Ni swala la kutoa kipaumbele tu, wameshindwa kuajiri webmaster kwa ajiri ya ku-update website ya chama...ni kitu cha kushangaza sana kuona website ya chama iko doro wakati ile wabsite ni dynamic ni rahisi tu ku-update....Hivi mbona inaonekana ni tatizo sana hiki kitengo kusikia maoni ya watu na kuboresha huduma zake. Ukienda kwenye website yao imelala doro kabisa wakati matukio yanatokea kila siku. Au Chadema hawana kitengo kama hiki? Kama hawana basi waanzishe ASAP!
Ni wazo zuri lakini kwa vile SISIEMU na serikali yake bado ni 'wababe', kuwawekea kila kitu hadharani officially vitu vinaweza ku-'back-fire' maana CCM hawachelewi 'kuchakachua' wacha tuendelee 'kuwastukiza na nguvu ya umma' .
Hivyo 'nguvu ya umma' kupitia JF ndiyo mojawapo ya source ya mawasiliano kwa sasa, maana kwa njia hii ya 'ushirikishwaji wa nguvu za umma' katika kueneza sera na habari za CHADEMA, chama kina uhakika kuwa huu moyo wa kujitolea kutoa habari za matukio toka mashinani ni dalili tosha CHADEMA inakubalika na 'kikishaeleweka' baadaye ktk KATIBA MPYA YA TANZANIA basi mambo yatakuwa more official. kwa sasa acha nguvu ya umma iburuzane na SISIEMU iwe maandamano, forums n.k
Mtindo wa mpaka 'katibu mkuu ofisi ndogo ya CCM Lumumba' kuwa njia pekee ya kutoa habari ni sawa na kupora haki za 'nguvu ya umma' kuwasiliana wenyewe kwa wenyewe bila kutegemea mfumo rasmi.
ndugu yangu CHADEMA kinakuwa tu kwa nguvu za mungu..wala hakuna kitengo idara wala hata dawati la mawasiliano ya umma...kuna idara ya habari na uenezi ambayo wamemuweka jamaa mmoja aliyewahi kuwa mbunge wa kisesa miaka ya nyuma na akashindwa shindwa baadaye mtu ambaye hana uwezo hata kidogo..mawazo yake yeye ni NGONO masaa 24..
SIKU WATANZANIA WAKIIJUA CHADEMA HALISI NDIO MWISHO WA UPINZANI NCHINI
Tusiwalaumu CDM kwa hili kwani chama kimepanuka kwa haraka mno katika kipindi cha kuelekea na baada ya uchaguzi 2010. Hizi zinaitwa growing challenges na taasisi zote zinazokuwa huyapitia haya. Matarajio ya watu kwa Cdm ni makubwa na kuyatimiza ni changamoto kubwa. Naamini wahusika wameyaona maoni yenu na muda si mrefu tutaona mabadiliko.