Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,314
Mohamed Said ni ukweli ulio wazi kwamba Historia inaweza kuthibitisha chochote kutegemea na yule anayetafiti na malengo pamoja na msukumo ulioko moyoni mwakeKapwila...
Kuna kitu nimekiona nimeona nikurudie nikuonyeshe ili upate yakini
kuwa kitabu changu kilikuja na taarifa muhimu sana katika historia
ya uhuru wa Tanganyika.
Soma hapo chini:
Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu kuhusu:
''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,
'' Minerva Press, London 1998.
''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary; Alexander M. Tobias and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''
Kapwila,
Huyu Alexander M. Tobias alifukuzwa chama kwa usaliti katika mkutano
wa kuunda TANU July 1954 kwa sababu alichukua majalada ya TAA
akawapa Special Branch.
Habari hizi alinipa marehemu Mzee Germano Pacha mmoja wa wale
waasisi 17 wa TANU.
Kapwila,
Bado unaamini kitabu hiki ni cha kupuuzwa?
[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.
Nkwesa...Mohamed Said ni ukweli ulio wazi kwamba Historia inaweza kuthibitisha chochote kutegemea na yule anayetafiti na malengo pamoja na msukumo ulioko moyoni mwake
Nkwesa...
Hilo usemalo si kweli.
Wewe uliyajua haya kabla?
Msukumo wa moyo ungekuwa ndiyo wa kuamua basi tungebaki na historia
ya TANU ya Chuo Cha Kivukoni.
Usitishike ni historia tu niliyoelezwa na wazee wangu.
Huenda wale waliokuja TANU baadae hawakuyajua haya.
Faiza, nimekundikia mtiririko mzima ili kukurahisishia; nikiandika nambari za post itakupotezea muda wa kutafuta. Hebu kanusha, au kuna mtu ametumia ID yako?
Vv
Kaka mohammed with all respect to you, i believe mtu anaye waambia wenzio "unazungumza pumba" "acha ujinga" "wewe ulisoma kweli" kwangu mimi siyo sign ya good and progressive conversation, i believe kama wewe katika honest dilagoeus hata kama sikubaliani, siyo kupondana kwa speliing mistakes au kama above, which to me is a sign of inferiority complexSadoliki,
Usiulize vyeti vya Maalim Faiza.
Inaelekea wewe ni mgeni hapa Majlis.
Faiza kajipambanua sana kama msomi makini si wa vyuo alivyosoma akiwa
keshakua bali hata vile vyuo alivyosoma akiwa na miaka 5/6.
Fanya utafiti mdogo.
Rejea nyuma humu Majlis soma michango yake utamjua.
Hapa Majlis ukileta habari ya vyeti utatufukuza wengi ingawa hatuna vyeti lakini
kwa kweli kwa namna yetu tunachangia kama mnavyochangia wasomi kama wewe
wenye vyeti.
Mtu hafukuzwi hapa barzani kwa kukosa cheti wala hakatazwi kuchangia kwa kukosa
cheti.
i am sorry to say, jibu lako limekaa kishabiki zaidi kuliko ulivyoeleza mwanzo. i am thus not interestedSadoliki,
Huyo ndiye Maalim Faiza.
Je, bado unataka kuona vyeti vyake?
Lugha ni lugha inaweza kuongelewa na watu wasokuwa waarabu, na sio kweli kuwa asili ya Waarabu wote wanaongea kiarabu toka kina Ismail, mtu mweusi huwezi kuwa mwarabu kwa asili unachanganya sana. Hivyo usiliseme kabila kuwa ndio asili ya watu maana hata WaTutsi wanaongea lugha ya Kibantu japo sii Wabantu.
Kaka mohammed with all respect to you, i believe mtu anaye waambia wenzio "unazungumza pumba" "acha ujinga" "wewe ulisoma kweli" kwangu mimi siyo sign ya good and progressive conversation, i believe kama wewe katika honest dilagoeus hata kama sikubaliani, siyo kupondana kwa speliing mistakes au kama above, which to me is a sign of inferiority complex
you are trying to write history, with semantics, haiwezekani hata kama ulizqaliwa kariakoo, justification ya kuwa mtu wa kutoka kenya kahamia tanga na kawakuta wenyeji waarabu ni theory yako na wenzako unewajua , kwangu mimi it make no sense na sitaki kupoteza muda ku argue on it, people might not notice the differenceUkija na pumba usiambiwe?
Ukiwa unaambiwa Mbantu kahamia Afrika ya Mashariki na kauta wenyeji na unaoshwa historia za wana historia waliobobea na wewe bado unabisha tu bila ushahidi wowote, basi kwa kuwa unaamini tu ulichofundishwa cha kujazwa ujinga.
Hakuna mahala nimeuliza "wewe ulisoma kweli?", huwa nnauliza, jee shule ulienda kusomea ujinga? kumbuka hilo.
you are trying to write history, with semantics, haiwezekani hata kama ulizqaliwa kariakoo, justification ya kuwa mtu wa kutoka kenya kahamia tanga na kawakuta wenyeji waarabu ni theory yako na wenzako unewajua , kwangu mimi it make no sense na sitaki kupoteza muda ku argue on it, people might not notice the difference
Unajua wewe unachekesha sana yaani unauliza maswali ambayo majibu yake unayatoa Google. Unauliza kuhusu Iraqw wakati wewe mwenyewe unatoa majibu yako Google,halafu unaona umeuliza swali gumu sana watu wanapokupuuza..Umechanganya mambo mengi sana mpaka nnashindwa ku "concentrate", sasa kama hautaki kujuwa North na South na wanahistoria walioboobea wanatumia "terminology" hiyo itakuwa wewe huna haja ya kujuwa asili za watu bali unataka ubishi wa kijinga.
Hilo la Makabila ya kibantu kufika 1,000 si muhali hata yakifika 2,000 lakini Wabantu watabaki kuwa Wabantu na Watabaki kuwa Walikuja Afrika ya Mashariki.
Unajuwa maana ya Bantu?
Nnakuwekea hizo "proofs" usome mwenyewe ili usije ukauliza "source". Hakuna aliyezaliwa anajuwa kila kitu, tunasoma, tunajifunza, tunajuwa, unless uwe ni mjinga wa kuzaliwa ndiyo utakataa kusoma waanazuoni waliobobea fani zao na proofs zao, unaweza kuwapinga walichoandika ukaja na chako chenye mashiko zaidi lakini huwezi kuwacha kuwasoma waliyoyaandika watu wengine. Sidhani kama wewe uko huko.
Nnankushangaa sana unapoona kuwa ni kituko mimi kuweka links za maandiko ya wanahistoria ujisomee mwenyewe ili yakuingie.
Unajaribu kufanya "character assassination" ya kijinga. Hunipati huko.
''The Torch on Kilimanjaro'' Kitabu Kilichofitiniwa Kisiingizwe Katika Mtaala wa Shule za Msingi za Tanzania Aliyesimama juu ya boneti ya Land Rover akihutubia wananchi ni Mwalimu Nyererena picha ya pembeni ni Nyerere na Kenyatta. Mwandishi akitoa maelezo kuhusu kitabu "The Torch on Kilimanjaro." |
Mohamed Seif Khatib katika Uzinduzi wa Kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro'' Kilimanjaro Kempinski Hotel kulia kwake ni Sheikh Abdillah Nassir |
|
Mwalimu akikiangalia kitabu ''The Torch on Kilimanjaro,'' ni kitabu kilichochapwa na Oxford University Press (OUP) Nairobi. Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa kuchapa vitabu kwa ajili ya shule za msingi madhumuni yakiwa ni kumsomesha mwanafunzi lugha ya Kiingereza na wakati huo huo ajifunze na historia ya nchi yake ili kujenga uzalendo. Waandishi kutoka Afrika ya Mashariki waliandika vitabu kiasi ya 15 isipokuwa Tanzania. OUP walimfuata mwandishi na kumuomba aandike kitabu kimoja ili angalu Tanzania na wao wawemo katika orodha ya nchi zilizoshiriki katika mradi ule wa kusomesha lugha ya Kiingereza Afrika ya Mashariki. Mwandishi akapeleka mswada Nairobi. Baada ya muda alikwenda Nairobi kuonana na mhariri ili kurekebisha mswada. Mhariri