Kisonge anguko lake limetimia!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
Maskan kaka ya ccm ya kisonge iliopo unguja eneo la michenzani round about, ambayo kwa miongo mingi ikitamba kuendesha siasa zanzibar na kuamini kuwa wao ndio wenye nchi wako ktk hali mbaya.

Jaribio lao la kwanza la kutaka kumsimika dr bilal awe rais wa zanzibar ili waendelee kuitawala ikulu na kuziburuza siasa za zanzibar lilishindwa dodoma kwa kuchaguliwa dr shein kuwa rais wa visiwa hivyo vya karafuu.

Baada ya hapo wakaanza kazi ya choko choko za chini kwa chini kushawishi wazanzibari hasa waunguja kukataa kura ya maoni kwa kupiga kura ya hapana na kusambaza vikaratasi kila kona.

Jana mheshimiwa rais wa zanzibar kawaondolea uvivu wakati alipokuwa akifungua majenereta yatakayozalisha umeme wakati wa dharura. Kawanyamba hadharani. Kawaambia ikiwa ccm imekaa na kuwataka wanachama wake wapige kura ya ndio wao ni nani kujifanya ai miccm wakubwa kuliko chama. Kwa hakika kawaumbua sana na nategemea kisonge siku zake za kutamba zimefika ukingoni
 
Kauli ya Karume kwa Wanakisonge ni hitimisho tu! Kwani, kwa Kisonge ilishapwaya baada ya Komandoo kuondoka madarakani.
 
mzee, nasikia mpaka dk kamfukuza mkuu wa wialya
mkuu hii sijaisikia. ila habari nilizozipata kwa mida hii kuwa watu wa kaskazini wameamua wengiwao kususa kupiga kura.

wao bado wanaendekeza ile chuki ya uarabu, na kuaminishana kuwa mchele na kokoto mseto haupikiki.

na kisonge na wahuni wachache wa CCM wanaendekeza hio fitina na wakidai ati wanataka ASP yao, wao wamekuwa ndio wafurukutwa na wapenda zanzibar kuliko yeyote.

kazi wanayo wana kisonge

kwenye bao lao la matangazo nasikia wameandika " kula mseto ni hiyari ya mtu"
 
nasikia mkuu wa wilaya ya kati. nasikia alihoji kwanini tume ya kura ya maoni inawashawishi watu kupiga ndio badala ya kuelimisha. kusikia mzee kamweka stop

Kama sababu ya kumfukuza kazi ni hiyo nna wasi wasi mkuu amekosea.
Alichosema huyo DC ni sahihi kabisa,,wao waliwatakiwa watoe tu elimu juu ya kadhia hiyo,,sio kuwashawishi watu waamue NDIO au HAPANA
nikweli kura ya NDIO inamanufaa zaidi ya ile ya HAPANA kwa mazingira ya Zanzibar,, hata hivyo kuna kitu inaitwa DEMOKRASIA
 
Mkuu wa walaya ya kati Ali Hassan Khamis...kuna tetesi hazijathibitishwa kuwa ndiye aliyeongoza kumtafutia wadhamini Dr.Bilal katika wilaya yake...na yupo bega kwa bega na Kisonge...Karume alishazipata habari zake na alikuwa akimvutia pumzi tu, vikaratasi vilivyosambazwa kusini vilimfika Karume na Kificho kabla ya kufika Makunduchi na Darajani...kilichofuata ndiyo hicho...!
 
Mwaka 1965 wananchi wa Tanzania walipiga kura ya maoni waamue watapendelea mfumo gani wa siasa kati ya vyama vingi au chama kimoja, Ulikuwa msimamo wa viongozi wa juu wa TANU na ASP kuwa wanataka chama komoja NDIVYO matokeo yalivyokuwa. Ban Maltipartism
Mwaka 1991 Tume Ya Jaji Francis Nyarari ilitafuta maoni ya watanzania kuamua wanataka mfumo wa gani wa siasa, Matokeo ya Tume yanasema 80% ya waliotoa mawazo yao walitaka mfumo wa chama kimoja (wakiamini ndio msimamo wa chama chao CCM) Viongozi wa juu wa CCM akiwemo Baba wa Taifa Hayati Mwl. Nyerer walipendelea mfumo wa Vyama vingi na NDIVYO ilivyokuwa.

Sitashangaa wazanzibari wanapoteza mamilioni ya pesa na Muda kupiga kura ambayo matokeo yake yanafahamika tayari.
 
Mkuu Mbogela,
You know, CUF baada ya kumalizana kule Bagamoyo ilikuwa tayari tunangojea kauli ya chama cha mapinduzi kupitisha azimio la kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa, lakini akili za akina Yussuf Makamba na Chiligati, walipokutana kule Butiama, wakaona haiwezakani kuwapa CUF ushindi hivi hivi wakataka lazima pawepo misuguano isiyokuwa ya lazima kama hiyo ya uchaguzi uchaguzi tu.
 
naam kura ya maoni imeamua kuwe na mseto.

wakati akina Kisonge walipita nyumba kwa nyumba kunadi kuwa wanataka Hapana.

na leo kwenye gazeti la mwananchi Rais Aman anataka picha yake ilioibiwa Ofisi ya Chama Kiswandui na ambayo ipo Kisonge irejeshwe kwa kweli Kisonge huu ni mwaka wao
 
Maskan kaka ya ccm ya kisonge iliopo unguja eneo la michenzani round about, ambayo kwa miongo mingi ikitamba kuendesha siasa zanzibar na kuamini kuwa wao ndio wenye nchi wako ktk hali mbaya.

Jaribio lao la kwanza la kutaka kumsimika dr bilal awe rais wa zanzibar ili waendelee kuitawala ikulu na kuziburuza siasa za zanzibar lilishindwa dodoma kwa kuchaguliwa dr shein kuwa rais wa visiwa hivyo vya karafuu.

Baada ya hapo wakaanza kazi ya choko choko za chini kwa chini kushawishi wazanzibari hasa waunguja kukataa kura ya maoni kwa kupiga kura ya hapana na kusambaza vikaratasi kila kona.

Jana mheshimiwa rais wa zanzibar kawaondolea uvivu wakati alipokuwa akifungua majenereta yatakayozalisha umeme wakati wa dharura. Kawanyamba hadharani. Kawaambia ikiwa ccm imekaa na kuwataka wanachama wake wapige kura ya ndio wao ni nani kujifanya ai miccm wakubwa kuliko chama. Kwa hakika kawaumbua sana na nategemea kisonge siku zake za kutamba zimefika ukingoni

Nilini shein kachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar?
 
Maanguko mengi yatatokea ila kutokana na namna katiba ya muungano ilivyokaa kama kutakuwa na mabadiliko yatakuwa kidogo. Kibaya zaidi hakutakuwa na mkosaji wa serikali ya mapinduzi maana wote watakuwa humohumo ndani ya serikali, hiyo ni sawa na ndoa ya mitaala ugomvi ni upangaji wa zamu za kulala vinginevyo wakikosa wote hulala njaa,
 
mkuu hii sijaisikia. ila habari nilizozipata kwa mida hii kuwa watu wa kaskazini wameamua wengiwao kususa kupiga kura.

wao bado wanaendekeza ile chuki ya uarabu, na kuaminishana kuwa mchele na kokoto mseto haupikiki.

na kisonge na wahuni wachache wa CCM wanaendekeza hio fitina na wakidai ati wanataka ASP yao, wao wamekuwa ndio wafurukutwa na wapenda zanzibar kuliko yeyote.

kazi wanayo wana kisonge

kwenye bao lao la matangazo nasikia wameandika " kula mseto ni hiyari ya mtu"

Kisonge ni watu waliokosa madaraka na mafisadi waliokuwa wakiishi kwa kutumia siasa za kibaguzi. Kisonge na watu wengine wa kaskazini wanatabia ya kudai eti ASP yao ni ile ya zamani wanaendekeza siasa za ubaguzi kuvuta hisia za wazanzibar. Zanzibar sasa hivi ni ya wasomi, zanzibar sasa hivi ina vijana wengi wanaishi nchi za nje Uarabuni na Ulaya (exposure) si ile zanzibar ya zamani ambapo watu wanadanganyika kirahisi. Ndio maana hawa watabakia peke yao kwani hakuna mzanzibar anafurahishwa na biashara ya ubaguzi iliyokuwa ikiendelea pale. Wakae tu huko Kwahani na Donge wakilishana sumu but Zanzibar inabadilika watu wamechanganyika mno inabidi na wao wabadilike kimtazamo badala ya kutumia siasa za kibaguzi kuhalalisha wizi wanaoufanya serikalini.
 
Kifo cha nyani miti yote huteleza hayo ndio yanaoendelea sasa Muembe kisonge .
 
Back
Top Bottom