Kiswahili kutumika primary hadi chuo Kikuu, Who is targeted?

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,483
kuna maswali nimejiuliza sana. wanasema syllabus ya mashule kuanzia primary hadi chuo kikuu wanataka kitumike kiswahili. kichwani kwangu nimejiuliza maswali mengi sana.

1. Pale chuo kikuu department ya kiswahili, kuna profesa yeyote ambaye watoto wake wanasoma shule ya msingi mlimani? au magari ya English medium schools yanapishana asubuhi kubeba watoto wao kupeleka international school?

2. kuna msomi yeyote ambaye angependa watoto wake waende shule zinazofundisha kiswahili tangu primary hadi chuo kikuu?

3. Maadamu nafasi ya kujifunza kiingereza ipo tangu mtoto akiwa mdogo, je, asome kiswahili na kiingereza atakuja kuhangaika ncho yeye mwenyewe akiwa mtu mzima? au mtoto azoeshwe kiingereza tangu akiwa mdogo ili kije kimsaidie hata akiwa mtu mzima katika kazi za kimataifa, biashara na mambo mengine?

4. kusema kiswahili iwe medium of instruction wanalenga watoto wa wenye nacho? au watoto wa masikini kayumba? isijetokea watoto wote wa wenye nacho wakaenda shule za kiingereza halafu watoto wa masikini wakaendelea kwenda shule zza kayumba, hapo si ndio tunazidi kutengeneza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho, watoto wa wenye nacho na watoto wa wasio nacho? mtoto wangu mimi anayesoma international school hata kama ya kubambia tu akajua kiingereza atakuwa katika level moja ya ushindani na mtoto wa shule za kayumba anayesoma kiswahili throughout?

5. ikija kuchukuliwa sensa, watoto watakaokuwa wanasoma shule za kayumba na watakao soma shule z akiingereza, haitatokea kuwa tumewatenga wasio nacho kuwatupia kule shule za kayumba ili sisi ambao kidogo Mungu ametujalia tuendelee kuwa juu na watoto wetu wawe kwenye nafasi ya ushindani zaidi ya wale akina kayumba?

6. je? kama tukiamua kusema kuanzia primary school watoto wote hata kwa kina kayumba, kama walivyofanya Rwanda, medium of instruction kiwe ni kiingereza, je, watoto wetu tunaowazaa watasahau kiswahili hiki ambacho tunajifanya kukilinda? mbona mimi nilizaliwa kijijini nikasoma kijijini lakini tangu nikiwa na miaka 15 hadi leo miaka mingi sana imepita sijawahi kuishi kijijini lakini lugha yangu ya kabila ninaijua vizuri kuliko hata kiswahili wakati mjini huwa siongei kabisa lugha yangu hadi mara chache sana nikutane na mkabila mwenzangu? hata mke wangu hajui lugha ya kabila langu. je, tukiweka kiwek iingereza kwani watoto wetu watakisahau icho kiswahili?

7. kwanini tusiweke english itumike primary hadi university?

8. na je? kwa maana hiyo, hiyo sera ikipita, ina maana hata hao kina st.mary's inabidi wafundishe watoto wao kwa kiswahili? kwa hiyo kutakuwa hakuna international school tz? na watoto wa ma diplomats nao wafundishe kama sisi? hao waliotoa proposal hiyo walifikiria haya?

9. ninaamini, mimi pamoja na wewe ambaye walau kwa mwezi unao uwezi kupata walai ka laki saba na kuendelea hata kama mwalimu wa primary, unao uwezo wa kupeleka mtoto wako english medium. hivyo watoto wa wakulima tu ndio watajikuta wamekusanywa kwenye hiyo sera. watoto wa walimu wa kiswahili pale university of dsm ambao wamekuwa wakinyoosha sana midomo yao mirefu kupendekeza kiswahili kitumike mashuleni, wote wanapeleka watoto wao english medium.

10. sote tunajua hasara ambayo vijana wetu wanaipata katika ushindani wa soko la ajira za kimataifa hata za kitaifa, mtu hajui kujieleza kwa kiingereza kabisa, kwasababu amesoma kwa kuchanganya. angeanzia primary hadi unviersity anasoma kiingereza angekuwa fluent kama wenzetu kenye na uganda.

WATANZANIA NI NANI AMETULOGA? mbona tunapenda sana unafiki na kuongea mambo ya usoni wakati moyoni tunawaza mengine? tunapenda kupendekeza kiswahili wakati watoto wetu tunawapeleka english medium hivyo wale wasio na uwezo ndio wapeleke kayumba?

bora nipeleke watoto wangu wakasoma uganda na kenya, hata mimi na waifu tukila matembele lakini watoto wangu nitawaepusha na huu ujinga wa kiswahili. Mungu ibariki Tanzania.
 
