mose
JF-Expert Member
- Jun 5, 2009
- 284
- 232
Pendo Lililobarikiwa,
Amani.
Jamiiforums sasa imekuwa ni Jukwaa la Kijamii la watu kutoka rika na makundi mbalimbali; wenye shauku ya kupenda na kutaka kujua mambo anuai-- yenye kuipa sifa ya sura ya jamii yetu, namna hii ilivyo na kwa lugha yetu hii ya Kiswahili.
Majadiliano, mashauri, udadisi, visomo, uchunguzi na utafiti ni vitendo bora vya bidii ya kiakili na nidhamu, vyenye kutuhakikishia wanajamii mwangaza zaidi na ladha bora ya ustaarabu wetu na basi mustakhabari wa kheri kwetu.
Maendeleo ni zao la chachu ya akili na haja ya kule kuzidi kuwa katika hali bora; lakini chenye kunasibu ukaribu wa wanajamii, jitahada za kijamii na matokeo yake ni nia ya kuliishi lile kusudi tulidhanialo kutawala jaala zetu sisi kama viumbe hai, vyenye utashi wa kiakili na katika mazingira yetu; tena katika majira na nyakati.
Sisi watu ni wenye kutafuta maana juu ya maisha yetu, matendo yetu na utumishi wetu; miongoni mwetu ili iwe kwamba uadilifu wetu upate kulandana na misingi ya haki, maadili mema na wajibu kutokana na kile tulicho na imani nacho--chenye kukutia tumaini, kusudi na mwongozo. Iwe kwa hakika, ama kusadiki; mwangaza binafsi, ama maelekezo ya kiushawishi wa taasisi ndani ya jamii yetu--iwe ni bidii na kuridhishana matakwa ya kijamii ama kutofuata mkumbo...
Jamii bora ni ile inayojinasibu na mwangaza bora katika dimensha zote za mapana ya jamii. Sayansi, Sanaa na Kujitambua vyatosha kuiimarisha nguvu ya kusimama kwa jamii; kufanya pembe tatu sawa kwa fikra ama wazo linaloweza kuakisi kusudi, nia na dhamira vyenye kushahibiana na matatu: uwezo, mazingira na mtu; Kwa kuwa, kupitia sayansi twajifunza kweli za asili; na pia kwa kujiongeza kimaarifa twaja kuwa na uwezo wa kuyamudu mazingira yetu na pia kwa kuielewa vema asili, sisi wenyewe twajielewa; na kisha sisi wenyewe tunatafuta muafaka wa kupendeza wa muonekano wa ustawi yetu, mambo yetu na ustaarabu binafsi wa kila mmoja wetu.
Ni kwa kutambua haya, na hasa kuzingatia kiu ya kujitambua; ya mwangaza, udadisi na uchunguzi; pia kutanua mapana ya visomo na sanaa; miye mwandishi wa haya nimechagua kutoa mchango wa kazi ya kufasiri -- kufasiri kazi ya kuandishi yenye maudhi nionayo ni bora na yenye msaada katika kuweka misingi ya maarifa zaidi, ujuzi na kufanya uweza bora katika mtu. Mtu aliye ni mwanajamii mwenzangu katika hata ukaribu huu wa lugha.
Kazi hii ni bora kabisa, kwa kuwa itamjengea yeyote aipitiaye uwezo kwa kupima na kulinganisha mawaidha na mashauri mengi juu ya mtu, dunia, viumbe, wakati na sura ya vile vinavyopitiliza wakati na maumbo. Pia kina maudhui ya utu bora, amani, mapenzi mema na undugu wa watu wote.
Kazi hii ni mwanzo tu, hakika mengi yatawezekana kufuatia na watu wengi wataona njia za msaada kuelekea kwenye moyo wa uelewa na unyenyekevu katika kujifunza na kutafakari. Pia kazi hii inaweza kuvuruga wengi kwa kuwa inawasilishwa kwa namna na picha tofauti na ile waliyozoea. Lakini walio na dhamira safi ya kupenda kujua mazuri yake watapata baraka zake, roho katika wao itawaongoza katika kumulika na mengine zaidi yafikayo katika macho na masikio yao.
