Kitabu cha BONDIA..

Kitabu cha BONDIA..

Msiri

Senior Member
Joined
Jan 10, 2010
Posts
124
Reaction score
100
TUWA.jpg
Je wewe ni mpenzi wa Riwaya za Taharuki, hususan kutoka kwa mkali wa riwaya hizo nchini, HUSSEIN TUWA? Kama jibu ni ndiyo, basi sasa ndio wakati wako wa kufunga na kufungua mwaka kwa riwaya kali ya BONDIA, ikiwa imesheheni taharuki yenye mshindo, kutoka kwa mwandishi huyu nguli wa riwaya za taharuki…HUSSEIN TUWA!

Hivi mtu anawezaje kufanya mauaji ya dhahiri mbele ya umati wa watu, na bado akaonekana hana hatia? Basi ndilo ambalo ROMAN KOGGA ndani ya riwaya hii alilokusudia kulifanya. Lakini unadhani alifanikiwa ilhali Inspekta FATMA, mwanadada makini na machachari (Utata wa 9/12) akiwa nyuma ya kila hatua ya nyenendo zake? MAJIBU YAMO NDANI YA KITABU HIKI MARIDHAWA, kwa mchango wa sh. 12,000/- tu! Hebu pata kionjo hapa chini:

Wewe ni bondia wa kulipwa. Mimi ni mpelelezi wa kulipwa. Sote ni mahiri kwenye fani zetu. Kwenye ulingo wako wa ndondi kuna mbinu kadhaa ambazo sina shaka unazijua sana…” MG alimwambia na kutulia kidogo, kisha akaendelea,

…basi na nje ya huo ulingo uliouzoea kuna mbinu tofauti na wachezaji tofauti ndugu yangu. Mimi ni mahiri kwenye mbinu za fani yangu, ambazo zinatumika nje ya ulingo wako. Na moja ya mbinu hizo ni kuchagua vita ambayo sio tu utashinda bali pia yenye tija zaidi na wewe.” Roman alibaki akimtazama kwa uso ulionuna huku Mark na Dan wakifuatilia hali ile kwa udadisi.

“Kuwalipizia kisasi wale watekaji sio vita yako ya msingi hivi sasa Roman, na hakuna tija na lililo mbele yako. Vita yako kuu iko ulingoni keshokutwa, kati yako na Deus...”

-- Bondia, Ukurasa 193.
Kitabu kinauzwa Sh. 12,000. Kinapatikana dukani KONA YA RIWAYA Kinondoni Block 41 nyuma ya jengo la Airtel 0655-428085. Kwa mikoani kinaweza kutumwa hadi huko kwa kuongeza shs 5,000 kwa usafirishaji.
 
Kitakuwa kizuri sana ngoja nikitafute
 
Hussein Tuwa sitakusahau daima kwa uhondo nilioupata kutoka katika kitabu cha MKIMBIZI na kitabu cha MTUHUMIWA.

Nimepata kusoma vitabu vingi kiasi lakini hivyo nilivyovitaja ni best of the best,,, na nilivisoma takribani miaka 10 iliyopita vikapotea, nimejaribu kuvitafuta madukani lakn nimeambulia patupu!!!

Hongera sana Hussein Tuwa kwa hadithi zako mujarrrabu...!!!

Sent from my HTC Desire EYE using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom