Ryan The King
JF-Expert Member
- Oct 6, 2016
- 2,789
- 2,706
Mambo wololo wololo Wakubwa.
Ungana Nami Tupa Wa Fasihi katika Simulizi hili la hisia, hisia tamu za mapenzi.
Jiachie....
Mlio wa ngoma unasikika na sauti ya wanawake wanaopiga vigelele inasikia umbali wa Mita 20 kutoka katika nyumba ya kina Adela. Adela alisikia sauti hizo alipokuwa bado yupo kitandani amelala.
Alijuliza moyoni mwake kuna nini huko nje. Adela alitoka na kumkuta Mama yake akiwa anatwanga kisamvu kwa ajili ya mboga za usiku.
"Mmh Adela ulikuwa bado umelala?"
Mama yake Adela alimuuliza Adela aliyejifunga kanga kwenye mabega akiwa anachukua kigoda cha kukalia.
Sauti ya ngoma na shangwe inaongezeka na kumfanya Adela amuulize Mama yake kuna nini. Mama hakuweza kumjibu kwani yeye mwenyewe Hakujua kilichokuwa kinaendelea.
Makundi ya Wamama yaliovalia sare ya madera yalikuwa yakipita jirani na nyumba ya kina Adela. Bila shaka walikuwa wakienda kwenye Shughuli ya harusi.
Mmoja wa wanawake waliokuwa wakipita alipiga vigelele na kubinua makalio yake na kukata mauno wenzake wakimshangilia.
"Alu lu lulu luuuu atajibeba, wakuolewa awe yeye"
Wale wanawake waliongea huku wakiangalia nyumbani kwa kina Adela.
Si Adela si Mama yake wote hawakuelewa chochote. Walibaki kushangaa tuu. Wale wanawake walipita kelele zao zikiendelea kusikika kwa mbali.
"Mama mbona wamesema vile mama?"
Adela alimuuliza mama yake aliyekuwa akitoa kisamvu kwenye kinu.
"Achana nao mwanangu hao ni wanawake Wasiojiheshimu"
"Kwani Mimi mbaya mama?"
"Hapana mwanangu we mzuri, huoni shapu umechukua kwangu, jicho lote langu, rangi ya Bibi yako, urefu wa Baba yako. Yaani Kama kuzaa nimezaa"
Mama Adela aliongea huku akijichezesha kwa maringo mbele ya mwanaye hali iliyomfanya Adela acheke.
"Mama kumbe umooo eehee"
Adela aliongea akiwa mchangamfu zaidi.
"Chezea Mimi weeeye, enzi zangu Wanaume walipigana vikumbo katika nyumba ya mzee Mbogo kwa sababu yangu"
Adela alikuwa akimuangali Mama yake akijielezea kwa kujigamba na maringo.
"Mtoto nilijaliwa kalio, sio hili lililozeeka, lilikuwa tako haswa"
Aliongea huku akilitingisha tako lake Adela amuangalia Mama yake huyo ambaye alikuwa kajaliwa haswa msambwanda wa haja.
"Mmh basi Mama maana"
Adela aliongea akinyanyuka kwenda ndani akitingisha msambwanda wake uliomkubwa haswa. Ni wazi alirithi kwa Mama yake.
"Mashalaah mtoto wangu kajaliwa, bila milioni nne mtoto hatoki humu ndani"
Mama Adela aliongea akiangalia tako la mwanaye. Alikiri kuwa mtoto wake anamakalio makubwa. Alijua kuwa yeye alivyokuwa Kama Adela hakuwa na matako makubwa vile.
Kelele za shangwe ziliongezeka. Ngoma zilirindima. Adela alitoka akiwa kavaa suruali nyeusi na blauzi ya kijani. Suruali yake ilichora chupi iliyokuwa imebeba akadumba kubwa iliyokuwa inatingishika.
Adela alimuaga Mama yake kwenda kuangalia kule kelele na sauti ya ngoma inapotokea.
Akiwa kwa mbali aliona watu wengi ambao wengi wao walikuwa wanawake waliovalia madera. Alidhangaa kuona watu hao kwenye nyumba ya kina Michael mpenzi wake. Ilibidi aharakishe kwenda kujionea kuna nini.
Ulikuwa mziki wa singeli uliokuwa ukiendelea uliowapagawisha wanawake hao ambao walikuwa wanatingisha makalio yao.
Adela alifika na kukuta wanawake washughuli wakipepeta matako yao na kukata mauno Kama panga boi.
aliwaona na wale waliopita nyumbani kwao wakampiga vijembe. Walivyomuona walisonya na kusema;
"Hehe heeeeeeee kaogeeee, wakuolewa uwe wewe"
Maneno hayo yalimchoma na mbaya zaidi alikuwa haelewi kinachoendelea.
Wadada wale walimfuata na kuanza kumzunguka na kuimba taarabu ya mafumbo. Lilikuwa onyesho mubashara kwa watazamaji waliokuwa pale.
Masikini Adela hakujua hili wala lile. Akili yake iliingia hofu na wasiwasi.
"Mabibi na mabwana mpoooooo"
MC alichombeza na kufanya watu kuitikia.
"Tupoooooooo"
Kidogo utulivu ukionekana.
"Harusi safii"
"Safiiiiii"
"Mambo biyeeeee sio biyeeeee"
"Biyeeeeee"
Waliitikia na vigelele gele juu.
" bwana harusi na Bibi Harusi sasa hivi Watakuwa Mubashara katika ukumbi wetuu. Wapi vigele gele kina mama"
"Alu lulu luluuuuu"
Wakina mama walipiga vigele gele Dj kwa mbali akiachia kamziki kasauti ya chini ka Singeli hali iliyowafanya watu waanze kucheza na kupiga kelele.
"Dj Achie gomaaaa hilo"
Adela alikuwa mpole Kama njiwa. Ujanja wote ulimpotea.
"Dj weka kichupa cha kuwatoa maharusi"
MC aliongea watu wakiwa kmya macho yakiangalia mlangoni ambapo maharusi watajia. Dj aliweka kichupa cha singeli mnato.
Maharusi walijitokeza mlangoni watu wakishangilia kwa jinsi walivyopendeza.
Adela hakuamini macho yake. Alihisi yupo kwenye zile ndoto za Abunuasi. Kama haitoshi alijihisi ni Alinacha kabisa.
Alimuona Michael akiwa ndiye Bwana harusi. Bumbuazi lilimchukua mpaka kwenye mji wa kushangaa. Aliduwaa. Sasa alikumbuka Yale maneno ya Wale wanawake.
"Kuolewa awe yeye"
Alizungumza kwa sauti ya chini kufuatisha maneno ya wale wanawake.
Vigele gele, shangwe na nderemo ziliongezeka. Michael alikuwa ananata na suti yake ya dark bluu. Alikuwa anaangaza macho yake huko na huko Kama mtu anayetafuta kitu. Adela alitamani macho yake yagongane na ya Michael.
Maharusi walikuwa tayari wamekaa sehemu zao. Wapiga picha walikuwa wanahangaika kuchukua picha ili kupata mapozi mazuri zaidi.
Adela machozi yalikuwa yakimtoka. Alihisi uchungu moyoni mwake.
Mwanaume aliyempenda ndio huyo anaoa.
Aliona hana sababu ya kuendelea kukaa pale. Akiwa katika huzuni aliita kwa sauti ya chini.
"Michael!"
Michael aliyekaa kule mbele aligeuza shingo Kama mtu aliyesikia kitu fulani. Ukweli ni kuwa hakusikia chochote kwani sauti aliyoitoa Adela isingeweza kufika kule mbele.
Waligongana macho, Michael alimuona Adela akiwa anatoa machozi. Adela alipoona Michael amemuona aligeuka Nyuma na kukimbia.
"Adelaa"
Michael aliita jina hilo hali iliyofanya watu washangae.
Itandelea....