Kiswanglish mpaka huku

mgendege

JF-Expert Member
Jul 18, 2020
299
350
Hivi kuchanganya kiswahili na kingeleza Tanzania tunafeli wapi huyu Alie Andika kwenye jengo hili vipi jengo la CCM Dodoma la Uchaguzi (UCHAGUZI HOUSE) neno UCHAGUZI halina Kiingereza au neno HOUSE halina Kiswahili?

Hapo neno HOUSE halina Kiswahili na neno UCHAGUZI halina Kingereza yake au mbona sielewi hapo, we umelewaje hapoView attachment 1529541

maxresdefault-2-660x400.jpg
 
Mkuu ulitaka waandike " uchaguzi nyumba" mbona Kama imekaa ki local sana!.. Bora "election house"

Hawa nawenyewe wanatuchanganya tu mi hapa English grammar yangu imeshapotea..😂
 
Aandikeje sasa NYUMBA YA UCHAGUZI.

Au ELECTION HOUSE.
Halafu sio jengo la Ccm hilo. Ninakushauri jifunze kuandika muandiko mzuri. Unakua kama hujasoma somo la muandiko aisee darasa la kwanza?
 
Hiyo ni sanaa ya uandishi, mfano uchumi house, biashara house, mafao haouse nk, haya majengo yote yapo miaka mingi
Sasa si ndio Ki Swanglish hicho, kuchanganya English na Kiswahili ndio Sanaa ya lugha? Lugha ipi ? English au Kiswahili?
 
Sanaa ya uandishi wewe unabadilisha unasema sanaa ya lugha?😂halafu kwani ni lazima upingane na mimi muda wote? Nilikukosea nini we jamaa?
 
Inasaundi poa sana.... Uchumi House, Watumishi House, Mawasiliano Tower!
 
Sanaa ya uandishi wewe unabadilisha unasema sanaa ya lugha?😂halafu kwani ni lazima upingane na mimi muda wote? Nilikukosea nini we jamaa?
nimepingana na wewe muda wote? mbona hata sikujui zaidi ya kuona comment yako na kujibu kama ninavyojibu comment nyingine?
 
Hapana, hapa hajachanganya lugha. Neno UCHAGUZI limetumika hapa kama NOMINO, sema tu kwa sababu lina maana nyingine tena kwenye lugha ya Kiswahili.

Yaani kilichofanyika hapa ni kama tuseme, angeweza hata akaliita jengo hilo MKAPA HOUSE Sasa jina MKAPA huwezi tena ukasema ni Kiswahili au ni Kiingereza.

Kwa mfano, tuseme kama ngeamua kuliita jengo hilo kwa jina la MAPUNDA HOUSE, ungemkosoa kuwa amechanganya lugha na alitakiwa aliite MADONKEY HOUSE?
 
Hivi kuchanganya kiswahili na kingeleza Tanzania tunafeli wapi huyu Alie Andika kwenye jengo hili vipi jengo la CCM Dodoma la Uchaguzi (UCHAGUZI HOUSE) neno UCHAGUZI halina Kiingereza au neno HOUSE halina Kiswahili?

Hapo neno HOUSE halina Kiswahili na neno UCHAGUZI halina Kingereza yake au mbona sielewi hapo, we umelewaje hapoView attachment 1529541

Kingeleza =Kiingereza.
Tunafeli =Je hili ni neno sahihi la kiswahili?
Alie Andika = Aliye andika.
Kingereza yake = Kiingereza chake.
We umelewaje = Wewe umeelewaje
 
Habari muheshimiwa!! Hapo hakuna kiswanglishi ni vile tu wewe hujaelewa, nami nakuelewesha kama ifuatavyo:-

Katika hilo jengo neno "UCHAGUZI" limetumika kama jina la jengo husika. mfano jina GRACE kwa kiswahili ni NEEMA, lakini katika uitaji wa majina mtu mwenye jina la GRACE huwezi kumuita NEEMA akakuitikia maana utakuwa umempotezea utambulisho wake na haki zake, vile vile kwa mtu mwenye jina la NEEMA.

Hivyo jina la Mtu au kitu huitwa kama lilivyo bila tafsiri.
 
Election kwa kiswahili Nini mkuu
 
iyo Kuanzia leo ni ELECTION HOUSE ova.brabra hatutaki sijui mkapa house au grace house unaweza ukabatizwa na neno UCHAGUZI Kama munesema ni jina majina hayawani hayo Kama vile upepo mwangwi sauti mungu shetani n.k
 
Naomba kujua umri wako kama hutojali!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom