Kitabu cha Trump

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,586
1,678
FIRE AND FURY (moto na ghadhabu) ni kitabu kipya juu ya rais wa Marekani Donald Trump; uwezo wake wa uongozi na maamuzi yake kwa jumla. Kitabu hiki kwa ujumla wake kinamkashifu vikali bw. Trump, kashafa zake nyingi: namna alivyoshirikiana na Warusi kuja madarakani na hata uwezo wake wa kiakili, "ana akili za kitoto".
Mwandishi wa kitabu hiki, bw. Michael Wolff bado anaishi Marekani na wala hakulazimika kuikimbia nchi yake, pamoja na kumkosoa vikali rais wake. Kwa uwelewa wa wenzetu hao wa kiongozi wao ni kuwa yeye ni mtu kama watu wengine.
Nisingependa sana kuifananisha nchi yangu Tanzania na Marekani. Isipokuwa jambo linalotia uchungu ni kuona kwamba wakati fulani tulikuwa tumepiga hatua kubwa sana kukaribia kufikia kiwango hicho cha ufahamu, ila katika miaka ya karibuni tumerudi nyuma (kana kwamba tulisahau kitu huko). Hivi sasa yaonekana kana kwamba kufikia hatua hiyo ya Marekani ni kitu kisichowezekana kabisa. Hili ni jambo la kuumiza moyo.
Na ndiyo maana nakumbuka masihara (mzaha, mahoka ) ya rafiki yangu eti:
Marais watatu wa Afrika Mashariki waliamua kwenda kumwuliza Bw. Yesu ( amani iwe juu yake) juu ya majaaliwa ya nchi zao.
Kenyatta: "Bw. Yesu, nimekuja uniambie nchi yangu yahitaji miaka mingapi iwe kama nchi za EU- Umoja wa Ulaya?"
Yesu: "Kwa hilo Kenyatta, Kenya mtahitajia miaka 200"!
Kenyatta arudi kwa wenziwe, Kagame na Magufuli akilia. Wanamuuliza, kulikoni? Awajibu, bw Yesu amenipa miaka mingi sana. Si mimi wala kizazi changu kitashuhudia ustawi huo. Ndiyo maana nalia!
Zamu ikaja kwa Kagame. Bila ya kuchukua muda mrefu bw. Yesu akamjibu: "ama kwa Rwanda, mtahitajia miaka 400"!
Halkadhalika Kagame akarudi analia: miaka mingi, hataishuhudia, si yeye wala kizazi chake.

Ikaja zamu ya rais wetu mpendwa. " Bwana Yesu, na jee Tanzania? Lini tutakuwa na ustawi wa kutajika, uadilifu na maisha bora kwa kila Mtanzania, mithili ya wenzetu wa EU ?"
Bwana Yesu akaonekana kustushwa na swali hilo, akasita na kunyamaa. Alipoibuka kumtazama rais wetu.....yeye ndiye akawa analia!

Nimesema huu ni mzaha wa rafiki yangu msiemjua, mkimtaka mtumieni "wasiojulikana"!
 
Hivi hii kitu inawezekana au ni movie?
 
Attachments

  • VID-20180106-WA0010.mp4
    7.9 MB · Views: 20
Jana namaliza "Behave: The Biology of Humans at Our Worst and Best" cha Dr. Sapolsky, naanza "Iran: A Modern History" cha Abbas Amanat, nikapewa hiki.

Nakisoma tangu jana, Iran itabidi kisubiri kidogo.
Good for your brain brother,
Good for you. .......
 
FIRE AND FURY (moto na ghadhabu) ni kitabu kipya juu ya rais wa Marekani Donald Trump; uwezo wake wa uongozi na maamuzi yake kwa jumla. Kitabu hiki kwa ujumla wake kinamkashifu vikali bw. Trump, kashafa zake nyingi: namna alivyoshirikiana na Warusi kuja madarakani na hata uwezo wake wa kiakili, "ana akili za kitoto".
Mwandishi wa kitabu hiki, bw. Michael Wolff bado anaishi Marekani na wala hakulazimika kuikimbia nchi yake, pamoja na kumkosoa vikali rais wake. Kwa uwelewa wa wenzetu hao wa kiongozi wao ni kuwa yeye ni mtu kama watu wengine.
Nisingependa sana kuifananisha nchi yangu Tanzania na Marekani. Isipokuwa jambo linalotia uchungu ni kuona kwamba wakati fulani tulikuwa tumepiga hatua kubwa sana kukaribia kufikia kiwango hicho cha ufahamu, ila katika miaka ya karibuni tumerudi nyuma (kana kwamba tulisahau kitu huko). Hivi sasa yaonekana kana kwamba kufikia hatua hiyo ya Marekani ni kitu kisichowezekana kabisa. Hili ni jambo la kuumiza moyo.
Na ndiyo maana nakumbuka masihara (mzaha, mahoka ) ya rafiki yangu eti:
Marais watatu wa Afrika Mashariki waliamua kwenda kumwuliza Bw. Yesu ( amani iwe juu yake) juu ya majaaliwa ya nchi zao.
Kenyatta: "Bw. Yesu, nimekuja uniambie nchi yangu yahitaji miaka mingapi iwe kama nchi za EU- Umoja wa Ulaya?"
Yesu: "Kwa hilo Kenyatta, Kenya mtahitajia miaka 200"!
Kenyatta arudi kwa wenziwe, Kagame na Magufuli akilia. Wanamuuliza, kulikoni? Awajibu, bw Yesu amenipa miaka mingi sana. Si mimi wala kizazi changu kitashuhudia ustawi huo. Ndiyo maana nalia!
Zamu ikaja kwa Kagame. Bila ya kuchukua muda mrefu bw. Yesu akamjibu: "ama kwa Rwanda, mtahitajia miaka 400"!
Halkadhalika Kagame akarudi analia: miaka mingi, hataishuhudia, si yeye wala kizazi chake.

Ikaja zamu ya rais wetu mpendwa. " Bwana Yesu, na jee Tanzania? Lini tutakuwa na ustawi wa kutajika, uadilifu na maisha bora kwa kila Mtanzania, mithili ya wenzetu wa EU ?"
Bwana Yesu akaonekana kustushwa na swali hilo, akasita na kunyamaa. Alipoibuka kumtazama rais wetu.....yeye ndiye akawa analia!

Nimesema huu ni mzaha wa rafiki yangu msiemjua, mkimtaka mtumieni "wasiojulikana"!
Wewe jamaa. BWANA YESU akalia?
 
mbona alishatumiwa wasiojulukana
 
Back
Top Bottom