Joseverest
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 53,261
- 72,431
ETYMOLOGY?Habari za leo. Napenda kuwapa rai ndugu zangu.
Najua sisi sote humu ndani ya hili *_kundi sogozi_* tunamiliki _*simu tamba*_. Tuweni makini kwani kutumia _*sikanu*_ zetu _*mkondoni*_ kunaweza wapa mwanya wezi wa mtandaoni kutuibia. Wezi hutuma _*maunzi laini*_ yanayoweza kuharibu _*kitumi*_ chako au kuingilia _*makavazi*_ ya _*sikanu*_ yako. Wakishatuma _*maunzi laini*_ hayo nawe pasi na kujua ukibofya _*kiungo*_ kilichobeba _*maunzi laini*_ unakuwa _*umeshapakua*_ na _*kusanidi mtaliga*_ wenye uwezo wa kubadili au _*kughushi nenomsingi*_ lako na hivyo kunyima uwezo wa kuitumia _*sikanu*_ yako kwa kuifanya _*puku*_ kushindwa kutambua amri unazoipatia _*baobonye*_ ya _*kiwambagusa*_ cha _*sikanu*_ yako.
*JE KISWAHILI KITUMIKE KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KWA NGAZI ZOTE ZA ELIMU?*
[emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652]
*Tafsiri ya maneno hayo*
1. Kundi sogozi = chatting group
2. Sikanu = smartphone
3. Kitumi=device
4. Maunzi laini=software
5. Kiungo=link
6. Kusanidi=install
7. Mtaliga=virus
8. Neno msingi=keyword
9. Puku=mouse
10.Baobonye=keyboard
11. Kiwamba gusa=touch screen
12. Makavazi=archives
13. Simu tamba=mobile phone
14. Mkondoni=online
15. Pakua=download
C&P
ETYMOLOGY?
Wanayaunda kutoka wapi? There is what we call the science of the origin of the word...etymologyHuenda mkuu..sijui haya maneno wanayatolea wapi
Habari za leo. Napenda kuwapa rai ndugu zangu.
Najua sisi sote humu ndani ya hili *_kundi sogozi_* tunamiliki _*simu tamba*_. Tuweni makini kwani kutumia _*sikanu*_ zetu _*mkondoni*_ kunaweza wapa mwanya wezi wa mtandaoni kutuibia. Wezi hutuma _*maunzi laini*_ yanayoweza kuharibu _*kitumi*_ chako au kuingilia _*makavazi*_ ya _*sikanu*_ yako. Wakishatuma _*maunzi laini*_ hayo nawe pasi na kujua ukibofya _*kiungo*_ kilichobeba _*maunzi laini*_ unakuwa _*umeshapakua*_ na _*kusanidi mtaliga*_ wenye uwezo wa kubadili au _*kughushi nenomsingi*_ lako na hivyo kunyima uwezo wa kuitumia _*sikanu*_ yako kwa kuifanya _*puku*_ kushindwa kutambua amri unazoipatia _*baobonye*_ ya _*kiwambagusa*_ cha _*sikanu*_ yako.
*JE KISWAHILI KITUMIKE KAMA LUGHA YA KUFUNDISHIA KWA NGAZI ZOTE ZA ELIMU?*
[emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652][emoji652]
*Tafsiri ya maneno hayo*
1. Kundi sogozi = chatting group
2. Sikanu = smartphone
3. Kitumi=device
4. Maunzi laini=software
5. Kiungo=link
6. Kusanidi=install
7. Mtaliga=virus
8. Neno msingi=keyword
9. Puku=mouse
10.Baobonye=keyboard
11. Kiwamba gusa=touch screen
12. Makavazi=archives
13. Simu tamba=mobile phone
14. Mkondoni=online
15. Pakua=download
C&P
mbona kiswahili kinawezekana tu? maneno haya yanaonekana kuwa mageni kwa sabababu tu hayatumiwi mara kwa mara, hata hiyo lugha unayoitumia ulijifunza polepole mpaka ukawa mahiri. tujibidishe tu tudumishe utamaduni wetu, tuachane na ukoloni mambo leo. LUMBA KISWAHILI, JISKIE HURU, KISWAHILI UTAMBULISHO WANGU, AJIRA YANGU.Mi nahisi tubaki hivhiv tulivyo maana hayo maneno mengine ukiyakosea kwa kuyatamka unaweza ukatoka nje ya mada husika
Mobile phone ni rununuHayo maneno nimeyapenda, ngoja niyatunze kwenye SIKANU yangu ili nisipokuwa MKONDONI niwe napitia.
Hapo nilikuwa najua BAOBONYE tu...
haswaaaShughuli pevu !!
Ndio ujifunze na mengine ya ziadaHayo maneno nimeyapenda, ngoja niyatunze kwenye SIKANU yangu ili nisipokuwa MKONDONI niwe napitia.
Hapo nilikuwa najua BAOBONYE tu...
[emoji15][emoji15][emoji15]Nakupa kongole Kwa arafa nzuri
utazoea tu kama ulivozoe MUBASHARA NA MAKINIKIAMi nahisi tubaki hivhiv tulivyo maana hayo maneno mengine ukiyakosea kwa kuyatamka unaweza ukatoka nje ya mada husika
kabisa mkuu..umeona eeWale wasomi na BAKITA watusaidie kurasimisha hayo maneno yawe vizuri tuyajue kila siku.