Kitabu cha Quran ni rahisi kukikariri

Kitabu cha Quran ni rahisi kukikariri

hamis77

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
18,250
Reaction score
26,640
KWANINI NI RAHISI KUIKARIRI QURAN?

Watu wengi wanaweza kuhifadhi nyimbo za Bongo Fleva, hadithi au mashairi ya Kiarabu, lakini hiyo haimaanishi kuwa ni Neno la Mungu. Kuweza kukariri kitu hakuthibitishi kuwa ni cha kiungu.

Vivyo hivyo, hoja kwamba Qur’an ni rahisi kukaririka haithibitishi uungu wake.

Qur’an iliandikwa kwa mtindo wa mashairi ya Kiarabu (balagha), ambao ni mtindo wa kifasihi uliokuwa maarufu sana miongoni mwa Waarabu kabla ya Uislamu.

Waarabu walikuwa jamii ya kihistoria iliyotegemea ushairi na masimulizi ya mdomo. Hivyo, walikuwa hodari wa kukariri mashairi na nyimbo.

Muhammad mwenyewe alizaliwa katika mazingira hayo na Qur’an inafuata mtindo huo wa kishairi, jambo ambalo linasaidia kuwa rahisi kuhifadhi.

Kwa hiyo, urahisi wa kuihifadhi Qur’an hauoneshi uungu wake, bali ni matokeo ya kutumia mbinu za kifasihi zinazojulikana na kukubalika sana katika jamii hiyo ya Kiarabu ya wakati huo.

Pia QURANI ni kitabu kidogo sana , Ukitazama ukubwa wa Qur’an ukilinganisha na Biblia, Qur’an ni ndogo sana. Kwa mfano

Qur’an ina jumla ya Aya 6,236 (isipokuwa baadhi wanataja 6,349 kulingana na mpangilio), na ina jumla ya takriban 77,430 za maneno.

Agano Jipya peke yake lina Aya 7,957, na lina jumla ya takriban 181,253 za maneno — tayari ni kubwa zaidi ya Qur’an nzima.

Biblia nzima (Agano la Kale na Jipya) ina jumla ya Aya 31,102 na maneno 783,137.

Hii inaonesha kuwa Qur’an ni fupi mno, haina wigo mpana wa maelezo ya historia ya mwanadamu, hatima, wokovu, tabia ya Mungu na kazi yake kwa binadamu kama ilivyoelezwa kwenye Biblia.

Hakuna mpangilio wa matukio kama vile kuumbwa kwa dunia, agano la Mungu na watu wake, maisha ya manabii mbalimbali kwa muktadha wa kihistoria, ujio wa Masihi, mateso yake, kifo na kufufuka kwake kwa ajili ya wokovu wa wanadamu.,Ni ngumu hata kuitumia Quran kufanyia shughuli za Archeology maana Haina mpangilio hata wa Chronology.

Tofauti na Injili ambayo inaleta ujumbe wa Mungu wa upendo kwa ulimwengu mzima kwa njia ya Yesu Kristo, Qur’an haielezi kwa kina juu ya dhambi, toba, neema, na wokovu wa milele kwa msingi wa upendo wa Mungu unaojitolea.

Qur’an inajikita zaidi katika sheria, hukumu, na matendo ya nje, badala ya kuzama kwenye mabadiliko ya moyo na kiroho.

Kulingana na wanazuoni wa Kiislamu kama al-Tabari na Ibn Ishaq, Muhammad aliwahi kutamka aya akiwatukuza masanamu wa Quraysh , Lat, Uzza na Manat akisema

“Hawa ni malaika wa Allah, na uombezi wao unakubalika.”

Baadaye alikana maneno hayo na kusema kuwa Shetani alimghilibu na kumuingizia maneno hayo.

Tukio hilo linajulikana kama “Satanic Verses” (Aya za Shetani).Na wengi wanaojaribu kuliweka wazi Huwa wanasomewa Fatwa ya kifo mfano Salman Rushdie,n.k maana haitakiwi kuwekwa wazi.

Swali linakuja kwa Sisi wachambuzi ,wachunguzi na wasomaji wa hizi dini mbalimbali ,

Kama kweli Qur’an ni ya Mungu na Muhammad ni nabii wa kweli, je, inawezekanaje Shetani aingize aya kwenye ufunuo wa Mungu bila kugundulika mapema?

Kama Shetani aliweza kumzidi maarifa Nabii huyo, basi usahihi wa Quran unaingia mashakani.

Hakuna tukio kama hilo linalosimuliwa katika maisha ya Yesu au Musa, ambao walionyesha uwezo wa kupambanua sauti ya Mungu na ile ya adui bila kuchanganya.

Katika maeneo mengi ya Afrika na hata Uarabuni, Qur’an hutumika na baadhi ya waganga wa kienyeji katika kuagua majini, kutoa ndumba au kufukuza mapepo. ,Nadhani mshakutana sana na Nazi zenye maneno ya kiarabu ,n.k

Kuna Aya maalum zinazoitwa "Aya za Kinga" au "Aya za Ruqyah" ambazo hutumika kwa shughuli hizo. (NITALETA MADA HII PANAPO MAJAALIWA)

Hii ni tofauti kabisa na Biblia, ambayo inaonesha wazi kuwa Neno la Mungu haliwezi kuchanganywa na uchawi au waganga. Katika Biblia, watu walipokuwa wanamwamini Yesu, walichoma vitabu vyao vya uchawi hadharani (Mdo. 19:19).

Kwa hiyo, hoja kwamba Qur’an ni rahisi kukaririka haiwezi kuwa msingi wa kudai uungu wake.

Kitabu hicho ni kidogo, kina vipengele vilivyopokewa kutoka kwenye mila za Kiarabu, na hata kinasimuliwa kuwa kilishawahi kuingiliwa na Shetani.

Kinyume chake, Biblia ni pana, kina, ina historia ya wokovu kutoka Mwanzo hadi Ufunuo, na mafundisho yake yamebeba ujumbe wa neema na upendo wa Mungu kupitia kwa Yesu Kristo.

Wokovu wa kweli hauji kwa kukariri, bali kwa kumjua na kumpokea Mwana wa Mungu
Yesu Kristo aliye Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6).
 
Umeeleza kinadharia ila uhalisia hali haipo hivyo maana ingekuwa kila muislamu kuhifadhi Qur'an lingekuwa jambo la kawaida.
 
Back
Top Bottom