Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Professa Kitila Alexander Mkumbo leo Septemba 12, 2025 amefanya kampeni za aina yake kwa kuomba kura kwa abiria walio ndani ya Daladala zilizokuwa zinachukua abiria katika Kituo cha Riverside, Ubungo Dar Es Salaam.
Kitila ambaye anaomba ridhaa ya kuwawakilisha wananchi wa jimbo hilo kwa mara ya pili aliwaomba abiria waliokuwa katika usafiri huo kumpigia kura Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akijiombea kura na yeye.