Swali, Kamati ya Bunge, Huduma za Kijeshi: Umewahi kutamka kwamba kundi la ushawishi la Wayahudi linatisha watu wengi sana hapa, na kwamba wewe sio Mbunge wa Israel wewe ni Mbunge wa Nebraska, na kwamba hili shinikizo linafanya watu wafanye mambo ya kipumbavu saa nyingine. Taja mtu mmoja kwa mawazo yako ambae anatishwa na kundi la ushawishi la Israel kwenye Bunge la Marekani.
Chuck Hagel, Waziri wa Ulinzi Mteule wa Obama: Aah, kwanza kabisa
Swali: Taja mmoja!
Hagel: Sijui
Swali: Kwa nini ulisema?
Hagel: Sikuwa na mtu kichwani niliemmaanisha
Swali: Unakubali kwamba ni maneno ya kichokozi na hakuna maneno ya kichokozi kuzidi hayo kuhusu uhusiano wetu na Israel na Bunge hili? Taja kitu kimoja cha kipumbavu ambacho tumesukumwa kufanya na kundi la ushawishi la Israel
Hagel: Nimesema nasikitika
Swali: Lakini ulitamka kwamba wanatufanya tufanye mambo ya kipumbavu, huwezi kutaja Mbunge mmoja anaetishwa, basi nipe mfano mmoja wa kitu cha kipumbavu ambacho tunashinikizwa kufanya hapa.
Hagel: Kwenye ule usaili nilikua naongelea...
Swali: Sawa, nipe mfano ambapo tumetishwa na kundi la ushawishi la kiyahudi la Israel kufanya kitu cha kipumbavu kuhusu Mashariki ya Kati, Israel au popote
Hagel: Siwezi
Swali: Ahsante, unakubaliana na mimi kwamba usingesema kitu kama hicho?
Hagel: Ndio nilichemka, nimeshasema hivyo.
========================================================
Kwa maoni yangu, inatia moyo kusikia wabunge wa Wamarekani wanapinga na kukasirishwa na nadharia ya kwamba Marekani inapelekeshwa puta na Israel, japo inawezekana ni kweli. Na nitafurahi Hagel akipita kwa sababu haamini katika upuuzi wa "Taifa Teule" wala kuifagilia fagilia Israel, japo ni Mkristo kama mimi.