Kitila Mkumbo: Wapinzani wa Tanzania wana ugonjwa wa kupinga kila kitu, apongezwa kupona ugonjwa huo

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,704
36,461
Katibu mkuu wa wizara ya maji, uvuvi na umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo ameibuka baada ya ripoti ya pili ya sakata la mchanga na kudai kuwa wapinzani wa Tanzania wanaugua ugonjwa wa kupinga kila kitu na kwamba wanatakiwa kumuunga mkono rais Magufuli kuokana na sakata la mchanga. Ameyatoa hayo katika moja ya akaunti zake za mitandao ya kijamii.

Aidha baada ya kutoa maoni hayo na kuwataka wapinzani kumpongeza rais Magufuli, wameibuka mashabiki wake na kumpongeza kwa kupona ugonjwa huo.

"Hongera sana ndugu Kitila, hatimaye tumegundua kuwa daktari mzuri wa kuponya ugonjwa wa kupinga kila kitu ni serikali, naona kuwa umepona kabisa baada ya kuingia kwenye matibabu ya serikali". Wameandika baadhi ya mashabiki wake wakihashiria kumpongeza.
 
Hawa ndio wakitumbuliwa wanaanza kulia kama watoto wadogo..muda utasema tu..hutakaa hapo milele..mnafiki mkubwa wèwe
 
Prof. Kitila namjua vizuri, hajawahi kuwa mpinga kila kitu wala kukubali kila kitu. Huwa anapenda kuchallenge lakini pia anapenda kuwa challenged. Mimi mwenyewe nishawahi kumchallenge Mara kadhaa na akanielewa.

Lamsingi tu uwe na hoja sio kushout!
 
Kweli naona dakitari wa kumtibu kapatikana. Kuukwaa ukuu sio mchezo. Utaacha kumsifia banyani pamoja na ubaya wake. ila kiatu chake dawaaa
 
Prof. Kitila namjua vizuri, hajawahi kuwa mpinga kila kitu wala kukubali kila kitu. Huwa anapenda kuchallenge lakini pia anapenda kuwa challenged. Mimi mwenyewe nishawahi kumchallenge Mara kadhaa na akanielewa.

Lamsingi tu uwe na hoja sio kushout!
Huyu ni mkumbo mpya sio yule unayejua siku akikosoa serikali ya CCM ntakutumia pesa m pesa
 
Yea huo ugonjwa ili mtu apone ni kupitia dawa mujarab iitwayo uteuzi.

Mkumbo na Mghwira washalamba hiyo dawa. Na wamepona.

Ujinga na unafiki unalimaliza taifa.
 
Kitila mkumbo hana jipya lolote, tumbo linamsumbua tu
Kitila in miongoni mwa watanzania wachache ambao no very resourceful. No MTU ambaye no very rational and flexible. Kabla hukauona udhaifu was mwenzako, unatakiwa kujiuliza we we una ujuzi gani kumzidi.
 
904875966199201ad7de6cfb2c7ec5f1.jpg
 
Kukosoa sio sifa, sofa kubuni au kutenda
Inategemea swala limekosewa katika ngazi ya URAIS huwez kubuni na kutenda, unakosoa alafu Rais anatenda kama mwakilishi kwenye hiyo ngazi, ukosoaji umeleta changamoto ya utendaji na ubunifu.
 
Inategemea swala limekosewa katika ngazi ya URAIS huwez kubuni na kutenda, unakosoa alafu Rais anatenda kama mwakilishi kwenye hiyo ngazi, ukosoaji umeleta changamoto ya utendaji na ubunifu.
Kwa mini usishauri namna ya kuboresha kama Luna maboresho yanahitajika?
 
Back
Top Bottom