akasafiri hadi Dar es Salaam baada ya kupata marekebisho na kazi ikakamilika. Kitabu kikachapwa. OUP wakafanya dhifa kubwa sana ya kukizindua kitabu Kilimanjaro Kempinski Hotel ambako wakuu wa Wizara ya Elimu walikaribishwa pamoja na vyombo vya habari. Mgeni wa heshima alikuwa Mohamed Seif Khatib. Waalikwa wote walipewa nakala moja ya kitabu na mwandishi alikieleza kitabu mbele ya hadhira ile. Kwa upande wao OUP walikisifia kitabu kile kuwa kitachangia katika watoto wa shule za msingi kujifunza Kiingereza na historia ya nchi yao hususan historia ya Mwalimu Nyerere alipoanza kudai uhuru wa Tanganyika mwaka 1954 hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1961. Aliposhuka tu kutoka kwenye jukwaa watu wa televisheni na magazeti wakamzunguka kumhoji kuhusu kitabu kile. Tanzania kitu chochote kinachomuhusu Nyerere kinauzika. Mwandishi na mchapaji OUP walitegemea makubwa kutoka kitabu kile. Haikuwa hivyo. Kitabu hiki kimepigwa chenga kuanzia mwaka 2007 licha ya juhudi nyingi za OUP kuwaandikia Wizara ya Elimu kuwaomba wakiingize katika mtaala wa kusomesha lugha ya Kiingereza. OUP walimweleza mwandishi kuwa wao hawajui kwa nini kitabu hiki chenye historia ya Mwalimu Nyerere hakitakiwi wakati kule Kenya kitabu cha Jomo Kenyatta ''The Kapenguria Six'' kilicho katika mradi huu kipo katika mtaala wa shule za msingi na kinasomeshwa. The Kapenguria Six Mswada mpya 'The School Trip'' ambao mwandishi aliwapa OUP na wakaupokea kwa ajili ya uchapaji baada ya kuona uzuri wa kitabu kile cha kwanza, OUP wameghairi kukichapa kitabu na maelezo ni kuwa mwandishi hauziki nchini kwake lau kama ana kipaji cha uandishi wa hadithi za watoto. Hata hivyo OUP walimshirikisha mwandishi katika mradi mwingine kwa ajili ya vitabu Afrika ''The Mermaid of Msambweni and Other Stories'' (2007) kitabu cha mkusanyiko wa waandishi kutoka nchi tofauti za Afrika Tanzania ikiwakilishwa na mwandishi huyu. OUP wala hawakushughulika kukitangaza kitabu hiki hapa Tanzania.Ndiyo maana husikika minong'ono kuwa kuna kitu katika uendeshaji wa serikali kinaitwa ''Mfumokristo.'' Huu mfumo inasemekana una watu wake unaowapenda na kuwatumikia. Je, Wizara ya Elimu ni moja ya taasisi zinazoongozwa na ''Mfumokristo?'' |
Unajua wewe unachekesha sana yaani unauliza maswali ambayo majibu yake unayatoa Google. Unauliza kuhusu Iraqw wakati wewe mwenyewe unatoa majibu yako Google,halafu unaona umeuliza swali gumu sana watu wanapokupuuza..
Hapa hatushindani, nimekuuliza tu vizuri na ushahidi wako wa Google ya kwamba Ikiwa hayo makabila (Sandawe na Baruge) ulodai kwamba ndiyo Makabila yenye asili ya Tanganyika, nilipokuuliza kama makabila hayo sio Wabantu ukanionyesha sio kwa sababu Asili yao wametoka North na South ina maana hata wao sio wenye asili ya Tanganyika.
Na kutoka North au South haina maana sio Wabantu ikiwa wewe unaamini Wabantu walitoka West Afrika iweje kutoka South au North sio wabantu. Huoni kama unajichanganya, huku unakubali hiki huku unakataa kingine chenye maana ile ile. Ni record gani inaonyesha West Afrika kulikuwa na Wabantu kabla ya Tanganyika na ndio asili yao isiwe Waarabu pia maana unawapenda sana.