Watanzania tumechoka na Lugha za watu ,,
Tumezoea kukariri tyuuu kiingereza.
Hamuoni nchi kama Japan, Marekani na nchi za Uarabuni zinatumia Lugha zao kama Medium at schools.
Sasa wabongo wenye Elimu duni, poor thnkng capacities wata lipinga.
Acheni tutumie Kiswahili hatutakariri tena Bali tutaelewa darasani.
 
Mawazo ya kipuuzi hayo. Unataka kusema huko Uingereza wanakojifunza kwa lugha yao ya Kiingereza hakuna wanaofeli masomo? Mzzzh...
 
Watanzania tumechoka na Lugha za watu ,,
Tumezoea kukariri tyuuu kiingereza.
Hamuoni nchi kama Japan, Marekani na nchi za Uarabuni zinatumia Lugha zao kama Medium at schools.
Sasa wabongo wenye Elimu duni, poor thnkng capacities wata lipinga.
Acheni tutumie Kiswahili hatutakariri tena Bali tutaelewa darasani.
pamoja na kusema hayo, je? watoto wako wewe umewapeleka shule za kayumba au english medium. kuwa mkweli.

vilevile, japan, china na nchi nyingine sio kwamba hawapendi kiingereza, wanahangaika sana kujifunza kiingereza. nchi nyingi wasizoongea kiingereza watu wanapata shida sana kujifunza kiingereza kwasababu kiingereza kinatawala dunia, kazi za kimataifa, seminar za kimataifa, vitu vingi vya kimataifa itabidi usome kiingereza.

wewe kama unaogopa kiingereza labda unaona kigumu, ujue kuwa kuna watu icho kiingereza wanaona kama kiswahili tu, usiogope kimbombo. kama kweli wewe unapeleka mtoto wako kwenye shule za kiswahili basi uwe wa kwanza kurusha jiwe hapa. tuwe wakweli tunawatenga watoto wa masikini bure kwasababu asilimia kubwa yetu sisi tulionacho kidogo hatutapeleka watoto wetu shule hizo za kiswahili. bora nimpeleke hata nje ya tz kuliko kumpeleka kwenye kiswahili.

kiswahili mimi kilinitesa sana, kwanza nilisoma shule za kayumba hadi university, na nilipoanza kutoka nje ya nchi kusoma na watu waliotumia english ndipo nilipoona umuhimu wa kimombo. tusilimit watoto wetu kwenye soko la kimataifa la kibiashara na ajira kwa kukumbatia kiswahili ambacho hakina hata terminologies za technologia. laiti kama ningesoma english medium kuanzia primary nisingepata shida semesters za mwanzo kwenye nchi za watu nilipoonekana nababia tu kimombo. nashukuru Mungu kwa miaka mingi nimeishi huko niko fluent.
 
Ngeli ni lazima, anayetaka kiswahili chini hadi juu namshangaa sana, hata china na japan wakisoma some courses kama programming Ngeli hawaikimbii, lazima waitumie tu.. Kiswahili chenyewe hakina vocabularies za kutosha kwa hizi technical terms, tutabaki kuanza kupanga maneno na kukariri mapya tu huku ya Ngeli tayari yapo, Tutumie Ngeli chini hadi juu twende kimataifa, hata Nigeria wenyewe mziki wao tunausikiliza sababu wanaimba Ngeli... Kiswahili kifutwe ka vipi ikiwezekana hata mtaani Tutumie Ngeli maana spelling mistakes zenyewe zimezidi humu JF kiswahili hatukijui... Ngeli sio lugha ya mzungu, ni lugha ya binadamu, aliyesema Kuna lugha ya mzungu au mwafrika hajitambui.. Wazungu si watulipishe ka vipi tukitumia kiingereza kama kweli wao ndo owners
 
watu wanaona kigumu. wanakimbia ngeli wakisingizia kiswahili kama tunu ya taifa kumbe wanasepa ngeli.
 
Wanalengwa watoto wa makabwela
ni watoto wa makabwela tu ndio wanalengwa. hata watoto wa hao wanaosapoti kiswahili hapo chuo kikuu udsm wanapeleka watoto wao english medium. si unafiki huo?
 
Hapo nakubaliana na wewe inajengwa tabaka ya elites.

Mfano, Kiswahili kuanza kukijaza maneno mapya ya Kisayansi itakuwa sshida kubwa sana, itakuwa ni kama kujifundisha lugha mpya isiyokuwepo duniani.

The only solution labda tutumie maneno ya Kiarabu ya kisayansi jumla jumla, ndiyo lugha pekee itayokuwa rahisi kuingiliana na Kiswahili kuliko lugha nyingine yoyote ile.
 
for poor people like us education is the key for our liberation"wanaada mazingira ya kutawala wanetu
 
tuwaachie shule hizo watoto wa vijijini, watoto wa manzese, tandale na mbagala?
 
kuna maswali nimejiuliza sana. wanasema syllabus ya mashule kuanzia primary hadi chuo kikuu wanataka kitumike kiswahili. kichwani kwangu nimejiuliza maswali mengi sana.

1. Pale chuo kikuu department ya kiswahili, kuna profesa yeyote ambaye watoto wake wanasoma shule ya msingi mlimani? au magari ya English medium schools yanapishana asubuhi kubeba watoto wao kupeleka international school?

2. kuna msomi yeyote ambaye angependa watoto wake waende shule zinazofundisha kiswahili tangu primary hadi chuo kikuu?

3. Maadamu nafasi ya kujifunza kiingereza ipo tangu mtoto akiwa mdogo, je, asome kiswahili na kiingereza atakuja kuhangaika ncho yeye mwenyewe akiwa mtu mzima? au mtoto azoeshwe kiingereza tangu akiwa mdogo ili kije kimsaidie hata akiwa mtu mzima katika kazi za kimataifa, biashara na mambo mengine?

4. kusema kiswahili iwe medium of instruction wanalenga watoto wa wenye nacho? au watoto wa masikini kayumba? isijetokea watoto wote wa wenye nacho wakaenda shule za kiingereza halafu watoto wa masikini wakaendelea kwenda shule zza kayumba, hapo si ndio tunazidi kutengeneza gap kati ya wenye nacho na wasio nacho, watoto wa wenye nacho na watoto wa wasio nacho? mtoto wangu mimi anayesoma international school hata kama ya kubambia tu akajua kiingereza atakuwa katika level moja ya ushindani na mtoto wa shule za kayumba anayesoma kiswahili throughout?

5. ikija kuchukuliwa sensa, watoto watakaokuwa wanasoma shule za kayumba na watakao soma shule z akiingereza, haitatokea kuwa tumewatenga wasio nacho kuwatupia kule shule za kayumba ili sisi ambao kidogo Mungu ametujalia tuendelee kuwa juu na watoto wetu wawe kwenye nafasi ya ushindani zaidi ya wale akina kayumba?

6. je? kama tukiamua kusema kuanzia primary school watoto wote hata kwa kina kayumba, kama walivyofanya Rwanda, medium of instruction kiwe ni kiingereza, je, watoto wetu tunaowazaa watasahau kiswahili hiki ambacho tunajifanya kukilinda? mbona mimi nilizaliwa kijijini nikasoma kijijini lakini tangu nikiwa na miaka 15 hadi leo miaka mingi sana imepita sijawahi kuishi kijijini lakini lugha yangu ya kabila ninaijua vizuri kuliko hata kiswahili wakati mjini huwa siongei kabisa lugha yangu hadi mara chache sana nikutane na mkabila mwenzangu? hata mke wangu hajui lugha ya kabila langu. je, tukiweka kiwek iingereza kwani watoto wetu watakisahau icho kiswahili?

7. kwanini tusiweke english itumike primary hadi university?

8. na je? kwa maana hiyo, hiyo sera ikipita, ina maana hata hao kina st.mary's inabidi wafundishe watoto wao kwa kiswahili? kwa hiyo kutakuwa hakuna international school tz? na watoto wa ma diplomats nao wafundishe kama sisi? hao waliotoa proposal hiyo walifikiria haya?

9. ninaamini, mimi pamoja na wewe ambaye walau kwa mwezi unao uwezi kupata walai ka laki saba na kuendelea hata kama mwalimu wa primary, unao uwezo wa kupeleka mtoto wako english medium. hivyo watoto wa wakulima tu ndio watajikuta wamekusanywa kwenye hiyo sera. watoto wa walimu wa kiswahili pale university of dsm ambao wamekuwa wakinyoosha sana midomo yao mirefu kupendekeza kiswahili kitumike mashuleni, wote wanapeleka watoto wao english medium.

10. sote tunajua hasara ambayo vijana wetu wanaipata katika ushindani wa soko la ajira za kimataifa hata za kitaifa, mtu hajui kujieleza kwa kiingereza kabisa, kwasababu amesoma kwa kuchanganya. angeanzia primary hadi unviersity anasoma kiingereza angekuwa fluent kama wenzetu kenye na uganda.

WATANZANIA NI NANI AMETULOGA? mbona tunapenda sana unafiki na kuongea mambo ya usoni wakati moyoni tunawaza mengine? tunapenda kupendekeza kiswahili wakati watoto wetu tunawapeleka english medium hivyo wale wasio na uwezo ndio wapeleke kayumba?

bora nipeleke watoto wangu wakasoma uganda na kenya, hata mimi na waifu tukila matembele lakini watoto wangu nitawaepusha na huu ujinga wa kiswahili. Mungu ibariki Tanzania.
Mkuu kuhusu shule ya Msingi Mlimani hujafanya utafiti wa kutosha nenda tena kaulize pale Mlimani Primary school hasa ile mpya wapo kibao watoto wa Madokta na Maprof.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom