Kisutu: Robert Kisena afutiwa Mashtaka ya utakatishaji fedha na Mahakama. Yeye na Mkewe wakamatwa tena, wafunguliwa mashtaka mapya

Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Robert Kisena na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji fedha

Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Cheni Shi (32).

View attachment 1098229

Washtakiwa hao wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu91(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai(CPA) sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Wakili wa Serikali, Grory Mwenda amedai mahakama hapo kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao .

Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema shauri hilo lilikuja chini ya kifungu namba(91) cha CPA sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Washtakiwa hao walisomewa mashtaka yao jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na Mawakili wa Serikali, George Barasa, Ester Martin, Moza Kasubi na Imani Imtumezizi.

Barasa alidai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka hayo likiwamo moja la kuongoza uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, wizi wakiwa wakurugenzi, mashtaka manne ya utakatishaji fedha, manne ya kughushi, manne ya kutoa nyaraka za uongo, mawili kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na moja la kuisababishia mamlaka hasara.

Katika shtaka la kwanza, ilidaiwa kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 kwa mamlaka waliyokuwa nayo waliusababishia mradi wa UDART hasara ya Sh.bilioni 2.41.

Katika shtaka lingine, ilidaiwa kuwa mshtakiwa wa kwanza na wanne, Robert na Shi, wanadaiwa kati ya Mei 26, 2016, wakiwa benki ya NMB tawi la Ilala, wakiwa wakurugenzi wa Kampuni Longway Engineering huku Kisena akiwa Mkurugenzi wa UDART walifanya muamala wa Sh. milioni 603 kupitia akaunti ya benki ya UDART kisha kuzihamishia fedha hizo katika akaunti ya Longway na baada ya siku mbili wakijua fedha ni za kughushi.

Katika shtaka lingine, ilidaiwa kuwa Mei 30, 2016, Robert na Shi katika benki ya NMB tawi la Ilala, walijipatia nyaraka kwa njia ya udanganyifu kutoka katika benki hiyo ikiwa na jina la Fund Transfer Request Form ikiwa na tarehe ya Aprili 6, 2016, kwa lengo la kuonyesha Sh. milioni 750 zimelipwa na Kampuni ya Longway kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa kituo cha UDART Kimara, Kivukoni, Ubungo na Morocco, huku wakijua ni uongo.

Martin alidai shtaka la Robert na Shi, Juni 8, 2016, katika benki ya NMB tawi la Ilala walijipatia kwa njia ya udanganyifu Sh. milioni 595.92 kutoka UDART kwa kuonyesha zimelipwa na kampuni ya Longway ambayo imehusika katika kutengeneza vitu mbalimbali vya mradi huo, huku wakijua ni uongo.

Ilidaiwa kuwa Aprili 6, 2016 katika benki ya NMB tawi ya Ilala, Robert, alighushi nyaraka hiyo kwa lengo la kuonyesha Sh. milioni 594 zimelipwa kwa kampuni ya Longway ambayo imejihusisha na uandaaji, utengenezaji wa vitu mbalimbali wakati ni uongo.

Katika shtaka la kutakatishaji fedha linalowakibili washtakiwa wote wanne, wanadaiwa kuwa kati ya Mei 25, 2015 na Desemba 31, 2016 wakiwa jijini Dar es Salaam kwa nia ovu walibadilisha thamani ya mafuta ya zaidi ya Sh. bilioni 1.21 kuwa fedha ya thamani hiyo baada ya kuyauza mafuta hayo, huku wakijua mafuta hayo ni zao la kosa la wizi.
Kosa lingine ni la kujenga kituo cha mafuta bila kuwa na vibali vya EWURA ambalo linamkabili Robert na Kulwa ambao wanadaiwa walilitenda Januari 1, 2015 na Desemba 31, 2017 maeneo ya Jangwani Ilala.

Inadaiwa kuwa washtakiwa Robert na Kulwa wakiwa wakurugenzi wa Kampuni ya Zenon Oil na Gas Ltd kwa pamoja walijenga kituo hicho cha mafuta bila kuwa na kibali cha EWURA.
Inaweza kuwa kesi nyingi za serikali ni za kubambikiza.

Kama ni kweli hata kama wameachiwa heshima yao imevurugwa sana.

Huyu Robert mmmmmm! ana mambo mambo mengi hayaeleweki.

Kuna wakati alihusishwa na familia ya Rais mstaafu mmoja. Labda kesi hiyo ulikuwa ikielekea kuwagusa vigogo hao.
 
Mbona wend
Hao wanaoza mwaka wa NNE MBONA hawashindi.Tutajie msukuma aliye ndani.
Mbona wengi tu tembelea magereza ya Mwanza,shinyanga nk utawakuta wasukuma wengi tu wanasota kwa makosa mbali mbali kwani hawako juu ya sheria.No research no right to say..
 
Kule wataozea Ruge, Harbinder, Malinzi na Aveva ila hawa wasukuma team Bashite aka mla raha wanatoka tu tena kwa kufutiwa mashitaka baada ya kunegoshieti.
Peter Noni ni mchaga? Nyumbu Mzee wewe
 
Duh kumbe usukuma umefika mpaka huku? Wakuu kuanzia leo mimi ni msukuma na Kesho nitatoa tangazo rasmi gazetini la kubadili kabila kwani usukuma umekuwa ni hazina kubwa awamu hii.
MD Wa Vodacom na wenzake wale wakenya ni wasukuma? MNA akili za kipimbi sana nyie nyumbu
 
Aisee wasukuma wanafutiwa tu mashitaka. Wapi Lugumya. Kisena na ile UDA ilivyofeli jamani. Haya Nduhu tabu.
Lugumi anatakiwa kuokoka, amrudie Mungu wake, kwa jinsi alivyoponea kwenye tundu la simba ngekuwa mimi ningehama nchi..
 
hu
Katika Jitu jinga wewe ni namba moja.Umekaa kuleta hisia za kikabila kabila tu huishi Kuwataja wasukuma wanakusukuma nn?.kwa hiyo sheria isichukue mkondo wake siku kisenha anashikwa kwa kosa la utakatishaji PESA Wabaguzi dhidi ya wasukuma mlishangilia leo ameshinda kesi imekuwa wasukuma wanafutiwa kesi acha mambo ya kibaguzi tujenge nchi yetu bila kujali makabila yetu.
huo ni ukweli? But haya yoote na mengine yatapita?
 
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea nalo dhidi ya washtakiwa hao .
Hakuna awamu hiki kifungu kinatumika kama sasa inaonekana huyu DPP siku hzi hapend kabisa kuendeleza case sjui kwann
 
Kuna umuhimu wa kuangalia hizi powers za DPP. Kuwe angalau na maelezo ya kiliwasukuma kufungua mashitaka na ni wameona mpaka wameamua kufuta. Kuna mtu kaumia hapa, unapomnyima mtu uhuru wake kwa miezi kadhaa, halafu unasema tu, sina nia ya kuendelea, haina tofauti na kumfunga mtu jela bila sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom