Kitila Mkumbo, Mulika watendaji DAWASCO Kawe, wanaichonganisha Serikali na Wananchi

Loxodona

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
354
618
Kwanza nianze kwa kuipongeza Serikali Kwa kutusambazia maji katika eneo leo. Pamoja na Nia njema ya Serikali kutupatia maji. Baadhi ya watendaji wa Dawasco wamekuwa wakikwamisha juhudi za Serikali kusambazia maji wananchi wake.

Kwa Muda wa Mwezi sasa baadhi ya wakazi wa Mbezi Juu tumekuwa tukipewa Story nyiiiiingi na Watendaji wa Dawasco - Kawe badala ya Maji. Zoezi la ugawaji maji huku juu limegubikwa na ubaguzi na ubabaishaji mkubwa.

Kabla ya mtendaji wa Dawasco wa sasa hapo Kawe hakukuwepo na ubaguzi katika ugawaji maji. Tunampongeza Sana Dada Judithi H. Singinika, Regional Manager - Dawasco Kawe. Kwa kutimiza wajibu wake bila upendeleo katika kipindi chake.

Cha kushangaza, wanaosambaza Maji Kwa Malori wao wanapewa maji Sisi wa Majumbani maji hatupati. Inamana maji toka Ruvu, yanaubaguzi??Kuna fufunu kuwa wenye Malori wanawezesha watendaji wa Kawe ili wasifungue maji Kwa wananchi ili wenye Mabowser waweze kuuza maji.

Tunakuomba ufwatilie suala hili hapo Kawe mana ubabaishaji huu umekuwa ukiwatesa Sana wananchi wengi wanyonge wanaoishi maeneo haya kwani ndoo ya Maji inauzwa Hadi TZS 500 inapotokea crisis hii ya kukatika Kwa maji Kwa muda mrefu. Naomba wenye contacts za Katibu Mkuu Mkumbo waweke hapa ili tuweze kumfikishia ujumbe huu kirahisi na Kwa haraka kwani ni shida Sana.
 
Exactly! Kitila Mkumbo hii Taasisi itawakosanisha na Wananchi kama juhudi za maksudi hazitachukulkwa. Maji ni Uhai na yanamgusa kila mwananchi. Hivyo ubabaishaji kwenye huduma hii ni hatari.
 
Back
Top Bottom