Kitanzi kwa wafanyakazi nchini: Pensheni sasa mpaka ufikie miaka 55 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitanzi kwa wafanyakazi nchini: Pensheni sasa mpaka ufikie miaka 55

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Molemo, May 3, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  kuna habari nimezipata kutoka mtu wa ndani NSSF kuwa pesa zetu zimeliwa zote na serikali sasa wanakuja kutunga sheria mpya mwezi wa saba bungeni kuwa mwanacha hutapewa pesa zake mpaka utakapostaafu.mimi nadhani kwa wale wanachama wa NSSF na mifuko mingine ya jamii tutakuja kulia kama wazee wa africa mashariki tusipokuwa makini na hii serekali,
  naomba kuwasilisha
  source ---nssf

  Hakika tunaweza kusema ni kitanzi kwa wafanyakazi masikini wa Tanzania.Habari za kuaminika kutoka wizara ya fedha na mifuko mbalimbali ya kijamii zinasema serikali inajiandaa kupeleka mswada bungeni katika bunge lijalo kwamba ni sharti ufikishe miaka 55 ndipo uweze kupata mafao yako.
  Kwa hivi sasa kama mfanyakazi ataacha kazi katika makampuni mbalimbali binafsi anaweza kupata pensheni yake ndani ya miezi sita.Hali ni hiyohiyo kama mfanyakazi ni mgonjwa anahitaji matibabu basi aweza kupata mafao yake.
  Lakini kwa mswada huu mpya unaotarajiwa ukipitishwa mfanyakazi yeyote katika makampuni na mashirika mbalimbali hataweza tena kupata mafao yake hata kama ameacha kazi mpaka atakapofikisha miaka hiyo 55.
  Habari zaidi zinasema mifuko hii ya kijamii hasa NSSF yamewekeza katika miradi mikubwa isiyo na faida na pia yamekuwa yakikopwa na serikali lakini inashindwa kulipa kwa wakati.Hali hii imesababisha fedha za wanachama kupukutika na njia pekee ya kuepuka aibu hii ni kuandaa mswada kama huu utakaoacha kilio kikuu kwa wafanyakazi nchini.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  It was only a matter of time NSSF wangekumbana na ukuta wa ukweli. Uwekezaji wa NSSF ni mbovu sana na umeegemea siasa. Lakini tatizo kubwa ambalo wamekuwa wanafumbia macho ni ukweli kuwa sasa NSSF ni fully fledged Pension na sio Provident Fund.

  Zamani NSSF ilikuwa Provident Fund (NPF) na taratibu za kuendesha NPF ni tofauti, mtu akistaafu unampa hela zake hapo hapo. Lakini kama ni Pension maana yake utamlipa kiasi hapo hapo na bado utalazimika kumlipa kiasi fulani kila mwezi mpaka afe. Sasa tangu NSSF itoke kwenye NPF si muda mrefu na hawakuwa na mzigo mkubwa wa kulipa wastaafu mpaka wafe, but with time ile idadi inaongezeka wakati huo huo hela ndio kama hivyo wamekewekeza kwenye miradi tata na mingine ni ya kisiasa hivyo kulipwa ni tabu (ref report ya CAG).

  Ninavyofahamu mimi kwa sasa kuna mfuko mmoja tu ambao uko 'solvent' - ni PPF. Pamoja na mapungufu yao lakini hawa wana uwezo wa kubeba mzigo wao wa 'pension' na hata uwekezaji wao sio wa kasi kama NSSF. Mifuko mingine kama LAPF, PSPF nao wana matatizo makubwa maana wamekopesha/wekeza na muda wa waastafu unanyemelea! Siasa nyingi.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  May 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tumewaambia haya mambo miaka mitano mkasema tuna 'chuki binafsi ' . Mnashtuka ghala tupu?
   
