Paul Kijoka
JF-Expert Member
- Oct 25, 2010
- 1,399
- 256
Tanzania ni nchi maskini bado hivyo tusitegemee lugha yetu kukua kwa haraka labda mtu ajifunze kea ridhaa yake na ili sisi tafanikiwe ktk nyanja mbali mbali tunahitaji kujifunza kingereza kwa namna moja au nyingine kitasaidia kujikwamua ktk hatua kadhaa tunazokutana nazo maishani
Ndugu yangu mimi nakaa nje ya Tanzania kwa miaka mingi sasa. kabla ya kuondoka Tanzania nilikuwa proud sana na kiswahili lakini baada ya kukaa nje nimegundua viongozi wetu walikosea sana kusisitiza kiswahili na kupuuza kiingereza!! Ndugu yangu narudia tena kwa nchi masikini kama Tanzania, lugha ya kiingereza ni muhimu sana.
Hapo kwenye mstari...ni kweli au urongo???
Hivi mjerumani(mwenye uchumi unaoongoza barani ulaya) ametumia kiingereza kufika hapo alipo???!!!
Nadhani maendeleo ni zaidi ya lugha...kama hatusomi, hatufanyi kazi kwa bidii, hatulei na kukuza ubunifu, sifikiri kama lugha pekee itatufikisha kwenye nchi ya kanaani!!!
Nakumbuka tukiingia sekondari miaka ya mwanzo wa tisini, tulikutana na vijana kutoka Arusha School ambao walikuwa wakisakata kimombo kweli kweli...lakini baada ya muda nasi tukiwa tayari kimombo kimenza kukubali...tulikuwa level moja na hatimaye baadhi yao tukawapiku, siri ikiwa ni kujituma na kusoma kwa bidii.
Niseme kwamba, tunakihitaji sana kizungu na kwa maneno ya Mh Lowasa, tunakihitaji kichina. Lakini bado bila ya vitu hivyo nimevitaja hapo juu...Lugha si lolote si chochote.
Ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.
1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana Tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(English) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.
Hoja hii umeitoka kwa kukurupuka,hujatuonesha madhara yake. Kwahiyo ina matatizo gani sasa!!! Au ulitaka kumaanisha kuwa ukifika China na hela yako huwezi kununua bidhaa? kwahiyo watanzania wajifunze Lugha zot e za dunia hii kwamba ukitaka kwenda Rwanda, Angola, SA, Brazil, Korea, China.... ujifunze lugha zao kwanza. Au unamaanisha hakuna wakarimani? Ukienda kuomba omba at?
2. Wageni wakija Tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano PITA KUSHOTO. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.Mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara Tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda Kenya na Uganda kuchukua bidhaa kuliko Tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa Lugha.wanasema kwenda Tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.
Hoja hii ni kichekesho, kwakifupi hiyo ndo ajira ya watu wetu kufanya kazi ya ukarimani. Nadhani hujui kuwa pengine hawana wakitakacho na kama kingekuwepo basi wataitumia lugha yetu mara moja. Alafu Sasa tukitoka hapo tutakuomba upendekeze tutafsiri ata majina yetu, mitaa yetu..... hii ni hatari, kisa tuwapendezeshe wageni. Wanaenda kenya si kwakuwa kunatumika Kiingereza bali ni sera na taratibu nzuri za uongozi wa Kenya. Huku serikali imelala. Ni ufisai kwenda mbele. na kwa taarifa yako wakija huku wanaenda kwa wamasai na si UDSM mf!
3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya Lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?
Hoja hii si ya kweli. Nadhani hujafanya itafiti au umetumwa kuinusuru CCM na ulalaji usingizi na kukosa ubunifu. Hapa bila kuuma uma maneno ni uzembe wa Serikali na idara ya utalii hasa wizara nzima. Hakuna anayewazuia kutangaza kwa lugha zote za dunia hii. Wamelala.
4.Tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa BONGO. (Kwa wale mliobahatika kuangalia stand up Zambia kilichorushwa na Africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia Joti, Masanja.
Ndugu yangu, tatizo hujanijibu maswali yangu ya awali, una mambo mengi huyajui, nakusaidia, Kazi yoyote ni lazima uisomee. kama hujaisomea uifanye kwa kiwango cha kimataifa. Kina masanja wanaifanya kwa kiwango cha Bongo hasa Dar na Uswazi tu. hawa jamaa wamekuja tu toka mtaani na wasanii wetu wengi hawajaona ata ubao! Sasa unataka wafanye maajab gani hapo. Unawajua waswana na mziki wao ambao unapendwa dunia nzima? Wanatumia lugha gani? Wanakijua Kiingereza? Unakumbuka wale Makirikiri walitinga hadi ufunguzi wa kombe la dunia. Unamjua msomi Mr. Bean? Anasaidiwa na Lugha?
5.Tuna wachungaji wazuri sana(Pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.B Joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba Joshua unaupako kuliko wengine.
Hihi nayo kaili. Sasa Unailinganisha Nigeria na TZ? hawa jamaa wameanza usanii muda mrefu sana. TB Joshua ni msanii alafu promo tu! Ila ni bora ukumbuke Kuwa babu wa loliondo alivuta watu wengi kwa usanii wake bila shaka na si kwa kiingereza. pia mambo ya imani uendana na inani ya watu. Watu wanaenda yesu alipozaliwa na kumalizia maisha yake si kwakiingereza. Au waislam hawaendi Saudia kwakujua lugha. Hoja yako ni dhaifu na niya kitoto.
6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri Wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema YES, YES YES.
Si bure wewe umetumwa na magamba, hivi mkuu unasema kweli hapo! Acha hoja za kipuuzi wewe, hapo ni ufisadi tu. Nakuomba uwatake radhi kina Prof. Shivj, Dr. Nshala, Prof. Majamba, kuwa hawajui kusoma mikataba. Tumia kichwa vizuri unapotaka kudanganya au kuwazuga watu. Ebu angalia Ndg. yangu, Karamagi hajui kiingereza? Kwahiyo ukijua kiingereza unaijua sheria tayari!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Unachanganya lugha na utaalamu au??????
7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'Tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,Kenya, Uganda zambia lakini Tanzania hakuna na hata katika ratiba yao Tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?
Quote by Jidu
ndugu yangu!haya unayozungumza umefanyia utafiti kweli?hivi lugha ndio kikwazo cha sisi kuto tambulika au kuto kuwa na maendeleo?naomba nitofautiane na wewe kwa hilo.mimi na amini fikra sahihi huja kwa lugha sahihi inayoeleweka kwa jamii husika.nilisha wahi fika china,kwakweli wale jamaa ni kichina kwa kwenda mbele unaweza shindwa nunua kitu dukani au kwenda mahali fulani kwa kuwa mmeshindwa kuelewena kwa lugha lakini hebu angalia walivyopiga hatua kimaendeleo kwa kila nyanja!hivyo basi usitukuze lugha za kigeni na kuacha za kwako kisa eti hatutaendelea,jaribu kuja na mbinu mbadala ya sisi wapi tumekosea ila hili la lugha hapana!
Tatizo ni kwamba hata watetezi wa Kiingereza hawakijui sawasawa wanafuata mkumbo tu! Ukweli ni kwamba Kiswahili kina uwezo tosha kabisa wa kujifunza isipokuwa kunakosekana msukumo wa kisiasa. Nilitazama siku moja mdahalo wa lugha ya kiingereza juu ya lugha gani itumike kufundishia nilicheka hadi mchozi kunitoka kwani waliojifanya eti wanatetea kiingereza walizungumza kiingereza kibovu kweli kweli! isitoshe eti ndiyo walikuwa walimu! Si ajabu sana kwa watu kutetea lugha ya mtawala wao kwani hata waingereza wenyewe kiingereza hakikuwa lugha yao rasmi ya kufundishia na waliihusudu sana lugha ya wakoloni wao wafaransa na kilatini. Utawala wa kule ulipofanya maamuzi ya kutumia lugha ya kiingereza pekee kufundishia inasemekana wapo waliopinga hadi mmoja wa maprofesa kuamua kujiua ili asiishi kuishuhudia aibu ya kuporomoka kwa elimu! Natamani mjinga yule angerudi leo aone jinsi watanzania wanavyojikomba kwa waingereza sawa na yeye! Wachina wamefika walipofika baada ya kufanya maamuzi magumu ya kuachana na lugha za wageni kufundishia na kuamua kutumia lugha yao! Mtu mmoja tu aliibadilisha hali hiyo; Mao Tse Tung! Tatizo letu kubwa ni kufanya maamuzi nusu nusu, eti wanafunzi wasome darasa la kwanza hadi la saba kiswahili na kisha kiingereza la Tisa na kuendelea! Nasisitiza tena, tunahitaji viongozi wenye ubavu wa kufanya maamuzi magumu ili kufikia lengo la kukifanya kiswahili lugha rasmi ya kujifunzia, lakini si hawa wanaoinajisi na kuisaliti kila siku hadi Bungeni.Quote by Masauni
