'Kiti moto' ni salama

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,302
Likes
37,954
Points
280

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,302 37,954 280
WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk John Magufuli amesisitiza tamko la serikali kuwa nyama ya nguruwe, maarufu kama Kiti Moto, ni salama kwa kuwa hakuna taarifa za kuathirika kwa wanyama hao.

Kuibuka kwa ugonjwa wa Mafua ya Nguruwe kulisababisha hofu kubwa nchini mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuua watu nchini Mexico, hata hivyo serikali iliwatoa hofu wananchi kwa kueleza kuwa nguruwe wa Tanzania hawajaathirika na kwamba ugonjwa huo unaambukiza kwa hewa na si kula nyama hiyo maarufu nchini.

Mwishoni mwa wiki, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk John Magufuli alikuwa na kazi nyingine ya kuihakikishia Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Kilimo na Mifugo kuhusu wanyama hao.
"Nguruwe wako salama," alisema Dk Magufuli kwenye kikao cha kamati hiyo jijini Dar es salaam.

"Kama wangekuwa wana matatizo na kuathirika na homa hiyo hadi sasa tungekuwa tumepiga marufuku ulaji wake kwa wananchi.

"Kwa hiyo wanaokula waendelee kula na wapo wanaendelea lakini wasiokula kama mimi tunaoita haramu, tusile."

Alifafanua kwamba, wizara yake imekuwa katika mchakato wa kutekeleza Sera ya Taifa ya Mifugo ya mwaka 2006 na kuongeza kwamba rasimu ya mwisho ya mkakati huo imeandaliwa.

Dk Magufuli aliongeza kwamba waraka wa Baraza la Mawaziri wa kupitisha mkakati huo umewasilishwa kwa katibu mkuu wa baraza hilo.

Rasimu hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuboresha mazao yote ya mifugo ili yaweze kuwa salama zaidi kwa mlaji. Mwishoni mwa mwaka jana, Tanzania ilikumbwa na tishio kubwa la homa ya mafua ya nguruwe na kufanya hata baadhi ya shule nchini hasa mkoani Mwanza kufungwa kwa muda.

Magufuli.jpg
WAZIRI wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk John Magufuli ambaye amesisitiza kuwa nyama ya Nguruwe maarufu kwa jina la 'Kiti moto' iko salama, hivyo wananchi waitumie kama kawaida
 

darcity

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2009
Messages
3,962
Likes
5,506
Points
280

darcity

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2009
3,962 5,506 280
Kipindi hiko alikuwa bingwa wa kuhesabu idadi ya samaki baharini, mitoni, miferejini mpaka ziwani hadi mayai na watoto wa samaki!

Sasa ni bingwa wa kuhesabu kodi.Nil
 

Forum statistics

Threads 1,189,736
Members 450,798
Posts 27,645,707