wao mkuu
 
Back
Top Bottom