Kitakachoikumba Dunia mwaka 2036

apophis asteroid iligunduliwa 2004 na ndio iyo habari ya iyo asteroid kuipiga dunia zilipozuka lakini kwa uchunguzi uliofanywa na torino impact hazard scale 2013 umegundua uwezekano wa apophis kuiangukia dunia na kuleta madhara ni asilimia 2.7 tu.
 
Naona watoto wameiharibu thread,ingejadiliwa kwa dhumuni jema tungejifunza mengi...


Mzee,tazama filamu ya Temonator II :Judgement Day utaelewa nini kitatokea wakati huo...

Naelewa inawezekana uliwahi kuiangalia filamu hiyo kishabiki au kama filamu tu lakini hukuelewa hasa ujumbe nyuma ya filamu hiyo...

Iangalie tena na tena na zingatia kuelewa kinachosemwa na dhumuni la hiyo filamu utaanza kunielewa taratibu....

Ukishindwa rudi uje uniulize...
JF imevamiwa
Ubora wa zamani umepotea mkuu
 
31946315_1928447503845735_2447714343165362176_n.jpg

Dunia yetu ni sayari ya tatu kutoka kwenye jua. Mirihi (“Mars”) ni ya nne na Mushtarii (“Jupiter”) ni ya tano na kubwa kuliko zote katika mfumo wa jua wa Sol.
Katikati ya Mirihi na Mushtarii kuna ukanda wa mawe, wenye upana wa kilometa milioni 550, unaoizunguka sayari ya Mushtarii kwa mwendokasi wa kilometa 80,000 kwa saa. Katika ukanda huo kila jiwe lina mzingo wake (“orbit” yake) na lina nguvu yake ya uvutano, ndani ya nguvu kubwa ya uvutano ya Mushtarii.
Kwa sababu ya tofauti katika nguvu za kiuvutano (“gravity resonance”) wakati mwingine mawe hayo hugongana kwa kani kubwa zaidi hivyo kusababisha mengine yaende nje ya mizingo yao asilia, na kumeguka kutoka katika nguvu ya uvutano ya Mushtarii, na kudondoka angani, kama ilivyokuwa kwa Apophis.
Apophis ni jiwe linalotegemewa kugongana na dunia yetu mnamo mwaka 2029. Lakini kwa sababu ya tundu dogo lililoko ndani ya nguvu ya uvutano ya Dunia, lijulikanalo kitaalamu kama “gravitational keyhole”, lenye kipenyo cha kilometa 2.5, litakapopita ndani ya tundu hilo, Apophis halitaigonga Dunia! Lakini litajipanga tena kuigonga Dunia mnamo mwaka 2036 au mwaka 2068, kama mwaka 2036 litapita tena ndani ya “keyhole”.
Iwapo Apophis halitapita ndani ya “keyhole” nini kitatokea duniani? Kwa sababu ya msuguano wa molekuli za hewa, Apophis, litakapoingia katika angahewa ya Dunia litawaka moto lote (kama linavyoonekana kwenye picha); na kabla halijagusa ardhi kwa kishindo kikubwa, mionzi ya gama itasambaa dunia nzima ndani ya muda mfupi tu na itaua kila kiumbe hai kitakachoonekana juu ya uso wa Dunia! Ni vile viumbe tu vitakavyokuwa chini ya ardhi ndivyo vitakavyopona. Kwa hiyo, haitaathirika Amerika peke yake. Dunia nzima itaathirika.
Kuna njia kuu tatu za kuzuia Apophis isigongane na Dunia mbali na “keyhole”, ambazo gharama zake ni kubwa mno kwa nchi moja peke yake kujitolea.
Njia ya kwanza ni kutumia mabomu ya nyukilia: Kabla Apophis halijafika kwenye angahewa ya Dunia, wanaanga wanapaswa kutua juu yake – huku likiendelea kushuka – na kupandikiza mabomu ya nyukilia kisha wao kuondoka haraka, na mabomu hayo kulipuka, hivyo kusambaratisha jiwe zima.
Hata hivyo, wanasayansi wanaona njia hiyo si nzuri sana; kwani Apophis halitasambaratika lote, halitasagika kabisa, litasambaratika katika vipande vidogovidogo. Vipande hivyo vikianguka kwenye ardhi ya Dunia bado vitaleta madhara makubwa.
Njia ya pili ni kutumia nguvu ya uvutano (“gravity tractor”): Katika njia hii wanasayansi itawabidi watume chombo cha angani, chenye uwezo wa kuzalisha nguvu kubwa ya uvutano kuliko ile ya Apophis.
Chombo hicho kitaruka hadi chini ya Apophis na kuanza kushuka na Apophis huku, wakati huohuo, kikifungulia nguvu yake ya uvutano ili nguvu hiyo ipambane na nguvu ya uvutano ya Apophis.
Kwa sababu nguvu ya uvutano ya chombo cha angani itakuwa na nguvu kubwa zaidi kuliko ile ya Apophis, chombo cha angani kitaanza kuukokota mzingo wa jiwe la Apophis taratibu na kuusogeza mbali kidogo na mzingo wa dunia yetu; ili Apophis litakapofika duniani lipishane na dunia yetu kwa angalau kilometa elfu kadhaa. Hapo pia bado kuna ubishi wa nani agharamie chombo hicho na kwa faida ya nani.
Njia ya mwisho ni njia ya kutumia mwanga wa jua (“solar sail”): Wanasayansi hapa itawabidi wafanye kitu ambacho hawajawahi kufanya: Kutengeneza vioo vikubwa, maelfu kwa maelfu, watakavyovining’iniza katika eneo kubwa la angani ili vikusanye umeme (“photons”) kila baada ya dakika nane kutoka kwenye jua na kuuelekeza umeme huo moja kwa moja hadi kwenye jiwe la Apophis.
Nguvu ya pamoja itakayotengenezwa na vioo hivyo italisukuma Apophis na kuusogeza mzingo wake mbali kidogo na mzingo wa Dunia ili vipishane. Hali kadhalika, njia hii gharama yake si ndogo na hakuna nchi itakayojitolea kuingia gharama kubwa kiasi hicho wakati kila nchi itaathirika.
Kama Amerika inatawala anga na inatawala Dunia, kama alivyowahi kusema Rais David Eisenhauer mwaka 1957, jukumu la kulilinda anga na Dunia ni la Amerika.
jukumu la kulilinda anga na Dunia ni la MUNGU siyo Amerika acha kuabudu sayansi na Amerika.[/QUOTE]
 
Introduce fear to these motherfuckers and control them.....

Only fools will agree with this....
 
kwa vile dubwana la NIBIRU lilipita, na hili litapata tu. waache kutuweka roho juu. stress za maisha yetu tu zinatosha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom