Kitanzi kwa wafanyakazi nchini: Pensheni sasa mpaka ufikie miaka 55

tatizo ni teuzi zitokazo kwa urais wa kifalme. Wakurugenzi waajiriwe kama wafanyakazi wengine but kwa mkataba. Kwa kuwa ndani ya nnsf hakuna mwakilishi wa wanachama basi bunge lilidhie uajiri wa hao wakurugenzi. basi
 
Si kweli. PPF ndani ya mwezi unachukua. Pia PPF ukitaka kuona michango yako si lazima uende kwenye ofisi zao. Unaingia tu online unapata information zako. Sema kingine!
Majungu fitna na wivu wa mifuko mingine baada ya NSSF kuonekana ni tishio katika uwekezaji.

Kuna jamaa yangu aliupopata nafasi ya kusoma akapewa chake full, niambieni ni mfuko gani ukitaka chako unapewa bila zengwe?

NSSF ndio mfuko wa aina yake maana ndani ya miezi 6 unakula full fungu lako tokea mwajili wako alipopeleka vithibitisho vya michango yako niambieni shirika gani lina speed kama hiyo?

NSSF muda wowote bila zengwe ukitaka kwenda kucheki michango yako unapata na full detail tena umekaa kwenye kiyoyozi bila urasimu kama mashirika mengine mara printer mbovu mara sahihi ya bosi ni shirika gani lipo hivyo?

NSSF ndio shirika pekee linalochangia maendeleo ya nchi kama wahisani kwa majengo. elimu na miradi mbali mbali ni shirika gani lingine lipo hivyo?

Narudia, WIVU, FITNA, MAJUNGU ni jadi ya watanganyika. mwacheni Dr. Rama achape kazi.

Shame.
 
Hela watukate warejeshe bila faida , na kodi watukate 120000 TSH +30% ya kinachozidi Laki saba....! mfanyakazi ni huyohuyo umtungie sheria ya kupata hela ya jasho lake mwenyewe kwa kweli nchi hii kubwa lakini hatutaenea. ni waalati wabunge wasijejaribu kupitisha hili liwe sheria watakuwa na wakati mgumu mno kwenye majimbo yao.
nawakilisha
:A S 465:
kuna habari nimezipata kutoka mtu wa ndani NSSF kuwa pesa zetu ziakazimeliwa zote na serikali sasa wanakuja kutunga sheria mpya mwezi wa saba bungeni kuwa mwanacha hutapewa pesa zake mpaka utakapostaafu.mimi nadhani kwa wale wanachama wa NSSF na mifuko mingine ya jamii tutakuja kulia kama wazee wa africa mashariki tusipokuwa makini na hii serekali,
naomba kuwasilisha
source ---nssf

Hakika tunaweza kusema ni kitanzi kwa wafanyakazi masikini wa Tanzania.Habari za kuaminika kutoka wizara ya fedha na mifuko mbalimbali ya kijamii zinasema serikali inajiandaa kupeleka mswada bungeni katika bunge lijalo kwamba ni sharti ufikishe miaka 55 ndipo uweze kupata mafao yako.
Kwa hivi sasa kama mfanyakazi ataacha kazi katika makampuni mbalimbali binafsi anaweza kupata pensheni yake ndani ya miezi sita.Hali ni hiyohiyo kama mfanyakazi ni mgonjwa anahitaji matibabu basi aweza kupata mafao yake.
Lakini kwa mswada huu mpya unaotarajiwa ukipitishwa mfanyakazi yeyote katika makampuni na mashirika mbalimbali hataweza tena kupata mafao yake hata kama ameacha kazi mpaka atakapofikisha miaka hiyo 55.
Habari zaidi zinasema mifuko hii ya kijamii hasa NSSF yamewekeza katika miradi mikubwa isiyo na faida na pia yamekuwa yakikopwa na serikali lakini inashindwa kulipa kwa wakati.Hali hii imesababisha fedha za wanachama kupukutika na njia pekee ya kuepuka aibu hii ni kuandaa mswada kama huu utakaoacha kilio kikuu kwa wafanyakazi nchini.
 
Hivi serikali ilisema umri wa mwanadamu kuishi ni miaka mingapi vile?
 
Ndio Mkuu wangwana hupenda argument zenye nguvu na documented kama hiyo yako. Naifagilia. Wabunge waikomalie serikali kama walivyoikomalia mpaka wakawafire mawaziri. Wasikubali mswada huo. Magazeti na wadau wengine kama wewe waendelee kufanya advocacy.
 
Tume ya katiba nae naona anaanza kunitafuta. Inauma sana yaani j'3 nilkuwa naongea na rafiki yangu mmoja yeye ni mfanyakazi wa serikalini na ana 48yrs akanambia anataka aache kazi ili angalau apate mafao yake ya NSSF yamsaidie kufungua biashara maana anadai mpaka sasa hana nyumba, watoto hawapati elimu bora na anazidi kuwa masikini. Leo hii hawa wapumbavu wanakuja na porojo za namna hii.

Hivi watumishi wa serikali michango ya inapelekwa NSSF ?
 
Hii sheria ni
kandamizi na haiendani na wakati tuliopo. Wanadhani kila mtu anafanya
kazi serikalini? Nani anataka kutumikishwa hadi awe na umri wa miaka 55?
Hawa wanaojaribu kufikiria kuzuia watu kuchukua pension zao hawana
mawazo ya kijasilia mali na wana akili mgando. Kwa mfanyakazi mwenye
mkataba wa miaka mitano na ameanza kazi akiwa na miaka 25 ina maana
akifikisha 30 anamaliza mkataba wa kazi na kujikita katika biashara. Je
asubirie kwa miaka 25 ndio aje alipwe pensheni yake? Huu ni uwendawazimu
wa serikali ya CCM, hawana mawazo ya 21st century yenye kujikita zaidi
kwenye kujiajili baada ya kufanya kazi kwa muda mfupi ya kuajiriwa.
Mfano mimi mzigo wangu saizi unakaribia 30M na lengo langu ukifika 40
miaka miwili ijayo niachane na kazi za kuajiliwa nikajasilie mali na
nitakuwa nimebakiza miaka 20 kufika 55...

Yani nilikuwa ninekuandalia majibu mazuri sana wewe na wenzio lakini simu imeyaondoa. inaniuma sana..why u ar not informed guys??? dah..ngoja nipate komputa nije niwa-inform!
 
Hii tetesi nilishawai kuisikia kwa mkurugenzi mkuu wa lile shirika linalo simamia haya mashirika ya hifadhi ya jamii " Wakati ule alisema wao wanataka kupendekeza kua mwanachama asiruhusiwe kuchukua mshiko wake mapaka atakapo fikia umri wa kustaafu" kwa hiyo nadhani ndio hivyo wanataka kuipeleka hii hoja bungeni? na Hoja yake ilibase kua kuna wazee walichukua mafao yao mapema na sa hivi wanataabika, kwa hiyo wameona ni bora wazuie mtu kuchukua chake mapema! " niliposikia hii kitu aisee nikasema ngoja niwai kuchukua mshiko wangu mapemaa!
Ila nnachowaaomba wabunge wetu wasipitishe hii hoja, other wise wamwachie mwanacahma mwenyewe kuamua ni lini anataka kuchukua mshiko wake..
 
Back
Top Bottom