Sasa kwa wewe msomi tuambie kina nani wenye Asili ya Tanganyika maana hata hao Wa Iraqw ambao ni Wambulu ambao pia ni Wahamiaji kutokana na asili yao ya wachungaji kuhama kutafuta nchi za malisho ya mifugo yao. Na kuhusu waarabu wewe mwenyewe umeweka kipande hicho hapo juu na kimesema nini baada ya highlight yako kuwa:- Arab Identity is based on one or More genealogical, Linguistic or Cultural.
Sasa wewe unataka kunambia mwarabu ambaye hajui kiarabu sio Mwarabu maana hapa Canada wapo wengi tu. Na hata watoto wa kibantu wasojua lugha hata moja ya Kibantu. Wajamaica, Wahaiti, Wamarekani weusi hawa ni wa asili gani? Wapo waswahili hapa hapa Dar hawajui hata lugha moja zaidi ya kiswahili hawa wana asili gani?
Hakuna record yeyote iliwahi kuonyesha Wabantu sio wenyewe wa Tanganyika kwa sababu Tanganyika sio Manyara wala Arusha peke yake na haiwezekani kabila dog lilohamia likawa ndio kabila kubwa Tanganyika pasipo kupigana vita na kuwaua wenyeji.
Na halafu kumbuka waloipa Zanzibar jina la ZenjBar sio Wa Oman wala Saudia ila Washihir, Washiraz na Waburush walokuja kwanza kabisa kufanya biashara ya viungo, dhahabu na vito. Kwa hiyo huwezi kutumia lugha moja kutafsiri neno kwa sababu wewe unakijua kiarabu cha Karne ya 21. Your very wrong na wewe pitia hapa:- The name Zanzibar came from a combination of two Arabic words, 'Zinj', meaning black, and 'barr', being the Arabic word for land, the result meaning 'Land of the Blacks'.
Ok naona twenda moja baada ya jingine. Nionyeshe mahala panaposema maana ya Cush sio Weusi. na Cush ties sio lugha ya watu weusi. Neno weusi walimaanisa kundi gani? Hiyo website ya Wazanzibar wenyewe utasemaje mwandishi hajui maana, ikiwa wewe mwenyewe unatoa ushahidi wako ktk website kutupinga sisi Wabantu tunaoijua Asili yetu. Kama huyo Mzenji hajui, kwa nini na wewe usiwe hujui unapopingana na Wabantu!...Tazama unavyojikanganya tena.
Link niliyokuwekea inakuonesha wazi kuwa hao ni Cushite na si Bantu na kama ulikuwa umenisoma vizuri bila kiherehere ungeona na DNA proofs, zinazoleta mkanganyiko wa historia na imefikiwa kusema amma Tanzania au Ethiopia, unajuwa kwa nini? very simple, ni amma hayo makabila yalitokea North kuja South amma yalianzia hapo Tanzani kwenda North.
Hakuna Mbantu aliyetokea North, hakuna historia hata moja inalosema hilo, kama unayo yako tuwekee. Palipoandikwa wametokea North utakuta amma Cushite amma Semite. Kwa hiyo usichanganye mambo.
Mwisho wa yote nikakuwekea link inayoonesha ni nani Waarabu na wapi kwao na hiyohiyo link inaonesha yale yale niliyokuuliza uliyoshindwa kuyajibu. Pole sana.
Nnajuwa hapo ukweli umeuelewa lakini unataka tu, kuchanganya mambo, watu kama wewe nawaelewa sana wala hamnipi shida, mnajifunza kwa kupopowa.
Naam, nnakuwekea link kwa kuwa sasa hivi Library zipo mtandaoni, unataka nini zaidi ya hicho, hata teknolojia hauithamini? Unashangaza sana. Leo hii ni kuna "dream world" kwa wapenda historia kwa jinsi tulivyowekewa maktaba na archives za dunia humuhumu mtandaoni. Cha ajabu hapo nini? au hilo kwako ni kituko?
Huyo aliye translate neno Zinj kutoka hiyo website uliyoiweka haijuwi maana ya Zinj. Na pia haijuwi maana ya "barr", barr nilikuelezea maana yake hususan kwa Kiswahili ambayo haina utata kabisa ni bara. Land kwa kiarabu ni "ardh" ndipo kwa Kiswahili tukapata neno ardhi na si "barr".
Kwa hiyo hukohuko kwenye mtandao ulpoiowa hiyo maana wamepotosha na ndiyo maana nawe umepotoka kwa kuwa Kiarabu ahaujuwi kwa hiyo ulichokisoma ukaona aaah, hiki ndiyo sawa, basi hata hutumii akili yako japo kiduchu ukatumia Kiswahili unachokijuwa ambacho kipo karibu zaidi na Kiarabu kupata tafsiri sahihi? Unashangaza.
Nnaona kwa kuja na maana hiyo uliyoitoa kwa ku google pia mtandaoni, niliyoibomonda hapo juu, ya neno Zinj inammanisha haijuwi maana yake, mimi ntakupa jibu.
Maana ya Zinj ni pua-pana. Zinj Bar - Bara la watu wenye pua pana. Unajuwa kwanini wakawaita hivyo? kwa sababu kama ni weusi hata wao hao Waarabu kwa wingi wao ni weusi (post yangu kuhusu Arabs inafafanuwa hilo) sasa wewe mwenyewe mweusi halafu ukamwite mwenzako mweusi si itakuwa ni kituko? Tofauti ya weusi wa Magharibi na Mashariki ni pua zao, hilo halina shaka kabisa, tazama nchi zilizotajwa kwenye post ya ARABS niliyokuwekea juu, utayakinisha hilo. Na hiyo ni moja ya Tofauti ya Semites na Bantus ni pua za na si rangi zao tu.
Sasa hiki nilichokupa hapa "orijino" changu na nnaku refer kwenye links ili kukuhakikishia tu point yangu.
Kuhusu Wabantu kuwa sio wenyewe Tanganyika ni kosa kusema hivyo, inabidi uelewe, wewe ulivyohamia Dar ulikutana na wenyeji wa Dar. Na ukaishi mpaka ukawa na wewe ni mwenyewe Dar na hilo halikupi haki ya kusema na hao uliowakuta si wenyewe.
Kwa mantiki hiyohiyo Semites na Cushites wapo Tanganyika na wao pia ni wenyewe tena wao ni wa zamani zaidi ya Wabantu kutokana na historia.
Hilo la Wahindi na Washihiri ni mada nyingine kabisa, ndiyo maanaa hapo awali nikakusihi ununuwe kitabu kiitwacho Empires of the Monsoon, cha Richard Hall, ungepata majibu ya yote hayo. Na nnakuhakikishia yule mtu anajuwa kuandika, hutatamni kukiweka chini ukianza kukisoma, utapata kuelewa humo kuwa Vasco Da Gama aliitazama Kilwa kwa mbali kutokea kwenye meli yake hakupato kutia mguu wake Kilwa. Mabaharia wake tu walishuka? Jee, kwanini? jisomee.
Pia utapato kujuwa hili ji bahari kubwa kwanini likaitwa la Hindi? ni nani aliyeliita hivyo?
Kuna uwenyewe na uenyeji. Uafrika si Ubantu pekee na pia Utanganyika si Ubantu pekee ni zaidi ya hapo, sana tu.
Hujajibu bado, Jee unajuwa maana ya Bantu?
Mohammed Said,
Mimi nakukubali sana katika maelezo yako wala sii kwamba hakuna ukweli wowote isipokuwa Historia ya Nchi huandikwa WATU walohusika na kwa minajiri gani. Kama ni UHURU wa Tanganyika kina AbdulWahid hawakuutaka UHURU wa Waislaam wa Tanganyika isipokuwa UHURU wa WATU wote wa Tanganyika haikubagua dini wala Kabila. Kwa hiyo unapoandika kuhusu wazazi wako ungewataja tu majina yao na michango yao, basi kitabu chako kingepata sifa kubwa sana nchini pengine hata kusomwa mashuleni.
Kosa ullifanya ni kupeleka Udini zaidi ya kuonyesha michango yao isipokuwa mchango wa Uislaam katika Uhuru wa Tanganyika kiasi kwamba ukawaweka hata watu walopingana na TANU juu ya Uhuru wa Tanganyika kina Takadir na AMNUT kuwa katika mashujaa walosahaulika. Kama kweli kweli waislaam walitaka Uhuru wao basi wangekiunga chama hiki cha AMNUT mkono badala ya TANU kilichochanganyikana na watu wa makabila mbali mbali.
