Kitambulisho kwenda Zanzibar

Ni sahihi sana mkuu.
Sidhani kwa mfano mikoa ya Kigoma, Katavi, Mwanza, Shinyanga na Tabora kwa wanaostahili kuwa na kitambulisho cha mpiga kura walizembea maana bila kitambulisho hupati tiketi ya treni.
 
Sio ujinga ni sahihi ki usalama, ili kukitokea ajali ni rahisi kugundua bado nani hajaokolewa na anatokea kata gani. Mbona hata kwenda mwanza au Safari yeyote kwa Ndege ni hivyo hivyo, yani lazima uwe na kitambulisho.
Unajaribu kutueleza kwamba ajali hutokea ukisafiri kwenda Zanzibar peke yake? Ukisafiri kwa mfano toka Dar kwenda Mwanza, huwezi kupata ajaili, ..na unahitaji hiyo barua ya serekali ya mtaa? ..ni wajibu wa chombo chochote kinachokusafirisha kuwa na taarifa zako muhimu, kwa madhumuni uliyoyataja!
 
Mkuu cheti cha kuzaliwa hakina sifa ya kuitwa kitambulisho.
That is my point!!
 
Kwahiyo hapa unakataa au unaunga mkono?
 
Sisi watanzania tabia ya uongo hatuwezi kuacha.
Mtu kwao anajulikana kwa jina la John akienda kwingine anajulikana kwa jina la Juma, swala la kuweka utaratibu wa vitambulisho bandarini ni la msingi sana ili kupata majina halisi ya watu, tena ni vizuri utaratibu huu na mamlaka nyingine wauige ili kupunguza wimbi la watu ambao maiti zao hushindwa kutambulika na ndugu zao endapo ajali ikitokea
 
Wapige passport size afu waende kwa Uongozi wa mtaa au kijiji wapewe barua ya utambukisho. That's over Sir!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…