Na Ezekiel Kamwaga
Kitila, Zitto na Ado: The Story
Hii ni hadithi kuhusu wanasiasa watatu maarufu hapa nchini ambao wanatambulika kwa majina yao ya kwanza badala ya yale ya ubini. Katika siasa hii ni kete muhimu kwa sababu si wanasiasa wote hubaki kujulikana kwa majina yao ya kwanza hata baada ya miaka mingi ya kutumikia umma.
Hapo mwanzo, Kitila alikuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO). Mwaka 1999, DARUSO walipata ugeni kutoka Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). Mmoja wa wageni hao alikuwa kijana aliyeitwa Zitto Zuberi Kabwe; aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wanafunzi wa SUZA.
Akiwa Sekondari ya Kibohehe, Kilimanjaro, Zitto alipata alama A nane katika Mitihani ya Form Four. Alipata A katika msomo magumu kama Hisabati, Kemia, Fizikia na Biology. Alikuwa kijana mwenye akili nyingi.
Baada ya kukutana na kuzungumza, Kitila akabaini kwamba amekutana na kipaji kikubwa cha uongozi. Akamwambia Zitto; "Wewe unapoteza muda SUZA, njoo UDSM utumie uwezo wako vizuri. Nitakusaidia."
Zitto alienda kusoma Zbar kwa sababu hakutaka kukaa mwaka mzima kusubiri kujiunga na UDSM. Lakini alikuwa ameomba pia kujiunga na chuo hicho. Kitila alipoenda kutazama, akabaini kwamba Zitto aikuwa amepata nafasi UDSM. Akamshawishi Zitto aache SUZA aje UDSM. Zitto akakubali.
Kitila akawa rafiki yake wa kwanza chuoni. Wakaendana. Wakawa maswahiba.
The Rest, as they, Is History.
Takribani muongo mmoja baadaye, Kitila huyohuyo - sasa akiwa Mhadhiri wa UDSM na mmoja wa wasomi mashuhuri nchini, akashuhudia kipaji kingine kikiibuka katika siasa za wanafunzi za UDSM.
Kijana huyo akajipambanua kwa uwezo wa kujenga hoja, uchapakazi na uungwana. Kitila akamwona na akachukua jukumu la kumfunda (Mentor) kijana huyo. Akamfanya aamini kwamba anaweza kuwa na mchango akiingia kwenye ulimwengu wa siasa.
Kwa sababu ya mrengo wake wa kijamaa, kijana huyo akajitosa katika chama cha ACT Wazalendo. Akaanza kazi kwa kujitolea. Akapokewa na Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe; yule swahiba wa Kitila wa muongo mmoja uliopita.
Alipopewa wadhifa wa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, kuna waliobeza kwamba kijana huyo hatamudu mikiki ya siasa rasmi. Leo hii, kijana huyo, Ado Shaibu, ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho.
Sina hakika kama Zitto au Ado wangekuwa hivi walivyo pasipo kukutana na Kitila katika wakati muhimu kwenye Maisha yao.
Inawezekana Kitila Mkumbo tayari ametoa mchango mkubwa katika siasa za Tanzania kuliko vile ambavyo tunafahamu sasa.
Mwenyezi Mungu amemjalia uwezo wa kung'amua vipaji mahiri pale anapoviona. Lakini pia kajaliwa uwezo wa kulea na kukuza vipaji hivyo.
Hii si tabia ya Kitanzania. Wengi wetu hupenda sisi ndiyo tubaki juu miaka yote na wengine kubaki juu.
Nataka kusema neno moja leo; Hooooraaaayyyy to Professor Kitila Alexander Mkumbo.
Heri kwa Walezi na Wakuzaji
Ezekiel Kamwaga
Dar