Kwa nini unapenda sana kumshusha Nyerere pamoja ya yote alotutumikia? kwa sababu Mkristu au kwa sababu wazee wako hawakupewa nafasi. Mzee Ali Sykes hadi anatutoka alikataa siasa kabisa yeye mwenyewe na historia inatuonyesha wazee wengi waliacha siasa baada ya kutimiza wajibu wao wakafanya biashara zao.
Wewe ni mwandishi mzuri sana na unajua kuzitafuta habari lakini unakumbwa na hili jinamizi la Udini ambalo kama nilivyokwambia wazungu wanapenda sana kuwasoma watu kama wewe kwa sababu wanajua upeo wa fikra zako na utaweza kuwa hatari kiasi gani. Na katika hali kama ya leo ya Ugaidi unaweza kuwepo katika list ya watu wanaotazamwa sana kwa sababu wanaamini watu kama wewe ni hatari na je umeweza vipi kuwalaghai wengine kuwajaza chuki dhidi ya wakristu au watu wengine.
Haya yalifanyika sana Uingereza wakiwaachia masheikh wakizungumza wazi Trafalgar Square, kumbe wakiwachunguzana kuchukua picha za watu wanaohushulia mara kwa mara mihadhara ile, Ilipoanza tu habari za Ugaidi wakakusanywa hata wasokuwemo na kwa sababu kama hizi usidhani unafanya la maana sana ikiwa ncjhi yako yenyewe kitabu chako kimepigwa marufuku. Think big mkuu wangu nakuasa tu.
Ok naona twenda moja baada ya jingine. Nionyeshe mahala panaposema maana ya Cush sio Weusi. na Cush ties sio lugha ya watu weusi. Neno weusi walimaanisa kundi gani? Hiyo website ya Wazanzibar wenyewe utasemaje mwandishi hajui maana, ikiwa wewe mwenyewe unatoa ushahidi wako ktk website kutupinga sisi Wabantu tunaoijua Asili yetu. Kama huyo Mzenji hajui, kwa nini na wewe usiwe hujui unapopingana na Wabantu!...
Ni ushauri tu nilompa Mohamed Said, yeye anaweza uchukua ama kuuacha. Wewe una haki na kila sababu ya kufuata, kusoma unalolitaka sijakukwaza. Tuendee la mada yetu acha hizi habari za kubwabwaja maana wewe ndio unabwabwaja hovyo na Uarabu wa kupaka na haki ya Mungu... nakushangaa sana...Mpaka leo wanazungumza sana lakini si Trafgar Square ni Hayde Park Speakers Corner. Tena nnakuwekea link umsikilize sana Blagrovr, huyu ni favorite wangu wa Hyde Park: https://youtu.be/wZN2eAe_iuY
Ni favorite wangu kwani ana high capacity ya general knowledge.
Kitabu cha Mohamed Said kipo, mimi nimekinunuwa Dar.
Vipi unataka kutuamnisha bila "nukuu: hata moja kutoka kwenye kitabu unachokisema? hautuoneshi Mohamed Said kaandika "uchochezi" huu ukanukuu? Tujionee wenyewe? Tukuamini vipi? Unakuja na kubwabwaja na kuhororoja bila kuleta ushahidi? sitaki kuamini na wewe capacity yako ndiyo iko hivyo. Unanshangaza!
Sasa wewe unaniuliza mimi Mbatu nitashidwaje kujua maana ya BANTU ikiwa neno lenyewe ni la Kibantu, umekunywa nini leo au bado una search ktk site kujua maana yake?. Bantu, Abantu ni WATU nalitumia sana katika lugha yangu.. Wewe uliye mwarabu kwa kiarabu maana yake nini?Kwanza ungeanza kwa kujibu swali langu ingekuwa raha sana.
Swali lako ni irrelevant kabisa tena, kwa kuwa hakuna sehemu niliyoandika kuwa Cushites ni weupe au weusi, sijagusa kabisa hilo.
Lakini ntakujibu hilo swali baada ya wewe kujibu swali langu unalolikwepa.
Jee unajuwa maana ya Bantu?