Kitchen Parties isiwe ya kina mama tu na kina baba pia wawepo

mlukosi

Member
Sep 10, 2013
53
18
Kuna mtu leo kanifanya niwaze upya huu utaratibu ni nani hasa anaepaswa kuwa mtoa mada, mama au baba? Imekuwa ni mazoea akina mama kuwa wahusika wakuu lakini kwa udadisi wangu wao hukazania maswala ya Chumbani yes binti anatoka kakolea kaiva kunako uwanja na mazingira yake, tena wengi wao hutumia uzoefu wao kufunza shida, vipi kuhusu mengine?

Kwanini isiwe baba mzazi ndio amfundishe bintiye jinsi ya kuishi na mumewe, hi ni kwa sababu tu tabia na mahitaji ya mume ayajua ayajua zaidi baba mwenyewe na si mke au mama. Wao wamekuwa chini ya mama wakati wote wa makuzi nafasi ya mwisho kwenda kumudu ndoa yafaa aifanye baba na si mama MH HII MNAIONAJE?
 
Kidume umejitutumua,
misuli umekutoka kwa surubu za kazi ngumu,
Umekaa mbele ya jopo la kina mama na vibinti,
huku mkononi umeshikilia Mic na kwa jisauti zito unaanza kumfunda binti yako huku wanawake wanapiga vigelegele...
Damn..!!
 
Hahahahahahah.... si kwa pozi hilo mkuu.... kwa mtazamo wangu Baba Mzazi yeye ndo anaepaswa kuhakikisha bintiye anakuwa na uelewa mpana tena wenye ualisia juu ya changamoto ze mme.... sisi tunajijua wenyewe!!!! hahaha dah si kwenye kitchen party lakini
 
Siku hizi kitchen party ni kwa ajili ya kujijazia zawadi na vyombo hamna mafunzo wala ujuzi au utaalamu. Kungekuwa na mambo ya maana kwenye kichen party ndoa nyingi zingetulia.
 
hamna mafunzo yoyote yanayofanyika kwenye kitchen party, zile ni mbwembwe tu, kama binti hajafunzwa alipokuwa kwao hamna muujiza unaoweza kutokea siku ya kitchen party ( it is a process, sio kitu cha siku moja)
 
Hahahahahahah.... si kwa pozi hilo mkuu.... kwa mtazamo wangu Baba Mzazi yeye ndo anaepaswa kuhakikisha bintiye anakuwa na uelewa mpana tena wenye ualisia juu ya changamoto ze mme.... sisi tunajijua wenyewe!!!! hahaha dah si kwenye kitchen party lakini
Anhaa, nishakusoma
 
Siku hizi kitchen party ni kwa ajili ya kujijazia zawadi na vyombo hamna mafunzo wala ujuzi au utaalamu. Kungekuwa na mambo ya maana kwenye kichen party ndoa nyingi zingetulia.
Tena kadi ya mwaliko inawekewa msisitizo : HATURUHUSU ZAWADI YA VYOMBO VYA PLASTIC hahahahaha
 
Yaani ndo mana napenda sana makabila yenye jando na unyago. Haya mafunzo yanapaswa kua ya jinsia mbili zote
 
Back
Top Bottom