Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Kitabu hiking kinasimulia jinsi Wanajeshi wa Marekani walivyoingia kwenye mtego wa Wachina wakati wa vita ya Korea 1950-1953.
Juni Mwaka 1950 NK iliivamia SK na kuteka kwa Kasi karibu nchi yote. Majeshi ya US yakaingia kuikomboa. Wakayarudisha majeshi ya NK hadi kwao. Yakawa yamepangwa kupigana vita hadi kwenye mpaka wa NK na China.
Vita ilikuwa ngumu sababu NK ni nchi ya vilima na majira ya baridi yalianza. Barbara zinapita kwenye mabonde membamba yakiwa na milima huku na huku. Ili kusonga inabidi mumpige adui kwenye vilima. pole pole majeshi ya Marekani yakawa yanawarudisha nyuma wa NK+Wachina. Wasijue kiumbe Wachina nao wanarudi nyumba lakini wamewaandalia mtego.
Majeshi ya US yalipoingia sana NK, China ikatuma Malaki ya Wanajeshi, na kisha ikafunga zile Barbara nyembamba za kurudia. Na sehemu nyingine wakilipua madaraja.
Majeshi ya US yakaanza kurudia nyuma. Huku watu wakifa na kulemaa kwa baridi Kali, na hapo wakipigwa vikali na Wachina. Bila msaada wa ndege majeshi yote ya US yangeweza kuangmizwa. Mainjinia walipiga kazi ya kujenga viwanja vya ndege na kujenga madaraja huku adui wakirusha risasi toka kila upande. Wagonjwa walioweza kutembea walipewa bunduki kulinda msafara. Wasioweza walijilaza kwenye magari na kupewa bunduki. Waliokuwa fiti walipanda vilima upande huu na ule wa barabara kumtoa adui.
Majeshi ya US na SK yalirudishwa nyuma hadi Seoul ikatekwa tena. Wengi wakifa kwa baridi na risasi. Baadaye walioweza kuwarudisha tena Wachina na wa NK kwao.
Inadaiwa wa US wakipigwa vibaya sababu kamanda mkuu aliongoza vita akiwa Japan bila kujua hali halisi ya Korea. Akiwamrisha tu makamanda wake wasonge hadi mpaka wa China.
Vita ya kwenye baridi na milimani ni mbaya sana.