Kitila Mkumbo zaidi ya umjuavyo

Kitila Mkumbo zaidi ya umjuavyo

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,408
Reaction score
3,269
Na Ezekiel Kamwaga

Kitila, Zitto na Ado: The Story

Hii ni hadithi kuhusu wanasiasa watatu maarufu hapa nchini ambao wanatambulika kwa majina yao ya kwanza badala ya yale ya ubini. Katika siasa hii ni kete muhimu kwa sababu si wanasiasa wote hubaki kujulikana kwa majina yao ya kwanza hata baada ya miaka mingi ya kutumikia umma.

Hapo mwanzo, Kitila alikuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO). Mwaka 1999, DARUSO walipata ugeni kutoka Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). Mmoja wa wageni hao alikuwa kijana aliyeitwa Zitto Zuberi Kabwe; aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wanafunzi wa SUZA.

Akiwa Sekondari ya Kibohehe, Kilimanjaro, Zitto alipata alama A nane katika Mitihani ya Form Four. Alipata A katika msomo magumu kama Hisabati, Kemia, Fizikia na Biology. Alikuwa kijana mwenye akili nyingi.

Baada ya kukutana na kuzungumza, Kitila akabaini kwamba amekutana na kipaji kikubwa cha uongozi. Akamwambia Zitto; "Wewe unapoteza muda SUZA, njoo UDSM utumie uwezo wako vizuri. Nitakusaidia."

Zitto alienda kusoma Zbar kwa sababu hakutaka kukaa mwaka mzima kusubiri kujiunga na UDSM. Lakini alikuwa ameomba pia kujiunga na chuo hicho. Kitila alipoenda kutazama, akabaini kwamba Zitto aikuwa amepata nafasi UDSM. Akamshawishi Zitto aache SUZA aje UDSM. Zitto akakubali.

Kitila akawa rafiki yake wa kwanza chuoni. Wakaendana. Wakawa maswahiba.

The Rest, as they, Is History.

Takribani muongo mmoja baadaye, Kitila huyohuyo - sasa akiwa Mhadhiri wa UDSM na mmoja wa wasomi mashuhuri nchini, akashuhudia kipaji kingine kikiibuka katika siasa za wanafunzi za UDSM.

Kijana huyo akajipambanua kwa uwezo wa kujenga hoja, uchapakazi na uungwana. Kitila akamwona na akachukua jukumu la kumfunda (Mentor) kijana huyo. Akamfanya aamini kwamba anaweza kuwa na mchango akiingia kwenye ulimwengu wa siasa.

Kwa sababu ya mrengo wake wa kijamaa, kijana huyo akajitosa katika chama cha ACT Wazalendo. Akaanza kazi kwa kujitolea. Akapokewa na Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe; yule swahiba wa Kitila wa muongo mmoja uliopita.

Alipopewa wadhifa wa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, kuna waliobeza kwamba kijana huyo hatamudu mikiki ya siasa rasmi. Leo hii, kijana huyo, Ado Shaibu, ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho.

Sina hakika kama Zitto au Ado wangekuwa hivi walivyo pasipo kukutana na Kitila katika wakati muhimu kwenye Maisha yao.

Inawezekana Kitila Mkumbo tayari ametoa mchango mkubwa katika siasa za Tanzania kuliko vile ambavyo tunafahamu sasa.

Mwenyezi Mungu amemjalia uwezo wa kung'amua vipaji mahiri pale anapoviona. Lakini pia kajaliwa uwezo wa kulea na kukuza vipaji hivyo.

Hii si tabia ya Kitanzania. Wengi wetu hupenda sisi ndiyo tubaki juu miaka yote na wengine kubaki juu.

Nataka kusema neno moja leo; Hooooraaaayyyy to Professor Kitila Alexander Mkumbo.

Heri kwa Walezi na Wakuzaji

Ezekiel Kamwaga
Dar
 
Kitila ni mtu mwema na anayejielewa. Ni moja ya watanzania wachache wanaopenda kuona wengine wakifanikiwa. Ni mtu anayependa kujenga hoja lakini pia kusikiliza wengine bila kuwabeza. Hilo peke yake ni sifa bora na ya kipekee kwa jamii ya kitanzania.

Kuhusu mrengo wa kijamaa;

Ukweli ni kwamba mrengo wa kijamaa ni mrengo ulioshindwa duniani. Hata katika nchi ambazo watu wake wana nidhamu, mrengo huo umeshindwa.

ACT haikuanzishwa kama chama cha kijamaa bali chama cha mrengo wa kati kushoto. Kwa bahati mbaya watanzania wengi wakiwemo hata viongozi wa vyama hawaelewi mambo hayo ya mirengo achilia mbali kuifuata.

