Kitanzi kwa wafanyakazi nchini: Pensheni sasa mpaka ufikie miaka 55


Inapaswa kamati ya bunge waufuatilie na hii mifuko ya jamii.

NSSF imejiwekeza sana kama ulivyosema pasipo kushirikisha wanachama. Na hata faida ya uwekezaji huu hatujui, imejenga majengo mengi na kukodisha, kuingia mikataba mingi na Serikali lakini hakuna taarifa aua ruhusa ya wanachama kuhusu faida ya uwekezaji huu.

Wajanja wanakula tu. Endapo mwanachama akiacha kazi anapewa pesa zake alizochangia na kafaida kadogo sana kanakoongezeka pale.

Sasa pesa imekaa muda mrefu, na wanaifanyia biashara; bado tuna miradi ya NSSF inayomiliki. Kwa nini faida isiongezeke?? au kuwe na mgao kila mwaka kwa wanachama.

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
Mifuko hii ni genge la mafia.

Kwa ujumla uwekezaji wa real estates ni gharama kubwa sana na kwenye nchi hii ambayo ufisadi umekuwa ni mtaji usitegemee kuona kuna faida yoyote kwa shirika na wanachama.

Menejiment zimejikita kwenye miradi hii kwa sababu ndio rahisi kuiba kwa 10% na price exaggerations na variation of design and other terms of the contracts justify wizi badala ya mradi kukamilika kwa bei ya bilion 10 unafikia zaidi ya 15 kama ambavyo miradi mingi ya ujenzi wa mashirika ya umma umefanyika kama tower twins-BOT,TCRA pale samu Nujoma na mengine mingi.

Tathimini ya thamani ya NSSF inaweza kuwa kwenye long term assets kama majengo ambayo thamani yake ni kubwa lakini kufilisika kwa shirika ni kushindwa kukidhi mahitaji ya kila siku kama kulipa madai ya kawaida kama hao pensioners.

Bado kuna safari ndefu katika kusimamia raslimali na kudhibit ufisadi huu.
 

Watunge tu hiyo sheria, ila tu watulipe stahili zetu zote kisha tuingie mkataba nao upya unaotumia hiyo sheria.
 
Naona wanataka kutufanya kama wazee wa EAC
Yelewiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Niligundua hii ishu ya mashirika ya umma kuishiwa/kupungukiwa uwezo wa kifedha, pale serikali ya JK ilipoanza kutapata kwenda kukopa ela kwenye commercial banks.
hooo tuchague viongozi kutoka mabila madogo. sifa hii ni mbaya maana tunapata viongozi dhaifu wasio na uwezo. tuache kubagua makabila makubwa tuangalie uwezo wa kusukuma mbele maendeleo. taswira hii mbovu ya uongozi ndio inayotufanya tushindwe kupata angalau watru 11 kutetea taifa letu ktk nyanja ya soka.
 

Mkuu mbona hii kitu imeshakua overtaken na events on the ground.

Bunge la Aprili 2012, kabla ya hoja nzito iliyotikisa bunge ya kutokua na imani na WM, wabunge walipitisha mabadiliko ya sheria ya usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii( na hapa inamaanisha mifuko yote sita) NSSF, PPF, PSPF, LAPF, GEPF,NHIF.

Moja ya vipengele vya hayo marekebisho, ni kuzuia mwanachama kuchukua pesa zake au kuwithdraw membership kabla ya kufikisha umri wa miaka 55.

Ingawa kuna uwezekano wa sehemu ya michango yake (50%) ikatumika kama dhamana pale anapotaka kukopa kwa shughuli za ujenzi tu.

Kwa hiyo mabadiliko haya yatacut across the whole sector ya hifadhi ya jamii(yaani mifuko yote) sio confined kwa NSSF peke yake.

Hivyo basi mkuu wa kaya akishatia sign yake kwenye muswada na kuwa sheria. Mambo ya kuvuta kilicho chako ndo itakua hadithi, may be uwe tayari na 55yrs.
 

What if kama nikiacha au kufukuzwa kazi mkuu? Ctaweza kuchukua my cash?
 
tatizo siyo kabila ila ni udhaifu wa mtu binafsi, mbona Mkapa ni kutoka kabila dogo na aliweza kujenga uchumi na kaondoka kaacha hadhina ikiwa na pesa za kutosha tu.
 
mbona inatisha sasa tanzania kila sehemu ni matundu matundu tu.jamani wanasiasa mnaifilisi nchi yetu.natamani 2015 ingekuja leo tumalize kazi
 

hooo tuchague viongozi kutoka mabila madogo. sifa hii ni mbaya maana tunapata viongozi dhaifu wasio na uwezo. tuache kubagua makabila makubwa tuangalie uwezo wa kusukuma mbele maendeleo. taswira hii mbovu ya uongozi ndio inayotufanya tushindwe kupata angalau watru 11 kutetea taifa letu ktk nyanja ya soka. safari hii ni lazima atoke kabila kubwa au maarufu
 
Wanaoifilisi NSSF ni
1. Serikali - imekopa hailipi.
2. Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe. Amekopa pesa hataki kulipa.
3. Wengine waliokopa bila kulipa.
 
MHH Kama nikweli ni hatari sana ni wizi niliwahi kuandika humu kwamba mfuko huu unaendeshwa kisiasa..lakini jee katiba ya sasa na sheria za mswaada haziruhusu kuzuia mswada kupelekwa bungeni..labda kuweka pingamizi mahakamani ..wenye uelewa watujulishe tuzuie hili ili tukatowe pesa zetu kabla maMBO HAYAJAHARIBIKA...

NA KWA HILI NAWASHAURI WABUNGE MAKINI WALIZUIE KWA NGUVU ZOTE...KWANI NI WIZI....
NSSF wanatumia vibaya pesa zetu ni moja katika shirika bovu kabisa..lakini watu huwa wanalewa wakisikia NSSF inajenga sijui nyumba za polisi,sijui daraja la kigamboni, sijui wamejenga UDOM..NK NK ..JII SIO KAZI YAO..
KAZI YAO NI KUWEKEZA FEDHA ZETU KATIKA MIRADI AMBAYO INA FAIDA KUBWA ILI WANACHAMA WAPATE MAFAO NA FAIDA NYENGINE ZITOKANAZO NA MICHANGO YAO

NAOMBA TUWEKE PINGAMIZI KWA HILI
 

Umenena mkuu.no coment.
 

Jaman tunaomba mtusaidie mnaofahamu kuhusu hii mifuko...wengine hatuna elimu ya kotosha kuhusu hizi social funds...ivi ukitaka kupata fedha zako unazokatwa kila mwezi hadi ustaafu au kuna sababu nyingine....engine wanasema hadi ueache kazi....plz i need help here
 
Hakika tunaweza kusema ni kitanzi kwa wafanyakazi masikini wa Tanzania.Habari za kuaminika kutoka wizara ya fedha na mifuko mbalimbali ya kijamii zinasema serikali inajiandaa kupeleka mswada bungeni katika bunge lijalo kwamba ni sharti ufikishe miaka 55 ndipo uweze kupata mafao yako.
Kwa hivi sasa kama mfanyakazi ataacha kazi katika makampuni mbalimbali binafsi anaweza kupata pensheni yake ndani ya miezi sita.Hali ni hiyohiyo kama mfanyakazi ni mgonjwa anahitaji matibabu basi aweza kupata mafao yake.
Lakini kwa mswada huu mpya unaotarajiwa ukipitishwa mfanyakazi yeyote katika makampuni na mashirika mbalimbali hataweza tena kupata mafao yake hata kama ameacha kazi mpaka atakapofikisha miaka hiyo 55.
Habari zaidi zinasema mifuko hii ya kijamii hasa NSSF yamewekeza katika miradi mikubwa isiyo na faida na pia yamekuwa yakikopwa na serikali lakini inashindwa kulipa kwa wakati.Hali hii imesababisha fedha za wanachama kupukutika na njia pekee ya kuepuka aibu hii ni kuandaa mswada kama huu utakaoacha kilio kikuu kwa wafanyakazi nchini.
 

Lo tumekwisha.Inatakiwa wabunge wote waungane bila kujali itikadi zao kupinga mpango huu haramu.Hiki ni kilio na hakika ni kilio kikuu kama cha mama mjane aliyefiwa na mwanaye pekee.
 
Japokuwa hujaweka source lakini tetesi hizi zimezagaa sana. Ni mpango kamambe wa serikali kuwakomoa wanachi wake, tena walipa kodi wakubwa nchi hii. Hii ni sheria mbaya na ikipitishwa nitaamini nia thabiti ya serikali ya JK kuwaua wananchi wake. So pathetic!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…