Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,502
- 6,458
Habari WanaJF?
Nimekuwa nikiona jamii ya watu wenye ulemavu wakikataa kutumika maneno ya Kiswahili katika ulemavu wao kwa madai kuwa yanaonyesha dharau kwao. Nimejiuliza sana kwa nini iwe ni walemavu wote?
Mfano: Zeruzeru - watu wenye Albinism
Kiwete - Wanataka waitwe walemavu wa miguu
Kipofu - Wanataka waitwe walemavu wa macho au wenye uoni hafifu
Taahira - Wanataka waitwe walemavu wa akili
Chongo - Wanaka waitwe walemavu wa macho pia
Mbilikimo - sijajua wanataka waitweje lakini ukimwita mtu mfupi Mbilikimo ugomvi wake haushikiki. Anahisi umemdharau.
Andunje - pia ni tabu tupu
Hebu wadau wa Kiswahili tupeni elimu, ni kweli Kiswahili kipo kwa ajili ya kubeza walemavu au ni wao walemavu wanajishtukia?
Nawasilisha