Kitabu kikitumiwa vyema na watunga sera wetu wa michezo tunaweza kuja kujenga Taifa Stars kwa ufanisi Sana.

Freewine

JF-Expert Member
Jan 7, 2018
257
212
1144054

Salaam bosses!!
Taifa la Tanzania linapitia wakati mgumu pale ambapo inaambulia kipigo kwa timu za kawaida Kama Lesotho, Kenya n.k
Wengi wa mashabaki wa mpira wanna mapenzi Sana na timu yao ya Taifa lakini wanaambulia kipigo. Mfano mzuri na kitendo Cha Taifa Stars kutolewa kwenye mashindano ya AFCON 2019 bila hata point moja kinauma Sana halafu Ni aibu kwa Taifa. High performance kwa timu ya Taifa katika mashindano haya yalikuwa Ni sehemu muhimu kwa Taifa letu la Tanzania kujitangaza kimataifa, ilikuwa Ni sehemu ya kuonesha talent za vijana wetu kisoka ili iwe fursa ya wao kuitajiwa na club kubwa nje na hivyo kukuza uchumi wetu Kama Taifa, lakini vyote hivyo vimekuwa Kama vimepepea na upepo hakuna Tena tumaini kwa Taifa inabidi kujipanga upya. Kitu ambacho kinaweza kuchukua Tena hata zaidi ya miaka 30 kushiriki Tena hayo mashindano.

Tanzania Kuna vipaji vikubwa Sana vya wachezaji lakini Jambo la kujiuliza kwa wote Kama Taifa tunakwama wapi??
Maendeleo ya Jambo lolote ktk Taifa yanaitaji mipango makini iliyowazi na inayoeleweka kwa Kila mwananchi ili kuweza kupata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi wote ambao ndio watekelezaji wakuu.
Kabla cjaendelea elewa faida hizi zitokanazo na uwekezaji sahihi kwenye sector ya michezo katika Taifa.
1. Michezo Ni njia kuu ya kuongeza utalii katika Taifa. hivyo unapokuwa na ligi nzuri, wachezaji wazuri wanaojituma uwanjani tegemea kuongeza idadi kubwa ya watu kuja kutalii pindi wanapokuja kuona michezo.
2. Faida kubwa ya michezo Ni uchumi wa nchi huweza kukua kwa haraka katika nchi iliyowekeza kwa usahihi katika michezo hasa soka.
Lakini swali Ni kwamba katika nchi hizi za kimaskini kama Tanzania zinaweza kumudu uwekezaji sahihi wenye tija katika sector ya michezo?

Hilo Ni swali gumu ambapo viongozi wa dunia ya tatu hufanya kitu kinaitwa zima Moto ili ionekane inasapoti michezo kumbe inaua michezo kwa kitendo Cha kupeleka budget pungufu katika sector ya michezo.
Vijana wenye talent wamekataa kuendelea na masuala ya michezo kutokana kwamba wanaona Kama Ni kupoteza muda wao bure kushugulika na kitu ambacho hakiko systematic.
Tumepata hubiri nyingi namna nchi zilizoendelea zilivyoweza kukuza sector ya michezo kwa kutumia uratibu wa uwepo wa Sport academy Kila mahali katika mitaa yao.
Lakini je linapokuja suala Hilo kwa nchi za dunia ya tatu, viongozi wake wataweza kumudu kuwezesha ujenzi wa hizo academy Kila mtaa?
Suruhisho la pekee na jepesi kwa nchi hizi za dunia ya tatu ni kutumia shule za serikali(public schools) zinazopatikana karibu Kila mtaa zitambulike pia Kama sports academy lengo likiwa kuweka mfumo rahisi unamuweza mwanafunzi kufikia mafanikio makubwa ya mpira bila kuathiri maendeleo yake ya darasani.
Vijana wengi wenye vipaji wamejikuta wakiua vipaji vyao vya mpira kwa kuofia kufeli mitihani ya kuhitimu kidato.

Mfano mzuri Ni Mimi katika shule ya msingi na mwanzoni hapo sekondari nilikuwa mchezaji mzuri Sana wa mpira na nilikuwa najiona mbali kwa uwezo wangu ule wa kuzunguka dimba lakini inaniuma pale ndoto yangu hiyo ilivyofariki pale nilipoanza kukaza mziki wa masomo ya sayansi katika shule ya kata ambayo ndo ilikuwa ikianza(nadhani changamoto zake msomaji unaweza ukazi imagine Kama hukuwai kuzipitia, No walimu)
Kwa hiyo kufa kwa ndoto yangu ile huwa inaniuma Sana nawaza pengine Sasa na Mimi ningekuwa kwenye headline za kutakiwa na timu Kama Asernal, city au barca. Lakini kwa hofu ya kufeli mitihani nikaamua Ni concentrate na masomo ili baada ya chuo niweze kiajiriwa kitu ambacho kimekuwa vise versa No ajira mpaka sasa. Sasa makosa haya na kujilauumu huku sipendi kuwakute watanzania wenzangu na hata waafrika wenzangu ndo maana nikatunga hiki kitabu kinachopatika Amazon kwa kaza Kama linavyoonekana hapo juu ili viongozi wetu na watunga sera wetu na wadau wa michezo tukipitie tuone namna gani tunaweza kuwa na muendelezo mzuri wa michezo katika nchi yetu kutoka utoto Hadi ujana.
Tukiamua kwa pamoja tunaweza kufanya mashindano ya AFCON na mashindano mengine ya michezo Ni nyumbani kwetu. Lakini tukiamua pia Kila kitu nchini kwetu kinatokea kwa mihemko ya kisiasa tujiandae kisaikolojia sisi Ni looser Kila wakati.
Asante vingi vimeongelewa kwenye kitabu naomba ukitafute ikikupendeza katka Amazon. Maendeleo hayana chama na waleta mabadiliko katika nchi Ni sisi hao hao wananchi.
 
Back
Top Bottom