Wakisema Kiswahili, "HICHI" ni cha watu gani,
HICHI ni neno dhalili, tumia "HIKI" nadhani,
Ila turudie swali, haswa ni cha watu gani,
Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.
Chazungumzwa Mrima, Mombasa hata Unguja,
Pwani yote kinavuma, kwa mbwembwe na kwa lahaja,
Na bara hata Musoma, kote wanakibwabwaja,
Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.
Kina mengi makusanyo, ya maneno mbalimbali,
Wa'rabu pia Wayao, Wandengereko Wandali,
Wote wametia yao, kwa lugha kuipa hali,
Nafikiri ni vigumu, kujua waanzilishi.
Kwa leo ninanyamaza, nitakuja tena kesho,
Nitazidi kuyawaza, wote tupate fundisho,
Ila usijenyamaza, kwa hii yangu mipasho,
Endelea kuuliza, mwanzilishi wake nani?
Miye mefikiri mno, kuamuwa jambo hili
Na huona lugha hino, lazima ina asili
Kwa sababu kulla neno, lina mwanzo wa usuli
Ndipo ha'mba Kiswahili, hi lugha ya watu gani?
11
Na iwapo hivi sivyo, niliyyoamuwa hili
Nionyeshani viliyyo, mubainishe ukweli
Nijuwe ambavyo ndivyo, tutowane mushkili
Kifunuke Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
12
Na iwapo atakuja, wa kunijibu suali
Namuomba jambo moja, twambiyane kiakili
Tusionyane miuja, jambo nisilo kubali
N'anambiye Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
.Daima unapotwanga, ni lazima kupepeta,
Kutenga chuya na chenga, ungo utaukamata,
Hapa ukishaboronga, mchele hataupata,
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
Ni lugha ya watu gani?, nambieni kiswahili.
Hata mimi wa omani,Kuongea ni halali.
Nasriyah wa yemeni, anatamba kila hali.
Kiarabu chetu sisi, kiswahili ni cha nani?
Kwa siri yake mtungi, aijuaye ni kata,
Na nyumba bila msingi, utapasuka ukuta,
Kila palipo na wengi, na mambo ya yatambata,
Kiarabu ni cha kwetu, kiswahili ni cha nani?
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Hamza wa Yusufali ,Al Naamani la pili
BARUBARU mashuhuri, makazi yangu Qatari
Kiarabu lugha yetu, kiswahili ni cha nani?
Dr Hamza Yusuf Al Naamany(Barubaru)
Itaendelea...
Wabara ni watu gani,
wavisiwani ni nani,
Kiswahili lugha yetu, Wabara na Visiwani
Inavuma hapa kwetu, hadi huko ghaibuni
Utamu wake Kibantu, maneno yake yakini
Imekopa vya Uarabu, navyo vya Jerumani
Itaendelea...
Daima unapotwanga, ni lazima kupepeta,
Kutenga chuya na chenga, ungo utaukamata,
Hapa ukishaboronga, mchele hataupata,
Nambiyani Kiswahili, ni lugha ya watu gani?
Ni lugha ya watu gani?, nambieni kiswahili.
Hata mimi wa omani,Kuongea ni halali.
Nasriyah wa yemeni, anatamba kila hali.
Kiarabu chetu sisi, kiswahili ni cha nani?
Kwa siri yake mtungi, aijuaye ni kata,
Na nyumba bila msingi, utapasuka ukuta,
Kila palipo na wengi, na mambo ya yatambata,
Kiarabu ni cha kwetu, kiswahili ni cha nani?
Tamati ndio akhiri, na jina langu ni hili
Hamza wa Yusufali ,Al Naamani la pili
BARUBARU mashuhuri, makazi yangu Qatari
Kiarabu lugha yetu, kiswahili ni cha nani?
Dr Hamza Yusuf Al Naamany(Barubaru)
Doha. Qatar
campanero ujajibu swali. Unaona mwenzako ameweka bayana anauliza Kiarabu ni cha waarabu, kihindi ni cha wahindi. sasa unaposema kiswahili cha watanzania wa bara na visiwani. Vipi mombasa, lamu, pate ambako wanaongea kiswahili. MIE SIJALIZIKA NA JIBU LAKO NAONA KAMA UMEPONDANGA PONDANGA TU.