 4. markach

  markach Senior Member

  #4
  May 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Habari hii kama ni ya kweli mi imenistua sana, kuna hatari ya pesa zetu kuliwa nasi tukabaki tunalia tu. Hakika ni kwamba itafika kipindi ambapo hii mifuko haswa nssf itashindwa kulipa mafao ya wastaafu kwani inakisiwi kuwa kuanzia mwaka 2020 idadi ya wastahafu itakuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa, na hapo ndipo tatizo litakapoanzia. Tuwe macho watanzania
   
 5. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #5
  May 3, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Huu mfuko ni genge la wahuni wanautumia kwa manufaa yao bila watanzania/wanachama kujua.Malengo ya mfuko ni mazuri ila unaendeshwa kiutapeli zaidi.
  MMM alishawahi kutoa thread za kutosha kuhusu huu mfuko unakoelekea .Wasiwasi wangu mimi;Ni kwa nini mfuko huu unafanya kazi kama Investment Bank bila ridhaa ya wanachama?.
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  NSSF wamefilisika kwa sababu ya kuwekeza miradi ya kisiasa ambayo hailipi na sasa kwavile wanakalibia kuwa insolvent wanajaribu kuwashawishi hao wanaowaita DIASPORA walete vijidola vyao ili viwasaidie kuziba mapemgo!!
   
 7. y

  yolo Member

  #7
  May 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani nssf wapo poa.according to the research by audit firm,inasema nssf wanaweza kujiendesha miaka 15 bila kupokea michango kwa wanachama na kuwalipa bila kufilisika.halafu leo hii unasema wamefilisika.nssf cyo serikali ya bongo na uwekezaji wao una manufaa kwa watz cyo ccm.
   
 8. T

  Thepremier New Member

  #8
  May 3, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nssf ipo juu jamani siyo kama masharika haya mapya yaliyokuja sasa hvi. Nssf ina huduma nyingi zaidi ya hyo ya kulipa wastaafu.
  Msiandike vi2 msivyönauhakika navyo. Nyambafu.
   
 9. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #9
  May 3, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza nikupongeze kwa kuliona hili sio siri huu mfuko mbovu utatumaliza hata utendaji wake ni wa mashaka kweli we twende tu
   
 10. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Niligundua hii ishu ya mashirika ya umma kuishiwa/kupungukiwa uwezo wa kifedha, pale serikali ya JK ilipoanza kutapata kwenda kukopa ela kwenye commercial banks.
   
 11. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  don't miss the point. Hatutaki mabadiliko ya sheria yakayoahirisha kupata mafao YETU hadi wakati hatuwezi kuyatumia, only because of 'mchwa'
   
 12. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2012
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Not true.
   
 13. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Nimeamini Tanzania ni zaidi ya uijuavyo.
  Hapa kuna ishu mbili. Tuingine mtaani tu-strike, kwa ajili ya kuwatoa hawa majambazi ccm, au tushike jembe tukalime kilimo kwanza, lakini kulalamika iwe NO...
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Nyie ni watu wa NSSF au? Wakati kama nyie unakuta hata hamjasoma ripoti za CAG halafu mnakuja kuitetea NSSF kisiasa hapa. Uzuri kila kitu kimeanikswa wazi kwenye ripoti za CAG. Eti kuna audit firm imefanya utafiti na kukuta NSSF uko fit. Huo utafiti kweli unaweza ku-overrule utafiti wa CAG? Kasome ripoti ya CAG kabla ya kupayuka ovyo.

  CAG: NSSF hatarini kufilisika

  MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) uko hatarini kufilisika na kupoteza fedha za wanachama wake. Hii inatokana na serikali kushindwa kurejesha katika mfuko huu, mabilioni ya shilingi iliyokopa au kudhamini katika miradi mbalimbali. Kwa mujibu wa Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya 2010/2011, fedha za wanachama, hata katika mifuko mingine ya jamii, ziko hatarini kupotea.

