Baraka Shamte anapopuliza baragumu lake

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,260
BARAKA SHAMTE ANAPOPULIZA BARAGUMU LAKE


Kwa mara ya kwanza kumuona Baraka Shamte ilikuwa mwaka wa 1995 siku ya pili baada ya Zanzibar kupiga kura Maalim Seif Shariff na Dr. Salmin Amour wakigombea nafasi ya urais.

Tulikuwa na kijiwe chetu pembeni nje ya mgahawa wa Passing Show.

Tuko pale kiasi cha mida ya saa tatu nne hivi.

Taarifa zilizokuwa zimezagaa ni kuwa Komando wa CCM Dr. Salmin Amour ameshindwa na Maalim Seif kashinda uchaguzi.

Kulikuwa na ukimya wa ajabu Zanzibar asubuhi ile.

Mashati ya kijani yalikuwa yanaonekana yakipita mitaani lakini vichwa chini na wengine wanaonekana wamesimama vikundi vikundi.

Hapo ndipo alipopita Baraka Shamte na shati lake la kijana kajiinamia anatazama chini yuko kimya.

Jamaa yangu mmoja Mzanzibari akaniambia, ‘’Salmin Amour ameshindwa uchaguzi kungekuwa na ushindi Baraka Shamte asingepita hapa kimya.’’

Naam siku ya tatu matokeo yakiwa bado hayajatangazwa tuko kiiweni, Baraka Shamte akapita kijiweni nasi tuko pale.

Baraka Shamte toka anakuja tunamuona kwa mbali kachangamka ananadi huku shingo katoa anatangaza kwa ulimu mzuri wa Kiingereza, ‘’We have won the election we are going to form the government.’’

Jamaa yangu akanigeukia akaniambia, ‘’Wamebadilisha matokeo.’’

Njia nzima Baraka Shamte anapita anapiga makelele na watu waliokuwa wamevaa mashati ya kijani wanamshangilia.

Haukupita muda ikatangazwa kuwa Komando Salmin Amour kashinda uchaguzi.

Mimi kazi yangu ikawa imekwisha.

Sikuwa na la kuniweka zaidi nikapanda Flying Horse ndiyo ilikuwa boti yetu enzi hizo nikarudi Dar es Salaam.

Chaguzi zote za Zanzibar zilizofuatia jumla sita mtindo ukawa huu.
Hili Baragumu la Baraka Shamte analopiga hajabadilisha nyimbo.

Nyimbo ni ile ile ingawa kwa hii ya leo naona ‘’notes’’ zake zimeongezeka ‘’melody,’’ nyimbo imekuwa tamu zaidi.

Mwalimu wangu somo, ''Introduction to Politics,'' Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Dr. Katabaro Miti alitufunza anasema mwanafunzi wa somo la siasa lazima ajifunze kutazama mazingira ya nyakati na kufanya utabiri wa nini kitatokea.

Nimepata mara nyingi kufuata mafunzo ya mwalimu wangu Dr. Katabaro Miti nikajaribu kutabiri uchaguzi wa Zanzibar.

Mara zote sifanikiwi katika matokeo yangu matokeo yanakuwa kama yale ya mwaka jana, mwaka juzi, mwaka kabla nk.

Nafanya, ''prediction,'' kisha nafanya, ''simulation.''

''Simulation'' na ''prediction,'' katika ''control,'' vinakubaliana lakini uchaguzi ukifanyika sheria zote za utafiti zinajipiga chini nashindwa kupata sababu kwa nini inakuwa hivi?

Nakwenda mbali zaidi na jibu ninalopata ni kuwa jambo lililo wazi halifanyiwi utabiri.

You cant predict the obvious.

Katika kipindi cha mapinduzi Azam TV Ijumaa iliyopita nimeulizwa kuhusu hali ya baadae ya Zanzibar baada ya miaka 60.

Baadhi ya watu wamenilaumu kwa kutojibu maswali kwa hali inayotegemewa kutoka kwangu kama kawaida yangu.

Katika swali hili ikawa ni ile ile ''merry go round,'' yangu niliyoanzanayo mwanzo wa mahojiano.

Baraka Shamte katoa jibu.

Muyaka bin Haji kuna kipande chake kimoja cha shairi kinasema: ''Mbona umeghafilika kwa jambo lisilo shaka?''

Mimi sijaghafilika.
In Shaa Allah tusubiri.
 
CCM ni Chama cha mashetani, alichokifanya kama Jecha ule NI utimilifu wa ushetani.

Ndio napatwa na shida ya mchakato wa kumfanya Nyerere mwenye heri ilihali yeye ndio founder wa hii dhulma dhidi ya sauti ya Wazanzibar.
 
Back
Top Bottom