Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 10,884
- 18,824
Maarufu kama The March of the 10,000.
Mwaka 401 kabla ya Yesu Kuzaliwa, Uajemi(Iran) ilikuwa ndiyo Dola kubwa zaidi duniani. Ikitawala kuanzia mto Indus Mashariki hadi bahari ya Mediteranea, Misri, na Uturuki yote. Mtawala wake alikuwa Xerxes, na alikuwa na mdogo anayeitwa Cyrus aliyetaka kumpindua. Cyrus alipewa eneo fulani Uturuki kutawala. Alikusanya jeshi kubwa la kama waajemi 100K na mamluki 10,000 wa Kigiriki Ili kwenda kumpindua kaka yake huko Babiloni(Karibu na Baghdad).
Jeshi likamarch kupitia Syria, likavuka mto Euphrates na kukaribia Babiloni. Hapo vita ikapiganwa na Cyrus akauawa. Jeshi la Cyrus lilikiwa kama 120K, na la kaka yake 1.2m. Katika vita hiyo wagiriki walishinda kwenye eneo walilowekwa kupigana, ila hawakujua kuwa Cyrus kauawa hadi asubuhi ilipofika. Hapo wakajikuta wapo ndani kabisa kwenye nchi ya adui na mfadhili wao kauawa.
Xerxes akawajia na kuwaambia waweke silaha chini na kuwa rafiki zake. Wakagoma. Wakasema wanachotaka ni kurudi kwao, kutoka Babiloni hadi Ugiriki. Lakini hawawezi rudi njia waliojia sababu ni jangwa hakuna chakula. Mfalme akawapa jeshi liwaongoze. Akitafuta nafasi awamalize maana aliona itakuwa aibu akiwaacha warudi kwao.
Njiani jeshi lile lililokuwa linalowaongoza lilifanya hila na kuwaua wajenerali wao wote, makapteni na wanajeshi wengine kama 200. Hapo wagiriki wakaona wameisha kabisa. Wakalala kinyonge. Usiku mtu aliyeitwa Xenophon akawaamsha na kuwaambia hawatakiwi kukata tamaa na kufa kizembe. Wabebe silaha, wachague viongozi na waanze kumarch kuelekea home. Safari ikaanza. Wanaambaa ambaa na mto Tigris kwenda kaskazini. Huku nyuma adui kawafuata na jeshi kuwapiga mishale na mawe. Kila siku wakijifunza mbinu mpya ya kupambana na adui. Mara nyingi wakimpiga na kumkimbiza. Wakaanza kumarch jioni na usiku na kuweka kambi mchana ili kuepuka kumarch huku wakipigana.
Wakamarch hadi kukutana na milima ya Wakurd. Huko juu waliishi watu wakali walioitwa Wacarduchians. Baada ya majadiliano wakaona huko ndiko afadhali kupita. Kwa siku saba walipigana na wakarduchi, vita kali ya kupanda na kushuka vilima, wakiporomoshewa mawe na mishale. Kutoka huko milimani wakaingia Armenia. Wakakutana na theluji na baadhi yao wakafa. Mtindo ukawa ni vita vita hadi wakafika pwani ya bahari nyeusi, kaskazini , mashariki ya Uturuki. Kulikuwa na shangwe kubwa baada ya kuiona bahari. Baada ya kupumzika wakaanza safari ndefu ya kumarch kuelekea magharibi. Wakipigana vita kali ili kujipatia misosi.
Baada ya kutembea wakipigana kwa kama miaka 2 na kutembea kilomita 3,500 wakafika nyumbani. Kati ya Wagiriki 10,000, walifika 8,500. Uzuri zaidi wa kitabu hiki upo kwenye jinsi Xenophon alivyoongoza jeshi na hotuba zake.