  Mbali na NSSF, mifuko mingine inayotajwa kuwa katika hatari hiyo ni Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF); Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali Kuu (PSPF), Mfuko wa Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF).

  Kulingana na taarifa ya CAG, sehemu kubwa ya fedha za wanachama ambazo hazijarejeshwa, zilikopeshwa kwa serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Katika chuo hiki, NSSF peke yake iliingiza Sh. 234.1 bilioni. Mifuko iliyosalia ilitoa jumla ya Sh. 181.3 bilioni.

  Katika ujenzi wa UDOM, PPF ilitoa Sh. 39.99 bilioni, PSPF (Sh. 105.9 bilioni), LAPF (Sh. 22 bilioni) na NHIF (Sh. 13.4 bilioni). Fedha hizo na riba yake hazijarejeshwa. Ripoti ya CAG, Ludovick Utouh, inasema kutorejeshwa kwa mikopo hiyo, iliyochukuliwa au kudhaminiwa na serikali, ni kinyume cha sheria ya udhamini ya mwaka 1974.

  “Kutolipika kwa mikopo hii iliyodhaminiwa na serikali kunaiweka mifuko hii ya hifadhi katika hatari ya kupoteza fedha za wanachama na kuhatarisha uwezo wa mifuko kufanya uwekezaji zaidi,” anasema na kuongeza: “Kushindwa kulipa madeni taasisi hizi ambazo baadhi yake zilipata udhamini wa serikali, kunatia shaka iwapo upembuzi wa kina wa wakopaji ulifanywa na mifuko ya kijamii kabla ya kutoa mikopo hiyo.”

  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau hakupatikana kwa maelezo kuwa alikuwa kwenye mkutano mkoani Mbeya. Lakini Meneja Kiongozi Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume amesema mikopo kwa serikali imetolewa kwa uangalifu na inalipwa bila matatizo na kwa misingi ya kibiashara. “Mikataba ya kisheria imesainiwa kukidhi mazingira mbalimbali ikiwa ni pamoja na iwapo itacheleweshwa…. Hakuna hatari yoyote ya fedha kutolipwa wala kupoteza fedha za wateja,” amesema Chiume.

  Lakini CAG katika taarifa yake ya kurasa 183, anasema, “Ukubwa wa kibiashara kati ya serikali na mifuko unatia shaka kutokana na kusuasua kwa serikali katika ulipaji madeni yake. Hii inahatarisha uendelevu wa mifuko hii.” Katika ukaguzi wake, CAG amebaini kuwa NSSF ilitoa Sh. 234.1 bilioni kwa mradi wa UDOM, lakini mkataba uliosainiwa ni wa Sh. 35.2 bilioni tu. Hii ni hatari kwa fedha za wafanyakazi na wastaafu.

  Akifafanua suala la fedha kwenye mkataba kutofautiana na fedha zilizotolewa, Chiume alisema mkataba ulitakiwa kuwa mmoja ambao ulisainiwa wakati wa awamu ya kwanza. Chiume alisema kwa awamu ya pili, kilichotakiwa ni kusaini addendum (makubaliano ya nyongeza), ambayo “yako mbioni kukamilika.”

  Utouh anaripoti, “Majengo kwa ajili ya awamu ya kwanza yalikamilika na kuwekwa katika matumizi mwezi Septemba 2008. Mpaka wakati wa ukaguzi 2010/2011, mfuko ulikuwa haujafanikiwa kukusanya malipo ya pango kutoka serikalini. Kwa msingi huo, hadi sasa limbikizo la riba limefika thamani ya Sh. 14 bilioni,” anasema Utouh.

  Mkopo huo ulitolewa kwa utaratibu wa kubuni, kujenga, kumiliki na kuhamisha ambapo mfuko ungepokea kodi iliyokokotolewa kwa riba ya asilimia 15 kwa kipindi cha miaka kumi. Vilevile CAG amebaini kuwa majengo yaliyojengwa kwa mkopo huo, hayako kwenye vitabu vya UDOM wala katika vitabu vya NSSF, kutokana na uelewa tofauti uliopo kati ya pande mbili zinazohusika.

  Kuna mikanganyiko katika uelewa kwa serikali na mifuko ya hifadhi, ameeleza CAG. Wakati mifuko inasema fedha zilizotumika kujenga majengo hayo zilikuwa mikopo kwa serikali, yenyewe serikali inadai fedha hizo ni uwekezaji wa kawaida wa mifuko hiyo.

  Mbali na UDOM, serikali pia haijalipa jumla ya Sh. 19.77 bilioni zilizotumika katika ujenzi wa ukumbi wa bunge, ambazo hazilipwi kulingana na makubaliano. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa inadai Sh. 8.96 bilioni, PPF (Sh. 7.9 na LAPF Sh. 2.91. Pia upo mkopo mwingine wa NSSF wa Sh. 5.33 bilioni na riba ya asilimia 15 kwa miaka kumi, uliotolewa kwa ajili ya ujenzi wa “taasisi ya serikali ya kiusalama” mwaka 2007.

  Mfuko mwingine uliowekeza katika mradi huo ni PSPF uliotoa Sh. 6.4 bilioni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, NSSF kwa udhamini wa serikali ilikopesha taasisi kwa shughuli mbalimbali. Kwa mfano, ujenzi wa nyumba za polisi kwa Sh. 20 bilioni na Sh. 12. 9 bilioni kwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam mwaka 2007 kwa ajili ya ujenzi wa Machinga Complex, Ilala. “Hadi sasa hakuna malipo ya riba wala sehemu ya mkopo hiyo yaliyofanywa. Hii ni kinyume cha mkataba,” inasema sehemu ya ripoti ya CAG.

  Kwa upande wa Machinga Complex, hadi tarehe 30 Juni 2011, mkopo na riba yake ulikuwa umefikia Sh. 15.3 bilioni. Ripoti ya CAG imeainisha pia mikopo mingine ambayo hailipwi kulingana na mikataba ya mifuko hiyo, bila ya kutaja viwango vyake.

  Mikopo hiyo ni iliyotolewa kwa Continental Venture (T) Limited, Meditech Industrial Co. Ltd, General Tyre (GT), Kiwanda cha Sukari Kagera, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na mgodi wa mkaa wa mawe wa Kiwira, mkoani Mbeya. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio amesema hajaona ripoti ya CAG na yuko safarini Tanga.

  Hata hivyo amedokeza kuwa hivi karibuni walikaa na CAG kujadili suala hilo na kubaini makosa ya kifundi katika uhasibu baina ya mifuko na serikali katika ujenzi wa UDOM; hivyo CAG kuahidi kuyashughulikia kwa upande wa serikali. Alipoulizwa ni makosa yapi hayo, Erio alimtaka mwandishi awasiliane na kaimu wake, Stephen Alfred ambaye ilielezwa kuwa yuko kwenye mkutano. Hadi tunakwenda mitamboni, Alfred hakupatikana.

  CAG: NSSF hatarini kufilisika | Gazeti la MwanaHalisi
   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  sawa mkuu, na yale ya PPF ikawaje?
   
 16. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Tutauza majengo yote tuchukue hela zetu.
   
 17. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Tafuta ripoti ya CAG ujionee senema za bure ndugu, usimalize povu bure manake utalihitaji siku ya kutendwa kweupee!
   
 18. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mtamuuzia nani? Kama machinga complex ukimuomba Manji anunue atasema anatoa sh milioni 100, hayo mabilioni mtalala nayo doro. Ref maghala yaliyonunuliwa nae hapo kitambo.
   
 19. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wana JF mshaanza kuamini TETESI..?!~
   
 20. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  vipi mkuu, kwani wewe unaamini tetesi kwamba JK ameita waandishi ili atangaze mabadiliko kwenye baraza la mawaziri?
   
Loading...