ACT - Ilianzishwa ikiwa na misingi 10. Sijui kama kuna hata mmoja ambao wanafuata kwa sasa. Kwa bahati mbaya ni kwamba chama kikishaacha kufuata misingi hakuna namna ambayo kinaweza kukwepwa kupoteza muelekeo na kuangukia kwenye mikono ya watu binafsi ambao watakiendesha wapendavyo.
 
Na Ezekiel Kamwaga

Kitila, Zitto na Ado: The Story

Hii ni hadithi kuhusu wanasiasa watatu maarufu hapa nchini ambao wanatambulika kwa majina yao ya kwanza badala ya yale ya ubini. Katika siasa hii ni kete muhimu kwa sababu si wanasiasa wote hubaki kujulikana kwa majina yao ya kwanza hata baada ya miaka mingi ya kutumikia umma.

Hapo mwanzo, Kitila alikuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO). Mwaka 1999, DARUSO walipata ugeni kutoka Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA). Mmoja wa wageni hao alikuwa kijana aliyeitwa Zitto Zuberi Kabwe; aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wanafunzi wa SUZA.

Akiwa Sekondari ya Kibohehe, Kilimanjaro, Zitto alipata alama A nane katika Mitihani ya Form Four. Alipata A katika msomo magumu kama Hisabati, Kemia, Fizikia na Biology. Alikuwa kijana mwenye akili nyingi.

Baada ya kukutana na kuzungumza, Kitila akabaini kwamba amekutana na kipaji kikubwa cha uongozi. Akamwambia Zitto; "Wewe unapoteza muda SUZA, njoo UDSM utumie uwezo wako vizuri. Nitakusaidia."

Zitto alienda kusoma Zbar kwa sababu hakutaka kukaa mwaka mzima kusubiri kujiunga na UDSM. Lakini alikuwa ameomba pia kujiunga na chuo hicho. Kitila alipoenda kutazama, akabaini kwamba Zitto aikuwa amepata nafasi UDSM. Akamshawishi Zitto aache SUZA aje UDSM. Zitto akakubali.

Kitila akawa rafiki yake wa kwanza chuoni. Wakaendana. Wakawa maswahiba.

The Rest, as they, Is History.

Takribani muongo mmoja baadaye, Kitila huyohuyo - sasa akiwa Mhadhiri wa UDSM na mmoja wa wasomi mashuhuri nchini, akashuhudia kipaji kingine kikiibuka katika siasa za wanafunzi za UDSM.

Kijana huyo akajipambanua kwa uwezo wa kujenga hoja, uchapakazi na uungwana. Kitila akamwona na akachukua jukumu la kumfunda (Mentor) kijana huyo. Akamfanya aamini kwamba anaweza kuwa na mchango akiingia kwenye ulimwengu wa siasa.

Kwa sababu ya mrengo wake wa kijamaa, kijana huyo akajitosa katika chama cha ACT Wazalendo. Akaanza kazi kwa kujitolea. Akapokewa na Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe; yule swahiba wa Kitila wa muongo mmoja uliopita.

Alipopewa wadhifa wa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo, kuna waliobeza kwamba kijana huyo hatamudu mikiki ya siasa rasmi. Leo hii, kijana huyo, Ado Shaibu, ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho.

Sina hakika kama Zitto au Ado wangekuwa hivi walivyo pasipo kukutana na Kitila katika wakati muhimu kwenye Maisha yao.

Inawezekana Kitila Mkumbo tayari ametoa mchango mkubwa katika siasa za Tanzania kuliko vile ambavyo tunafahamu sasa.

Mwenyezi Mungu amemjalia uwezo wa kung'amua vipaji mahiri pale anapoviona. Lakini pia kajaliwa uwezo wa kulea na kukuza vipaji hivyo.

Hii si tabia ya Kitanzania. Wengi wetu hupenda sisi ndiyo tubaki juu miaka yote na wengine kubaki juu.

Nataka kusema neno moja leo; Hooooraaaayyyy to Professor Kitila Alexander Mkumbo.

Heri kwa Walezi na Wakuzaji

Ezekiel Kamwaga
Dar
Kitila Mkumbo

Muasisi wa uasi wa mapinduzi ya kweli
 
Kwenye huu uzi mmoja Kitila ametumia IDs tatu.anaji support kwa uzi aliojianzishia....😂😂😂😂😂
Sisi inatusaidia nini, aende kwa WANYONGE kule anapotaka kugombea ndiyo akawaeleze.
 
Back
Top Bottom