Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Wakati Dunia ikiadhimisha siku ya Kiswahili, lugha hiyo sasa inaonekana kuvuka mipaka ya Afrika Mashariki, ambapo sasa Jukwaa la Kimataifa la Nasser la nchini Misri limejitokeza kuwawezesha vijana nchini humo kujifunza lugha hiyo.
Siku ya Kiswahili duniani huadhimishwa Julai 7 ya kila mwaka, ambapo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Utamaduni (Unesco) hushirikiana na serikali za mataifa mbalimbali kuadhimisha siku hiyo.
Akizungumza Julai 8, msemaji wa Jukwaa la Nasser Dk Hassan Ghazaly alisema wametumia maadhimisho hayo kuwaunga mkono na kuwawezesha vijana, sambamba na kukuza uwepo wa lugha ya Kiswahili katika majukwaa ya kikanda na kimataifa.
“Lugha hii inatambuliwa kama chombo chenye nguvu cha mazungumzo ya kitamaduni na daraja la mawasiliano ya kibinadamu.
“Idara inaendelea kutekeleza programu maalumu za mafunzo ya kitaalamu katika nyanja za ufasiri na uandishi wa habari za kimataifa, kwa lengo la kuwajengea vijana ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
“Hili linaenda sambamba na kuakisi nafasi inayozidi kuimarika ya Jamhuri ya Misri katika bara la Afrika na ulimwenguni kwa ujumla kupitia matumizi ya lugha ya Kiswahili,” alisema.
Alisema hadi sasa, jumla ya makala 1,455 tayari zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, na wanafunzi 228 kutoka vyuo vya Al-Alsun, Lugha na Ufasiri wamekamilisha programu za mafunzo ya kina kupitia jukwaa la mtandaoni. Wanafunzi wengine 50 wanajiandaa kujiunga na kundi jipya la mafunzo.
“Kama sehemu ya kukuza utofauti wa kitamaduni, jukwaa la "Makala na Maoni" linaloendeshwa na idara linatoa fursa wazi kwa vijana kuwasilisha mawazo yao kwa lugha mbalimbali, ikiwemo Kiswahili, ambapo michango takriban 300 tayari imechapishwa hadi sasa.”