Silazimiki sana kuzungumza kilichomo ndani ya kazi hii ya fasiri; itoshe kurejea tundiko mbili ambazo miye kama mtu nilipata kuleta humu kama mawaidha juu ya kazi hii kama nilivyoifasiri kutoka kwenye tovuti mama ya kazi nzima ya hichi kitabu:
Kuhusu kazi hii kuwa tofauti na 'injili' zingine:
Kuhusu Yesu katika hichi kitabu kusimulika kufundisha 'zaidi' juu ya uhusiano wa mtu na tunachokitaja Mungu':
***
Ninapenda kuweka tafsiri mchanganyiko--lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili
NINAOMBA VIRANJA WA KUKAGUA MAUDHUI (MODERATORS), MSIUHAMISHE KUNGINE UZI HUU; MIMI MFASIRI NIPO KUUTUMIKIA HUU KIMJADALA, MAZUNGUMZO NA UFAFANUZI UKIWA JUKWAA HILI HILI NILILOLICHAGUA HADI ZOEZI LITAKAPOMALIZIKA.
_________________________________
About the Author Levi H. Dowling
Kuhusu Mwandishi Levi H. Dowling
In response to inquiries from many friends of The Aquarian Gospel of Jesus the Christ for some information regarding the transcriber, we herewith give a short sketch. It was his great desire that each one should have the message regardless of the messenger.
Katika kuitikia maombi kutoka kwa marafiki wengi wa Injili ya Zama za Ndoo ya Yesu Kristu kwa habari za kuhusiana na mnakilishi, kwa nafasi hii hapa tunatoa picha fupi ya haraka haraka. Ilikuwa ni haja yake kubwa kwamba kila mtu ajelikupata ujumbe pasipo kujali ya mjumbe.
LEVI (Levi H. Dowling), was born Friday morning, May 18, 1844, at Belleville, Ohio. His father, Scotch-Welsh descent, was a pioneer preacher among the Disciples of Christ. Levi was always a student of the deeper things of life. At the age of thirteen, in his first public debate, he took the negative side against a Presbyterian Elder on "The Everlasting Punishment of the Wicked".
LEVI (Levi H. Dowling), alizaliwa Ijumaa asubuhi, Mei 18, 1844, Belleville, Ohio. Baba yake, mzao kutokea watu wa asili ya mchanganyiko wa kiskochi na Kiwelshi, alikuwa Mhubiri wa kwanza-kwanza miongoni kwa Wafuasi wa Kristu. Levi daima alikuwa mwanafunzi wa vitu vya kina zaidi vya maisha. Akiwa na umri wa miaka kumi na mitatu, mdahalo wake wa kwanza wa hadharani, alichukua upande wa kushoto dhidi ya Wazee wa Ki-Presbiteri juu ya "Adhabu ya kudumu milele ya Waovu".
He began preaching at the age of sixteen; and at the age of eighteen was pastor of a small church. He entered the United States Army at the age of twenty as Chaplain, and served in this capacity to the end of the Civil War. In 1866-7 he was a student at Northwestern Christian University at Indianapolis, Indiana. The next year he began publishing Sunday School Literature, issuing Sunday School Lesson Papers, Song Books, and a Children's Sunday School Paper. Much of his time was devoted to the cause of Prohibition. He was a graduate of two medical colleges and practised medicine for a number of years. He finally retired from the medical profession to resume literary work.
