KISUTU: Wema Sepetu na Wafanyakazi wake wakutwa na kesi ya kujibu! Kuanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuona msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili wana kesi ya kujibu kutokana kukabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Aprili 23 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kwamba Wema na wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Hakimu Simba ametoa uamuzi huo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa na Hakimu Simba, Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba amesema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea na wakionekana hawana kesi ya kujibu wataachiwa huru.

Hakimu Simba amesema baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Amesema washtakiwa wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuona msanii na mlimbwende wa Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili wana kesi ya kujibu kutokana kukabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Aprili 23 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na kwamba Wema na wenzake wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.

Hakimu Simba ametoa uamuzi huo baada ya kupitia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi watano wa upande wa mashtaka waliokuwa wakiongozwa na Wakili wa Serikali, Constantine Kakula.

Kabla ya uamuzi huo kutolewa na Hakimu Simba, Wakili Kakula aliiambia mahakama kuwa kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya uamuzi kama washtakiwa hao wana kesi ya kujibu ama la.

Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba amesema kwa mujibu wa sheria iwapo washtakiwa watapatikana kuwa wana kesi ya kujibu wataanza kujitetea na wakionekana hawana kesi ya kujibu wataachiwa huru.

Hakimu Simba amesema baada ya kupitia hoja zote zilizowasilishwa mahakamani hapo imejitosheleza kwamba washtakiwa wote wana kesi ya kujibu katika mashtaka yote, hivyo wana haki ya kisheria kuanza kujitetea.

Amesema washtakiwa wataanza kujitetea Mei 14 na 15, 2018.
kufuta kesi imeshindikana basi faini mil 3 au jela miaka 5. kwisha habari, sasa ombea yakukute ya kupost chupi au x uone kama utapelekwa ukafunzwe kutumia mitandao, na maanisha kuna matabaka.
 
Back
Top Bottom