Matatizo yaliyoko Arusha ni ya kwaida kama yaliyoko Dar, mwanza, tanga na kwingineko. bei za vitu vya madukani kama nguo na vifaa vya elekronics ndo bei iko juu lakini si sana. price margin kati ya vitu ya dar na arusha kwa vitu vingi haizidi 5000. Nyumba pia ni ghali lakini za kiwango cha kati ila nyumba ikishakuwa na rooms 3 na sebule na garage bei zake zinakuwa ndogo kuliko Dar kwani arusha haina wapangaji wengi wa kiwango hicho.
Sii kweli hata kidogo. Inaonekana aither umetokea Manispaa, Tanesco, au Maji.
Mimi nina makazi Arusha na Dar pia. Mji wa Arusha ni mdogo ukilinganisha na Kinondoni kwa mfano. Lakini ni mchafu kupindukia . Hebu anzia Shoprite kuelekea AIR port uone sehemu ya Ngarenanaro ambayo iko mjini kabisa ilivyokaa. Haifai hata kidogo ,then ndio njia wanapita wakuu wote na watalii pia. AIBU
Kuna hao AUWSA ambao hawafanyi lolote kuboresha huduma ya maji mjini. Huko milimani kuna vyanzo vingi sana vya maji ambapo Arusha ingekuwa mfano wa huduma bora ya maji kati ya mikoa yote nchini. Lakini wapi bwana. La ajabu zaidi ni pale wanapoingia garama ya kuweka bomba jipya kama walivyofanya eneo la Moshono -Suye halafu maji yote wanayadirect KARAMA Logde kiasi kwamba wananchi wanapata maji siku moja au mbili tu wiki.Utashangaa Wazungu wanavyowaifluence Wabongo wote waliopo kwenye hiyo Taasisi ikiongozwa na Munisi.
Hiyo Tanesco ndio usiseme. Toka mwezi wa 5 hadi sasa Arusha kuna mgao wa umeme. Mbaya zaidi wanapiga kimya kimya.
Hata baada ya kuingiza LUKU ambazo wananchi walizipenda badala ya zile walizokuwa wanabambikiza bili, inakuwa taabu kufungiwa .Ni hadi rushwa kupewa luku. Si aibu hii jamani?
Hiyo Manispaa haijawahi kuwa na uongozi thabiti wenye kuona mambo kwa mapana yake. Mara alikuja Job Laizer ambaye ni Mwarusha aliyewekwa na Lowasa akavurunda vurunda hapo weeee akaishia kustaafu. Aliyepo sasa naye hawezi kuwa na jipya maana alikuwa hapo hapo kama Afisa utawala. The same circle. Sasa usiombe uende huko Mipango Miji na Ardhi usikie akina mama wa mipango miji wanavyoargue . Huwezi kuamini waliwahi kufika hata darasa la tano. Aibu tupu.
Mimi nakubaliana na mleta hoja kwamba Ar . ni mji uliooza .Bora Tanga na Moshi. Uongozi ni wa kuunga unga tu kwa maslahi ya wakuu. Barabara ni mbovu na ni moja tu kuingia na kutoka hasa Njiro -Town. Beside inahost International Institutions nyingi tu ambao wakikaa wanasema kweli Watz hawana akili hata kidogo.
Habari ya viwanja Arusha ni muziki mzito. Kwanza hawapimi, na wakipima kupata ni mbinde. Watu hujinunulia viwanja toka kwa wenyeji na hujijengea bila utaratibu maalumu maaa kama nilivyosema hapo juu mipango miji Arusha literary hawapo.
Matokeo yake ni uharibifu wa maeneo na kuendea kuongeza squaters tu japo za nyumba nzuri. By the way kama hujui Arusha ndio mji unaoongoza kwa squater Tanzania Nzima. Unga LTD , Matejo, Kambi ya Fisi, Kijenge, sehemu za Mbauda to mention just a few.
Ukiacha tu hali ya hewa na kamzunguko ka hela Arusha is the worst town in in the real sense of towns per se.