Alianza kuhubiri akiwa na umri wa miaka kumi na sita; katika umri wa miaka kumi na minane alikuwa mchungaji wa kanisa dogo. Aliingia Jeshi la Marekani akiwa na umri wa miaka ishirini kama mpeleka visomo vya mafundisho ya dini jeshini, na alitumikia nafasi hii mpaka mwisho wa vita vya ndani. Mnamo mwaka 1866-7 alikuwa mwanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Kikristu cha Kaskazini-Magharibi Indianapolis, Indiana. Mwaka unaofuatia alianza kutoa maandishi ya kupitiwa ya Shule ya Jumapili, akitoa machapisho ya masomo ya Shule ya Jumapili, Vitabu vya nyimbo, na machapisho ya Watoto kwa Shule ya Jumapili. Mwingi wa muda wake ulijikita katika kutia nguvu katazo la uuzwaji wa pombe, miaka hiyo Marekani. Alikuwa Mhitimu wa vyuo viwili vya tiba na alifanya kazi ya tiba na madawa kwa miaka kadhaa. Hatimaye alistaafu kutoka kwenye uweledi wa kitiba ili kuendeleza tena kazi za maandishi.
Early in life, when but a mere lad, he had a vision in which he was told that he was to "build a white city." This vision was repeated three times with years intervening. The building of the "white city" was "The Aquarian Gospel of Jesus the Christ." This book was transcribed between the early morning hours of two and six--the absolutely "quiet hours."
Mapema maishani, alipokuwa kijana mdogo mdogo tu, alipatwa na Uono ambayo aliambiwa ya kwamba yeye alikuwa ni "wakulijenga jiji jeupe." Uono huu alirudia mara tatu kwa kupishana miaka kadhaa katikati yake. Ujengaji wa "Mji Mweupe" ulikuwa ni "Injili ya Zama za Ndoo ya Yesu Kristu." Kitabu hichi kilinakilishwa katikati ya masaa ya alfajiri sana ya saa nane na saa kumi na mbili--"masaa ya ukimya" kabisa kabisa.
Levi passed from earth-life August 13, 1911.
Levi alifariki maishi ya dunia Agosti 13, 1911.
The Publishers
Wasambazaji machapisho

The Aquarian Age Gospel of Jesus, the Christ of the Piscean Age
DIBAJI
Azma ya miye mfasiri, ni kutanua maarifa na hekima juu ya yote na tena basi kuhusiana na yote; maarifa ya jamii, sayansi na filosofia hai katika mtu.The Aquarian Age Gospel of Jesus, the Christ of the Piscean Age
DIBAJI
Silazimiki sana kuzungumza kilichomo ndani ya kazi hii ya fasiri; itoshe kurejea tundiko mbili ambazo miye kama mtu nilipata kuleta humu kama mawaidha juu ya kazi hii kama nilivyoifasiri kutoka kwenye tovuti mama ya kazi nzima ya hichi kitabu:
Kuhusu kazi hii kuwa tofauti na 'injili' zingine:
Kuhusu Yesu katika hichi kitabu kusimulika kufundisha 'zaidi' juu ya uhusiano wa mtu na tunachokitaja Mungu':
***
Ninapenda kuweka tafsiri mchanganyiko--lugha ya Kiingereza na Kiswahili ili
- iwe kama msaada wa masahihisho madogo madogo kadri itakavyojitokeza
- kusaidia wale wanaopenda kuboresha umahiri na uzoefu wao wa kumudu lugha zote mbili wayaone ya kujifunza
- kudhihirisha kwa watu wote kuwa dhana ya 'uchanga' wa lugha ya Kiswahili ni maneno ya wanaokosa mbinu na uwezo; na wale waghairishaji.
- Kusaidia wanalugha kufuatilia ufundi na ujuzi wa kutasiri; kuwa huu ni mchanganyiko wa yote mawili-- tafsiri na sanaa; kwa maana yapasa kwanza kusoma na kuelewa, kuweka picha kichwani na kisha kuisimulia tena upya kwa lugha tofauti huku ukikadirisha kwa kiasi cha juu kuwezekana, tafsiri ya neno kwa neno.