KERO Kitambulisho changu hakitoki toka mwaka 2020-2022

KERO Kitambulisho changu hakitoki toka mwaka 2020-2022

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

AJIRA SASA

Member
Joined
Sep 5, 2018
Posts
5
Reaction score
5
Habari,

Nilijiandikisha na nida mwaka kati ya mwaka 2020-2022 nikapatan namba vizuri tu lakini baada ya hapo sijawahi kupata kitambulisho changu mpaka leo.

Licha ya juhudi zangu kufuatilia katika ofisi mbalimbali niliambiwa ya kuwa kitambulisho kipo hatua ya mwisho kwenye mchakato wa kuprintiwa.

Inapita miezi na miezi lakini kila ukipiga simu jibu lao ni hilo hilo. Naomba muwaulize nida ni lini hizi card zitaprintiwa maana imekuwa wimbo wa kila siku na hakuna majibu ya kueleweka.

Kwa kukosa vitambulishp vya nida tunakosa huduma za msingi na kukosa fursa nyingi sana.

Swali langu kuna shida gani Huko nida?
 
Pole sana, mambo ya serikali ndivyo yalivyo...


Cc: Mahondaw

Tatizo ni CCM, mambo ya kitaalam wanaweka siasa na porojo
wanatengeneza matatizo ya kiutendaji makusudi ili baadae wakija kuyatatua tuwaone mashujaa, tuwashangilie na kuwasifu kumbe wao ndio kikwazo
 
NJE YA MADA

NIDA na viongozi wakuu wa Serikali watoe tamko khs vitambulisho vile vilivyo wekewa tarehe ya kuisha muda wa matumizi
kwamba vinatambulika au vitupwe havina kazi
 
Back
Top Bottom