Wewe ulifika china miaka gani? Nataka kukuhakikishia kuwa sasa hivi wanajifunza kwa bidii sana! Naomba ulewe hivi unaweza kuwa na ideas nzuri sana very constructive ideas lakini usipoweza kuzielezea hizo ideas kwa watu wakazielewa utamarginalized yourself. Dunia imekuwa ni kama kijiji. Maendeleo katika nchi yanaletwa katika kuwasiliana na si kuwasiliana sisi kwa sisi tu na watu wa nchi nyingine pia. Tukubali tusikubali Kiingereza ndio lugha ya kimataifa lazima tuifahamu kama tunahitaji kupiga hatua katika maendeleo
Paul Kijoka
Narudia kusema tena na tena nchi masikini hatutaendelea kama hatutakubali kubadilisha lugha ya mawasiliano na kuwa kiingereza. Natambua vizuri sana kuwa kuna other factors zinazochangia maendeleo ya nchi lakini pia Lugha ni one of the factor inayochangia katika maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja. Na pointi yangu nimeijenga katika msingi huo. Nchi kama Japan,china na german kunatofauti kubwa sana na sisi. Ni kupe mfano mzuri, unajua zaidi ya 50% ya watu wote wa dunia hii wanazungumza english lakini wazungumzaji wa kiswahili hawafiki ata 1% ya watu wote duniani. hii 1% haiwezi ikawa peke yake na lugha yake itafika mahali itashindwa kuendelea. tunatakiwa tuwe na mawasiliano mazuri na hiyo 50% ili shughuli za maendeleo zifanyike kwa urahisi.
Jamani si vibaya kuiga mambo mazuri ya mataifa ya wengine mfano nigeria, kenya, zimbabwe wanalugha zao lakini huwezi ukakuta kijana anashindwa kuzungumza kiingereza. Tuachane na fikra za kusema kila kitu tukiiga cha wazungu tunatafsiri kama neo colonialism. Tunashindwa kuangalia mahali tunapokosea tunabaki kusema wazungu wazungu.
Mkuu mbona unaleta story za kusadikika? weka reference. Ndugu yangu tembea uone!! inawezekana wewe umezaliwa Dar, umesoma Dar, Umepata kazi dar, umeoa ukiwa dar. Ulimwengu unaoufahamu ni Dar es salaam tu!! Katika karne hii ya Science na teknolojia, tunahitaji lugha ya kimataifa. Ninawafahamu wasomi wazuri sana wa kitanzania ambao walishindwa kuiwakilisha Tanzania katika nyanja za utafiti na sayansi nje ya nchi kwa sababu ya lugha ya kiingereza lakini mkiwa mnajadili kwa kiswahili ni vichwa si mchezo.Tatizo ni kwamba hata watetezi wa Kiingereza hawakijui sawasawa wanafuata mkumbo tu! Ukweli ni kwamba Kiswahili kina uwezo tosha kabisa wa kujifunza isipokuwa kunakosekana msukumo wa kisiasa. Nilitazama siku moja mdahalo wa lugha ya kiingereza juu ya lugha gani itumike kufundishia nilicheka hadi mchozi kunitoka kwani waliojifanya eti wanatetea kiingereza walizungumza kiingereza kibovu kweli kweli! isitoshe eti ndiyo walikuwa walimu! Si ajabu sana kwa watu kutetea lugha ya mtawala wao kwani hata waingereza wenyewe kiingereza hakikuwa lugha yao rasmi ya kufundishia na waliihusudu sana lugha ya wakoloni wao wafaransa na kilatini. Utawala wa kule ulipofanya maamuzi ya kutumia lugha ya kiingereza pekee kufundishia inasemekana wapo waliopinga hadi mmoja wa maprofesa kuamua kujiua ili asiishi kuishuhudia aibu ya kuporomoka kwa elimu! Natamani mjinga yule angerudi leo aone jinsi watanzania wanavyojikomba kwa waingereza sawa na yeye! Wachina wamefika walipofika baada ya kufanya maamuzi magumu ya kuachana na lugha za wageni kufundishia na kuamua kutumia lugha yao! Mtu mmoja tu aliibadilisha hali hiyo; Mao Tse Tung! Tatizo letu kubwa ni kufanya maamuzi nusu nusu, eti wanafunzi wasome darasa la kwanza hadi la saba kiswahili na kisha kiingereza la Tisa na kuendelea! Nasisitiza tena, tunahitaji viongozi wenye ubavu wa kufanya maamuzi magumu ili kufikia lengo la kukifanya kiswahili lugha rasmi ya kujifunzia, lakini si hawa wanaoinajisi na kuisaliti kila siku hadi Bungeni.
Ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.
1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana Tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya Tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(English) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.
2. Wageni wakija Tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano PITA KUSHOTO. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.Mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara Tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda Kenya na Uganda kuchukua bidhaa kuliko Tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa Lugha.wanasema kwenda Tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.
3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya Lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?
4.Tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa BONGO. (Kwa wale mliobahatika kuangalia stand up Zambia kilichorushwa na Africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia Joti, Masanja.
5.Tuna wachungaji wazuri sana(Pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.B Joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba Joshua unaupako kuliko wengine.
6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri Wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema YES, YES YES!
7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'Tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,Kenya, Uganda zambia lakini Tanzania hakuna na hata katika ratiba yao Tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?
Nchi nyingi sasa hivi zinajifunza Kiingera hata china taifa kubwa wako busy kujifunza kiingereza Sisi masikini wakutupwa tunangangana na kiswahili ambacho mwisho wake ni mipakani tu! Viongozi wetu lazima pia waanalie hiyo watu waanza kufundishwa kiingereza tangu chekechea, maofisini lugha ya kiingereza isisitizwe, mikutano maofisini ifanyike kwa kiingereza. WITHOUT ENGLISH YOU ARE MARGINALIZED YOURSELF
Wewe ulifika china miaka gani? Nataka kukuhakikishia kuwa sasa hivi wanajifunza kwa bidii sana! Naomba ulewe hivi unaweza kuwa na ideas nzuri sana very constructive ideas lakini usipoweza kuzielezea hizo ideas kwa watu wakazielewa utamarginalized yourself. Dunia imekuwa ni kama kijiji. Maendeleo katika nchi yanaletwa katika kuwasiliana na si kuwasiliana sisi kwa sisi tu na watu wa nchi nyingine pia. Tukubali tusikubali Kiingereza ndio lugha ya kimataifa lazima tuifahamu kama tunahitaji kupiga hatua katika maendeleo
Paul Kijoka
Narudia kusema tena na tena nchi masikini hatutaendelea kama hatutakubali kubadilisha lugha ya mawasiliano na kuwa kiingereza. Natambua vizuri sana kuwa kuna other factors zinazochangia maendeleo ya nchi lakini pia Lugha ni one of the factor inayochangia katika maendeleo ya nchi na mtu mmoja mmoja. Na pointi yangu nimeijenga katika msingi huo. Nchi kama Japan,china na german kunatofauti kubwa sana na sisi. Ni kupe mfano mzuri, unajua zaidi ya 50% ya watu wote wa dunia hii wanazungumza english lakini wazungumzaji wa kiswahili hawafiki ata 1% ya watu wote duniani. hii 1% haiwezi ikawa peke yake na lugha yake itafika mahali itashindwa kuendelea. tunatakiwa tuwe na mawasiliano mazuri na hiyo 50% ili shughuli za maendeleo zifanyike kwa urahisi.
Jamani si vibaya kuiga mambo mazuri ya mataifa ya wengine mfano nigeria, kenya, zimbabwe wanalugha zao lakini huwezi ukakuta kijana anashindwa kuzungumza kiingereza. Tuachane na fikra za kusema kila kitu tukiiga cha wazungu tunatafsiri kama neo colonialism. Tunashindwa kuangalia mahali tunapokosea tunabaki kusema wazungu wazungu.
ninaomba kuanzisha hii mada baada ya kusikia kwamba kuna mahali walimu wamefukuzwa kwa sababu ya kuongea kiswahili katika mazingira ya shule.
Niseme tu kwamba naunga mkono jambo hilo kwa asilimia mia. Sababu ni hizi hapa.
1. Tutambue kuwa kiswahili ni lugha inayozungumzwa sana tanzania na ukitoka nje ya mipaka ya tanzania kiswahili chako unaweka mfukoni! Lazima tujufunze lugha za kimataifa(english) ili tulahisishe mawasiliano na mataifa mengine.
2. Wageni wakija tanzania wanapata taabu kweli, matangazo ya biashara yameandikwa kwa kiswahili, barabara nazo unakuta vibao vimeandikwa kwa kiswahil mfano pita kushoto. Sasa jamani wageni wetu ambao wengi wanakuja kwa maswala ya biashara inakuwa ngumu sana.mgeni kuendesha gari tanzania ni ngumu sana. Mgeni kufanya biashara tanzania ni ngumu sana!! Kuna jamaa wafanyabiashara wengi sana nawafahamu wanaprefer kwenda kenya na uganda kuchukua bidhaa kuliko tanzania na sababu wanazozitoa ni ugumu wa lugha.wanasema kwenda tanzania ni gharama zaidi maana inabidi umtafute mkalimani ambaye utamlipa.
