Kitchen Party: Ushauri wa bure kwa makungwi

Kitchen Party: Ushauri wa bure kwa makungwi

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,678
Kitchen Party ni utaahira mwingine ambao sijui tumeupata wapi?
Eti kungwi hanijui mimi, hajui sipendi nini Na pia hajui napenda nini, yeye Na wanawake wengine ndugu wa mchumba wangu Sky Eclat wanamchukua mchumba wangu Na kumpeleka kwenye kitchen Party Na kuanza kumfundisha namna ya kuishi Na Mimi. Inanunua mimi nyie????

Kwanini msinialike Na Mimi niwepo kwenye masomo hayo? Au mnafundishana uchawi Na malimbwata?

Nawashauri Bwana harusi mtarajiwa awepo kwenye kitchen Party kama mnataka ndoa zenye mafanikio
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] imebidi nicheke

Lakini mbona wapo makungwi wa bwana harusi?? Sjui kwa mila na makabila mengine lakini najua bwana harusi naye anakua na kungwi wake pia
 
Unataka uwe unamkosoa mkeo asipofuata aliyofundwa? utavumilia kweli pale atakapoambiwa figa moja haliinjiki sufuria? Mafiga shurt yawe matatu mwaya..... naona unataka ufe kwa presha kabla ya harusi wewe!
 
Kama mafundisho ndio hayo hata akiwa Na dereva wa bodaboda, fundi majiko, Na mpemba muuza genge nitavumilia maana ndicho alichofundishwa akafanye kwenye ndoa yake
 
Sijawahi kuona +ve effects ya kitchen party.

Hao makungwi wengi wao hawapo katika ndoa

Wanaofanyiwa hivyo bado wana michepuko nje.

Wanaofundwa bado hawaridhiki na waume zao.

Ndoa za waliofundwa hazidumu na ni bora ya ambao hawajafundwa.

ndoa ni ya wawili, wanaoongezeka ni waharibifu muda wote
 
Shuleni siku zote lengo ni kufundisha mazuri. Kama kuna walimu watakuwa wanafundisha Utumbo basi ndiyo wenye makosa ila lengo la shule lipo palepale.
 
Nijuavyo ukweli makungwi wakike wanatakiwa kumfunda mwanaume

Makungwi Wa kiume wamfunde mwanamke
 
Harusi ni chain ya upigaji. Ni fursa kwa wajanja. Je mnataka makungwi wale wapi?
 
Njoo tanga bujibuju kuna makungwi wanawafunda wanaume, tena wanafundishwa kukata viuno kitandani na wanakua wazur SNA kitandani. Ndio maana wanaume wa kitanga wanahongwa SNA sababu wanajua mapz SNA
 
Back
Top Bottom