Madoa Matatu Yanayochafua Mioyo Ya Mama Zetu na Kuwaacha Wakiwa Watu Wapweke Zaidi na Kwa Kipindi Kirefu Zaidi ya Baba Zetu.

janfirst

Member
Nov 29, 2019
14
58
MAMA.jpg


Je, umewahi kufikiria kuwa Mama ndie kiumbe anaepitia upweke kwa kiasi kikubwa zaidi katika maisha zaidi ya Baba?

Ni ukweli usiopingika kuwa mama ndie namba mbili baada ya Mungu muumba wetu alieumba ulimwengu, kwani mama ndie binaadamu anaechukua nafasi kubwa zaidi katika kuja kwetu duniani hadi kukukua kwetu licha ya lawama nyingi anazotupiwa juu ya malezi ya watoto zake.

Licha ya nguvu alizonazo juu ya umiliki na ushawishi alionao katika malezi na utunzaji pamoja na ukuaji wa familia sikutegemea kuja kuona kuwa bado ni mtu mpweke zaidi na mwenye majaka ya moyo, kwani tunategemea kuwa ndie mtu namba moja wa kula matunda ya watoto pamoja na familia lakini uhalisia ni wachache wanaopata matunda hayo na kubaki kutumainia kuwa nitapata kesho.

Ni yapi hayo madoa matatu yanayochafua mioyo ya mama zetu na kuwafanya kuwa wapweke zaidi ya baba zetu?

Mama anapoingia katika mahusiano ya kimapenzi ama ndoa kwa mara nyingi na kwa mama waliowengi hutegemea kuwa mahusiano hayo ndio furaha ya maishani mwake kwani ataishi kwa raha na mwanaume aliempata pamoja na kujenga familia yao na watoto wao lakini kwa mara nyingi sana Mambo huwa tofauti kutokana na mambo yafuatayo:

DOA NAMBA MOJA
Maisha kati ya Mama, Mumewe pamoja na familia ya ndugu wa mume
Baada ya kuanza maisha haya ya pamoja kwa asilimia kubwa kina mama hukutana namaneno, manyanyaso na kero kutoka kwa ndugu wa mume aliemuoa na manyanyaso hayo huyapitia katika mambo mbali mbali na cha kuzidisha huzuni ni pale baba mda mwingi huwa katika mihangaiko ya kimaisha tofauti na mama. Na kwa kuwa ni kawaida mwanaume ameumbwa na kutojali sana na kuchukulia mambo kawaida kawaida au kuegemea zaidi kwa familia yake, basi huhisi mwanamke kawaida ni mlalamikaji sana juu ya vitu vidogo vidogo na mwisho wa siku kupuuzia kubeba changamoto za mama juu ya ndugu wa familia yake na ubaya zaidi mda mwengine mama huwa hafunguki kila kitu anachopitia kwa mumewe juu ya familia yake kwa kuhofia kuvuruga mahusiano ya mumewe na familia yake. Hivyo kupelekea mama tayari huingia doa la kwanza katika moyo wake na kumuacha na upweke wa kwanza licha ya bado kuendelea kuwa na maisha na mumewe.

DOA NAMBA MBILI
Hili hupatikana Pale baba na mama wanapoishi kwa pamoja kwa kipindi Fulani hivi kuna mambo kwa familia zilizonyingi hutokea na ni pale Baba anapoanza mahusiano na mwanamke mwengine nje ya ndoa yake, aidha kwa kuchoshwa na tabia za mama zetu (mapungufu) ama baba alioa mke ambae kumbe halikua chaguo lake,ama tu dharau za baba kwa mkewe,au pengine baada ya baba kuongezeka kipato, pamoja na sababu nyenginezo.

Kwa kawaida baba akisha anza kutupa macho yake kwa mwanamke mwengine, kwa namna moja ama nyengine nyumbani mapenzi hupungua na mda mwengine yaweza kuwa siri na hata ikawa dhahiri, wapo kina mama wanaoshindwa na kuamua kuondoka kumuacha baba, wapo wanaoachwa na waume zao lakini pia wapo kina mama wanaovumilia na ndio hawa huumia zaidi na kuongeza majeraha kwani hutaka kuendelea kutunza ndoa yake ilhali pia akiendelea na maumivu na mda mwengine bila hata ya kusema kwa familia yake akiamini anatunza ndoa na familia isivurugike watoto wakateseka. Hili nalo sasa huwa ni doa la pili wanalokumbana nalo mama zetu waliowengi zaidi na huwaacha mama zetu wakijawa na upweke lakini bado wakiwa na matumaini na kuamini nitapata mapenzi kwa watoto zangu.

DOA NAMBA TATU
Maisha ya Mama na watoto zake
Baada ya mama kuona amekosa mapenzi kwa familia ya mume wake na hata kwa mwanaume aliemtegemea kupata mapenzi na kudekezwa,kujaliwa na kuskizwa basi sasa matumaini huyaelekeza kwa watoto zake na huamini pamoja na kutumaini kupata mapenzi kutoka kwa watoto zake kwamba watamfariji, lakini pia kwa asilimia kubwa napo mambo huwa tofauti.

Baada ya watoto kukuwa sasa inabidi waingie katika masomo ama shuguli nyengine zinazowaweka katika pirika mda mwingi na mama kukosa kuwa karibu na watoto zake kwa mda mwingi na hasa ukizingatia zaidi kwa sasa pirika za kutafuta maisha zimekua mchaka mchaka kupindukia.
Lakini cha zaidi ni pale watoto wanapoanzisha familia zao sasa na kujikuta mda mwingi anashulika na familia yake zaidi ya mama yake na hata mda mwengine kupita wiki au hata mwezi mama hajapokea simu ya mwanae.

Mama waliowengi sio wenye tama kwa watoto zao ya kuwa lazima mtoto alete mali kwa mama au maisha mazuri lakini mama pia huwa kama mtoto sasa na yeye anahitaji mapenzi ya kuwa karibu na watoto zake na kujaliwa lakini anajikuta anakosa. Hapa sina maana kuwa watoto wote ndio huishi hivi ila kwa asilimia kubwa haya ndio maisha yalivyo.

Mama anakosa mtu wa kujua wala kujali hisia zake, mama anakosa mtu wa kumchekesha, mama anakosa mtu wa kupiga nae stori na kumkumbusha furaha za zamani angalau basi nae ajihisi bado anaishi na ana hadhi na thamani katika watu.Na hata wengine sasa kuwaona mama zetu washamba au wamepitwa na mda hawana hadhi ata ya kutumia smart phone. Mama anahitaji zaidi uwepo wa mtu zaidi ya kitu ila ukiwa nacho basi ni vyema ukala nae tena ikiwezekana zaidi ya unavyokula wewe.

Maajabu ya Mama

Licha ya yote hayo bado mama siku zote ndani ya nafsi yake hujihisi yeye ndio mwenye jukumu zaidi la kujali familia yake,kuisimamia na kuilinda. Hii ndio mana mama haachi kuiombea familia yake na mda mwengine baba anaweza asikatae kupokea kidogo alichonacho mtoto wake lakini mama akakataa na kusema hapana mwanangu hicho acha kikusaidie wewe mwanangu.

NI JUKUMU LETU WATOTO KURUDISHA FURAHA KWA MAMA ZETU KWANI TUTAMBUA KUWA MAMA ZET WANA MENGI YA KUHUZUNISHA KATIKA MIOYO YAO TUSIYOYAJUA BASI TUSIWAACHE PEKE YAO KWA MUDA MREFU KWANI KUFANYA HIVYO TUNAWAPA NAFASI YA KUWAZA YALIYOWAUMIZA, KITU AMBACHO HUWASABABISHIA MARADHI TOFAUTI TOFAUTI WAKATI DAWA TUNAZO WATOTO.- Janfirst.ksa
 
Kweli kabisa me nasoma kwa juhudi za Mama tena nimerudia shule bado ananisisitiza soma hadi ww uchoke nitakupa chochote kikubwa usome mwanangu, Baba alifariki miaka kumi iliyopita, yan Mama yangu ni nguzo yangu. Saizi nasoma chuo mambo mwemwele mwemwele, My Mama always is my no one.
 
Weee vipi? Unaonge kuwafurahisha akina mama au unaongea uhalisia? Kuzaa na kulea kiumbe mpaka kijitambue kunahitaji kipawa/kipaji ambacho kapewa mwanamke zaidi kupita Mme. Hata hivyo changamoto za maisha ya dunia hii ni nzito na zinatisha! Ni mwanamme pekee anayeweza kukabiliana na changamoto nzito zinazotisha hata kufisha! Mwanamke hawezi kabiliana na changamoto za dunia hii ambazo mwisho wa siku ndo zinaleta maendeleo na kusogeza huduma za jamii karibu na na jamii.
MLETA MADA UNAKOSEA SANA KUMLINGANISHA MWANAUME NA MWANAMKE! Kila mtu ana nafasi yake sanasana mwanamke ni mvumilivu na ana huruma wakati ambapo dunia haina huruma! Ni jasiri tu ndo anaweza Ku_conquer nii dunia mwanamke hawezi! Eti "Ni ukweli usiopingika kuwa mama ndie namba mbili baada ya Mungu muumba wetu alieumba ulimwengu ". Weeeese utakuwa bado kijana!
 
Sijui kwanini wanawake wanachukiwa na familia ya mme na kuchuliwa kama sio wanadamu.
Wakati huo huo wana watoto wa kike
 
Back
Top Bottom