3. Kenya inatangaza mlima kilimanjaro kwa sababu ya lugha wanayotumia inaeleweka duniani kote. Sisi tunatangaza mlima kilimanjaro kwa kiswahili wataelewa nini wageni?
4.tunawasanii wazuri sana wa muziki, tamthiliya, vichekesho, ambao wangesaidia sana kuitangaza nchi yetu kimataifa na wao pia kufaidika, lakini wamebaki eti wasanii wa bongo. (kwa wale mliobahatika kuangalia stand up zambia kilichorushwa na africa magic channel mtakubaliana na mimi wale jamaa 3 walioshinda sasa hivi ni comedian wakimataifa wanazunguka nchi mabalimabali sababu ni lugha tu, maana kwa ukweli hawawezi kumfikia joti, masanja.
5.tuna wachungaji wazuri sana(pastors) lakini mahubiri yao ni kwa kiswahili. T.b joshua anajulikana kila mahali kwa sababu mahubiri yake ni ya kiingeraza. Si kwamba joshua unaupako kuliko wengine.
6. Mikataba mibovu tunayoingia na wawekezaji ni kwa sababu ya lugha tunashindwa kuilewa vizuri wawekezaji wanapokuja ilitusionekane ni mbumbumbu wa kiingereza tunabaki kusema yes, yes yes!
7. Kwa watazamaji wenzangu wa aljazeera kuna kipindi kinaitwa 'tea cafe (kama sijakosea)kinaongelea maswala mbalimbali yanayohusu nchi husika kipindi hicho kinapofanyika. Kipindi hicho kimefanyika,kenya, uganda zambia lakini tanzania hakuna na hata katika ratiba yao tanzania haimo simply because hakuna watu kama wanasiasa na baadhi ya watu mahalufu ambao wako tayari kujadili kwa kimombo! Sasa dunia itatuelewa vipi matatizo na mipango yetu ?
Nchi nyingi sasa hivi zinajifunza kiingera hata china taifa kubwa wako busy kujifunza kiingereza sisi masikini wakutupwa tunangangana na kiswahili ambacho mwisho wake ni mipakani tu! Viongozi wetu lazima pia waanalie hiyo watu waanza kufundishwa kiingereza tangu chekechea, maofisini lugha ya kiingereza isisitizwe, mikutano maofisini ifanyike kwa kiingereza. Without english you are marginalized yourself
Ulichosema ni ukweli mtupu, ila tegemea kushambuliwa na watu ambao hawako tayari kuukubali hii fact. Tegemewa kuambiwa Wachina, Wajerumani, Wajapani, Wafaransa wanaongea lugha zao na wanaendelea.
Vile vile subiri kuambia kuwa unawaabudu wazungu.
Na mwisho kabisa, tegemea kuambiwa kuwa Nyerere aliasisi lugha takatifu ya Kiswahili - kwa hiyo anayekipinga anatenda dhambi kwa Mnyaz Mungu.
countries where english is a dejure /official language (list of countries where english is an official language - wikipedia, the free encyclopedia)
[table="width: 245"]
[tr]
[td]country[/td]
[td]region[/td]
[/tr]
[tr]
[td]botswana[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]cameroon[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]eritrea[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]ethiopia[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]ghana[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]jamaica[/td]
[td]caribbean[/td]
[/tr]
[tr]
[td]kenya[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]lesotho[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]liberia[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]malawi[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]namibia[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]nigeria[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]sierraleone[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]solomonislands[/td]
[td]oceania[/td]
[/tr]
[tr]
[td]southafrica[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]southsudan[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]sudan[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]swaziland[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]tanzania[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]thegambia[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]uganda[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]zambia[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[tr]
[td]zimbabwe[/td]
[td]africa[/td]
[/tr]
[/table]
hebu angalieni hizo nchi zinazoongea kiingereza. Wametuzidi nini?
Kiingereza sio muhimu kiviiile kwa maendeleo yetu. Ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, sera nzuri (siasa safi), na uongozi makini. Kiingereza is not one of the requirements. In fact, kama (kwa muujiza) tanzania ingekuwa economically superpower, majirani wote wangekuja tu kutafatua kazi na lazima wangejifunza kiswahili.
Hebu fikiria, kwa hapa nchini, inasemekana, kilimanjaro wameendelea zaidi kuliko sehemu nyingine. Je wanaongea kiingereza? Si wanaongea kichaga na kipare tu?