Kiteto, Siha hakukaliki

Kiteto, Siha hakukaliki

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,795
Reaction score
5,252
WAFUGAJI zaidi ya 800 wa jamii ya kimasai wamevamia eneo la wawekezaji wa kampuni ya utalii ya Tanganyika Film and Safary lililopo kijiji cha miti Mirefu na kuharibu mali mbali mbali zikiwemo nyumba 16 na magari tisa.

Katika tukio hilo wafugaji hao wanaosadikiwa kutoka Longido mkoani Arusha na Siha na kuweka kambi katika vijiji vitano vinavyozunguka eneo la mwekezaji wilayani humo mbali na kufanya uharibifu huo pia wanadaiwa kuingiza mifugo katika mashamba nane ya Ndarakwai na kuharibu mali ikiwamo kambi za watalii.

Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro,Geofrey Kamwela aliahidi kutoa taarifa juu ya tukio hilo baada ya kufanyika vikao vya pande mbili ikiwamo ya wafugaji na serikali wilaya ya Longido na Siha.

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mitimirefu, Israel Kileo tukio hilo lilitokea juzi saa 7 mchana, baada ya wafugaji kudaiwa kuingiza mifugo katika mashamba ya mwekezaji huyo kwa madai ya kukosa eneo la malisho katika maeneo ya vijijini.

Jana (juzi) mchana nilipewa taarifa ya kuwapo kwa vurugu ambazo zilisababisha wafugaji kuchoma nyumba,magari na mali nyingine za mwekezaji, pia kulikuwa na taarifa ya mtu kujeruhiwa kwa kupigwa risasi, alisema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Leonidas Gama alisema, serikali imesikitishwa na tukio hilo na kutaka jeshi la polisi kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote waliotenda tukio hilo.

Alisema kama serikali ikilifumbia macha jambo hilo,huenda likawakatisha tamaa wawekezaji, kwani mwekezaji huyo pamoja na shughuli zake lakini pia amekuwa akisaidia katika miradi ya kijamii kama Elimu na Afya.

Gama alisema chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha wafugaji kutafuta eneo la malisho kutokana na wingi wa mifugo waliyonayo na hali ya ukame uliopo sasa

Taarifa tulizonazo ni kwamba hadi sasa wafugaji wamepeleka mifugo zaidi ya 300 katika mashamba ya mwekezaji, Yule ametunza eneo analomiliki lina mazingira mazuri na kuna ranchi kwa ajili ya aina zaidi ya 65 za wanyama pori na ndege zaidi ya 300 wa aina mbalimbali, alisema.

Alisema eneo hilo limetoa ajira kwa wananchi zaidi ya 76 za kudumu na muda maalum huku pia kukiwa na ajira za watu 20 kila siku jambo ambalo pia linaimarisha hali za kiuchumi za wananchi wa vijiji vinavyozunguka.

Gama alisema eneo la mwekezaji linapokea zaidi ya watalii 2500 hadi 3000 kwa mwaka jambo ambalo linachangia mapato ya mkoa na taifa kwa ujumla na kwamba serikali haiwezi kukubali kupotea kwa wageni hao.

Mwekezaji wa kampuni hiyo,Peter Jones alikiri, kupata hasara ya mamilioni ya shilingi na kuongeza kuwa taarifa kamili ataitoa baada ya kufanya tathmini ya kina.

Alisema wafugaji hao walivamia eneo lake majira ya saa saba na kuathiri watalii wane ambao iliwalazimu kuwahamisha na kuwapeleka mkoani Arusha kwa ajili ya usalama wao huku kampuni ikilazimika kusitisha safari za watalii 10 kutoa nchi za Uingereza na Marekani waliopaswa kuja mwaka huu.

Naye kiongozi wa wafugaji katika kijiji cha kitendeni na Mitimirefu, Kitasho Simeli alisema, chanzo cha vurugu hizo ni kitendo cha askari kuwapiga risasi wachungaji hao na kuwatelekeza porini.

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametaka viongozi wa wilaya ya Kiteto na mkoa wa Manyara kuwajibishwa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya wakulima na wafugaji

Dk. Slaa alisema mauaji yanayotokea mara kwa mara wilayani Kiteto yanayosababishwa na migogoro ya ardhi yanaonyesha kushindwa kuwajibika kwa viongozi

Akizungumza na Tanzania Daima Jumapili, jana Dk. Slaa, alisema kutwa ya jana amekuwa akipokea simu lukuki zikimtaarifu hali ni mbaya na watu wanaendelea kupoteza maisha kutokana na mapigano kati ya wakulima na wafugaji kugombea ardhi, huku serikali ikiwa kimya na Watanzania hawajui.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, hadi jana mchana alikuwa amepewa taarifa watu wanane wamepoteza maisha katika Kata ya Matui na Olporotu, ingawa amewasiliana na IGP Ernest Mangu, aliyemthibitishia kuwa Polisi wako wilayani humo.

Mgogoro huo unaondelea una sura ya ukabila na unaendekezwa na viongozi wa kisiasa ambao ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ambao wana maslahi yao binafsi, alisema

Juzi Mkuu wa Mkoa RC Erasto Mbwilo, alifika huko wakamwambia kuna Masai wamezunguka maboma, badala ya kuchukua hatua akawaambia nendeni mkawaambie watawanyikendio maana nasema wameshindwa kuwajibika na nchi haina dira hivi sasa.

Alisema kazi ya serikali ni kuwahakikishia mazingira na haki ya kuishi wananchi, jambo viongozi hao wameshindwa kulisimamia na kumtaka Rais Jakaya Kikwete awatimue.

Amani haihubiriwi ila inatengenezewa mazingiramimi nashangaa sana ninapowasikia viongozi wa serikali tena wakubwa kabisa katika chombo kimoja cha habari wakihubiri amani, amani inatengenezewa mazingira, bila hivyo haki ya kuishi haiwezi kuwepo na ndicho kinachotokea Kiteto.

Haki ya kuishi hivi sasa haipo, wakulima na wafugaji hawakuandaliwa nani akae wapi na afanyie shughuli zake wapi. Serikali inashindwa kuweka mazingira ili haki ya kuishi iwepo, alisema.

Dk. Slaa, alisema Mkuu wa Wilaya, Martha Umbulla, ameshindwa kuwajibika muda mrefu kuondoa matatizo ya ardhi katika Wilaya hiyo, lakini amekuwa akiachwa.

Yule mama Mkuu wa Wilayatena alikuwa ni Mbunge mwenzangu, tunafahamiana na ni kabila langu. Hana uwezo Rais Kikwete anambeba, amuondoe ameshindwa kulinda amani, amekuwa akibagua na kuegemea ukabila, RC naye awajibishwe, alisisitiza.

Alibainisha kuwa, matatizo yanayotokea Kiteto yanatokana na vigogo kujilimbikizia ardhi, ngombe wengi na kumiliki ranchi kubwa hivyo kuona wakulima hawatakiwi

Tanzania hatupaswi kuwa na viongozi waoga, lazima maslahi ya pande zote yaangaliweangalia kuna Wizara ya Ardhi na Makazi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na ile ya Maliasili na Utalii, lakini wanashindwa kukaa pamoja kutatua matatizo kama haya ambayo pia tunayashuhudia Mvomero, Kilosa na kwingineko, alisema na kuongeza.

Tuna taarifa na ahata vyombo vya habari kuwahi kuripoti, serikali ilichangisha Wamasai mitamba kwa madai ya kupata fedha walizowaambia ni za kuwaondoa wakulima kwenye maeneo yao ili wapate sehemu za malisho, jambo ambalo halijafanyika, hivyo wafugaji kuamua hivi sasa kujichukulia hatua mkononi.

Kazi ya serikali ni kuhakikisha inalinda haki ya watu wake kuishi, lakini imeshindwa kuwajibika, utu umewekwa pembeni, Serikali haijali, alisema.

Kutokana na hali ya hatari Kiteto, maofisa kadhaa wa juu wa Jeshi la Polisi wamepelekwa huko kuhakikisha usalama unakuwepo, huku ikiripotiwa baadhi ya watu kuzikimbia kaya zao wakihofu mauaji na kukamatwa kuhusiana na mauaji hayo
 
serikali hii ipo kama haipo.....inafanya mpaka inatokea mkanyagano kati ya wakulima na wafugaji
viongozi wabovu wanabebwa sana shyttt hawafanyi lolote ku solve matatizo hayo
 
Nilisoma jana Michuzi Blog kuwa waziri mkuu amesema sasa mapigano ya wafugaji na wakulima basi. kauli hii aliitoa katika kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge jana, kikao ambacho jasho la walipa kodi ambao ni wakulima na wafugaji wamelipa kwa ajili ya maendeleo ya nchi lakini wao wanajilipa posho kwa ajili ya kutoa majibu mlainisho kama hayo. simple like that bila kusema wamejipanga vipi kukabiliana na suala hilo au ni mbin zipi mbadala na zile za awali, kwa Kauli ya pinda nikilinganisha na yale mauaji ya walemavu wa ngozi napata jibu rahisi kuwa huyu bwana anatishia kumwaga chozi mwisho wa siku.
 
Nilisoma jana Michuzi Blog kuwa waziri mkuu amesema sasa mapigano ya wafugaji na wakulima basi. kauli hii aliitoa katika kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge jana, kikao ambacho jasho la walipa kodi ambao ni wakulima na wafugaji wamelipa kwa ajili ya maendeleo ya nchi lakini wao wanajilipa posho kwa ajili ya kutoa majibu mlainisho kama hayo. simple like that bila kusema wamejipanga vipi kukabiliana na suala hilo au ni mbin zipi mbadala na zile za awali, kwa Kauli ya pinda nikilinganisha na yale mauaji ya walemavu wa ngozi napata jibu rahisi kuwa huyu bwana anatishia kumwaga chozi mwisho wa siku.

wafugaji na wakulima lazima wafahamu adui # 1 ni serikali na viongozi wake wote, wao ndiyo wanalea na kuchochea matatizo haya...mpaka watu wana uwana.
wao hawafanyi lolote wameweka as@s zao tu kazi kupiga mdomo, no action taken ya kusaidia matatizo haya ambayo ni ya muda.
ushauri wangu-wakulima na wafugaji wangenda hadi kwa mkuu wa wilaya au mkoa , police wawaonyeshe uchungu wao maana wana mwaga damu inayopotea bila sababu...wakat kuna viongozi was $@## tu wamekaaaaa tu hawajali
 
Serikali ya kudeal na matukio. Badala ya kuzuia kitu kabla hakija tokea, ona Kiteto leo viongozi wanakimbilia huko as if hiki kitu ni cha jana. Mh Lema alizungumza mapema sana hadi star tv wakafanya yale ,aneno ya Lema kama bango polosi na vyombo vya usalama wanajiandaa kuwapiga Chadema mabomu. Ndio intelijensia waliyo nayo siku hizi acha watu wanjinjane lakini sio Chadema wafanye mikutano. Ndugai kapiga kelele kuhusu Kiteto serikali kimya. Sasa Kilimanjaro serikali wanavuta shuka. Hii ni hatari sana kwa Taifa.
 
Serikali ya kudeal na matukio. Badala ya kuzuia kitu kabla hakija tokea, ona Kiteto leo viongozi wanakimbilia huko as if hiki kitu ni cha jana. Mh Lema alizungumza mapema sana hadi star tv wakafanya yale ,aneno ya Lema kama bango polosi na vyombo vya usalama wanajiandaa kuwapiga Chadema mabomu. Ndio intelijensia waliyo nayo siku hizi acha watu wanjinjane lakini sio Chadema wafanye mikutano. Ndugai kapiga kelele kuhusu Kiteto serikali kimya. Sasa Kilimanjaro serikali wanavuta shuka. Hii ni hatari sana kwa Taifa.

serikali na viongozi ni adui # 1 kwa wafugaji na wakulima.hawana msaada wowote, watu wanauwana damu isiyo na hatia inapotea tu.
hao viongozi wanaochaguliwa ni mzigo na chanzo
mbona sehemu zingine mikutano na mandamano polisi au jeshi linapelekwa...kwann wasipeleke huko
kiteto na siha...mpaka waziri akae kikao kipewe budgt
wapige hela....nchi hii ime feli kabisa
 
Nilisoma jana Michuzi Blog kuwa waziri mkuu amesema sasa mapigano ya wafugaji na wakulima basi. kauli hii aliitoa katika kikao cha kamati ya uongozi wa Bunge jana, kikao ambacho jasho la walipa kodi ambao ni wakulima na wafugaji wamelipa kwa ajili ya maendeleo ya nchi lakini wao wanajilipa posho kwa ajili ya kutoa majibu mlainisho kama hayo. simple like that bila kusema wamejipanga vipi kukabiliana na suala hilo au ni mbin zipi mbadala na zile za awali, kwa Kauli ya pinda nikilinganisha na yale mauaji ya walemavu wa ngozi napata jibu rahisi kuwa huyu bwana anatishia kumwaga chozi mwisho wa siku.
Ameeleza strategy zozote au atatumia ile style yake ya wapigwe tu...

Bila kupima ardhi na kuigawa kwa wananchi bila upendeleo mgogoro upo na utaendelea kuwepo. Mifugo inataka chakula na wakulima wanahitaji ardhi hiyohiyo kulima. The solution is very simple......
 
mbona Professor anajibu tu mesage za kumpa pole ina maana hizi hazioni?
 
serikali iko bize na chadema na na kuwasahau watu wake ccm kila kukicha inapoteza mtaji wa kura kutoka kwenye main capital yao wajinga wakulima na wafugaji jamani 2015 mtatafutana sana
 
mbona Professor anajibu tu mesage za kumpa pole ina maana hizi hazioni?


Tezi dume na pressure ya ESCROW vitamuweka pabaya.

wao husema anajishughusha na mambo mepesi joke, chart msgs, usingizi nakucheka zaidi, asifanye shughuli nzito na ngumu.
 
Serikali inashindwa hata na yule bwana mdogo wa Arumeru mh. Joshua Nasari ambaye ni mpambanaji migogoro kwenye jimbo lake iko ukingoni. Kisha unajisifu una mkuu wa wilaya, mwenyekiti wa halmashauri, madiwani achilia mbali mkurugenzi ambaye kazi ni kusafiri na kusign cheques na uhamisho. Ipo haja ya kubadili mifumo mibovu kuliko kuwa kama sasa.
Mpaka leo sijui hawa wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa ni vibaraka wa nani. Maana sioni wanachokifanya hata kufatilia miradi ya maendeleo.
 
Kwa ukubwa wa ardhi na eneo lilonalo Tanzania, mapigano yoyote ya kugombea ardhi ima kwa ajili ya ufugaji, kilimo au makazi ni matokeo ya Serikali mbovu isiyoweza kufikiria hata kwa kiwango cha ukubwa wa sisimizi. Ni mipangilio mibovu tu ya matumizi ya ardhi, na ulafi wa viongozi.
 
wakulima na wafugaji adui yenu ni serikali hiiiiiii
na viongozi wake.
 
Tezi dume na pressure ya ESCROW vitamuweka pabaya.

wao husema anajishughusha na mambo mepesi joke, chart msgs, usingizi nakucheka zaidi, asifanye shughuli nzito na ngumu.
ikulu kila siku wana toa update kuhusu tezi dume la rsis.....linavyoendelea ndyo kazi kubwa waliyonayo sahv....
 
Nataka nizungumzie ya uwekezaji siha na kwingineko nchini. Ya Kiteto
ni upuzi wa viongozi kupenda kuhubiri badala ya kutenda.Nilimwona mkuu wa mkoa wa manyara bw erasto
mbwilo akizungumza na wazee wapande zote mbili; wafugaji na wakulima. Anawaambia: "Ugomvi sasa basi!"
Hayo maneno yatasaidia nini kama si upuuzi tu?

Siha na uwekezaji.Uwekezaji katika nchi hii umeshabikiwa sana na ccm kwamba ni njia nzuri ya maendeleo na kwamba eti uwekezaji 'unatoa' ajira.Kwa hiyo wageni wengi wakapewa maeneo makubwa ya uwekezaji, siha mojawapo.Lakini ajabu ni kwamba serikali haikujua kwamba ardhi ni jambo la utamaduni mno.Huku kwetu tanzania mtu unatambua kabisa kwamba hili shamba (ardhi) ni ya mtu fulani na unakatiza njia kwenye shamba hilo kwenda kwenye shughuli zako.Hakuna anayekuuliza au kukushangaa kwa nini umekatisha njia shambani.Hili ni jambo watanzania tumelizoea sana.Wenzetu kwenye mambo ya shamba (ardhi) hawako hivyo.Shamba (ardhi) wanaita 'property' na ni kosa kubwa kukatiza njia kwenye shamba (property) yake. Hii kwenye sheria wanaita 'trespass' na mwenye shamba yuko huru kukufanya lolote alitakalo akikukuta kwenye property yake; kukupiga risasi ni jambo la kawaida.Waswahili wengi wamepata matatizo makubwa kuhusiana na mashamba ya wawekezaji.Waswahili hawa husema:Yaani hawa wawekezaji ni watu wa ajabu sana,kupita tu kwenye shamba lake ni ugomvi?Watu wabaya sana hawa, tuwaondoe!
Somo la property na trepass waswahili hawalijui na viongozi pia hawalijui.Kwa wawekezaji na waswahili chokochoko huanziaga hapa.

Kwa wamasai kwa mfano, ng'ombe mmoja mzururaji anatosha kuzua kasheshe kwa mwekezaji.Na mmasai lazima ahakikishe ng'ombe wake anakula na kushiba!

Kwa hiyo ya siha ni mgongano wa tamaduni na jambo hili wamasai (wenyeji) walitakiwa wasisitiziwe tangu mwanzo.
 
Wakulima na wafugaji waliitwa Dodoma kwenye BMK na masuala yao yamewekwa kwenye Katiba Inayopendekezwa! Sasa wanauwana, viongozi wa serikali wapo kimyaaaa!
 
Hii nchi iko kwenye auto pilot aliandika siku nyingi johnson mbwambo, there is nobody on the control panel
 
Back
Top Bottom