Kisima cha maji chahama baada ya Waziri wa Maji kufanya ziara

Malaika Mkuu

JF-Expert Member
Nov 5, 2014
901
907
Mtendaji aliesimamia Aapa kilikuwepo muda michache uliopita
255652860991_status_e29a0733c78341f594862eddd56b4868.jpg
 
Mtendaji: Aseee imekuaje tena kisima mbn kilikua hapa hapa dakika 2 tu zilizopita?

Mwenyekiti: Dah mweshimiwa ni kweli tulikaa nacho hapo sio muda hata asubuhi nilipita hapa nilikikuta kilikua na maji mengi kabisa.

Waziri: Aaah basi basi sawaa au itakua kimeenda kujaza maji alafu badae ivi kitaludi eti.

😂😂 Nchi ya ajabu sana hii inabidi tumkodi Putin au Kiduku kwa miaka 10 mambo yawe sawa.
 
Mtendaji aliesimamia Aapa kilikuwepo muda michache uliopitaView attachment 2267808
Kawaulize watu wa mabenki watakwambia vituko wanavyokutana navyo.mtu anaandika dhamana nyumba wakienda kukagua Kuiona wanakuta haipo anaapa kuwa ilikuwepo hapo hata yeye anashangaa haipo!! Kama wao wanavyoshangaa!!

Uaminifu Tatizo ndio maana inatakiwa staili ya kibabe kama ya Magufuli kusimamia wafanyakazi public sector
 
Duh.

Hii nchi itabidi kukaa na bastola mkononi. Waporaji ni wengi, magerezani hawatatosha.
Huwezi kuongoza nchi kama nyapara anayesimamia wafungwa. Nchi inaongozwa kwa mfumo maalumu na madhubuti uliowekwa baada ya kufanya research ya kina. Hawa watu wanaambiwa kila siku lakini wanajifanya ''mwache mama kwanza ajenge uchumi''.

Uchumi gani anajenga wakati watu ndiyo kwanza wanashindana kula? Kuna ofisi fulani jamaa yangu anasema ukiona watu wanavyopiga fedha kwa vikao hewa utalia. Mwezi uliopita alikunja milioni 11 za magumashi. Anasema kila mtu analalamika mambo yalikuwa yamebanwa mno wakati wa Magufuli, sasa wacha wapumue.
 
Kawaulize watu wa mabenki watakwambia vituko wanavyokutana navyo.mtu anaandika dhamana nyumba wakienda kukagua Kuiona wanakuta haipo anaapa kuwa ilikuwepo hapo hata yeye anashangaa haipo!! Kama wao wanavyoshangaa!!

Uaminifu Tatizo ndio maana inatakiwa staili ya kibabe kama ya Magufuli kusimamia wafanyakazi public sector
Wafanyakaz wa serikali wamekua wahuni sana yaaan wanatakiwa wasimamiwe na mjeledi ndiyo ataenda
 
Ila aweso anakumbana na vihoja huko field

Kuna ile ingine alienda sumbawanga sijui mbeya

Mvua ikawa inapiga pembeni ya mkutano wake
 
. Uchumi gani anajenga wakati watu ndiyo kwanza wanashindana kula?
Umesahau kuikamilisha sentesi hiyo,..., ngoja nami niimalizie; "kwa urefu wa kamba zao."

Mkuu 'macho', ninakubaliana nawe katika jambo la "mfumo"; lakini hatuna viongozi wa kusimamia hiyo mifumo, achilia mbali kujenga mifumo inayofanya kazi ipaswavyo.

"Unyapara", unaweza kuwa na nafasi yake muhimu sana kwa jamii kama hii yetu, mradi unyapara huo utendeke katika taratibu zinazoeleweka, kisheria , bila kuoneana wala kupendeleana.

Niseme tu, mada hii ni nzuri sana, huenda nikapata michango inayounga uamini wangu juu ya kuweza au kutoweza kwa serikali kusimamia kwa ufanisi shughuli zake zote bila ya kusemwa kwamba haina uwezo wa kufanya baadhi ya mambo, kama biashara.

Ngoja niangaze macho.
 
Mama akikopa hela,watu wanafurahia,zikija,eti wanajiita wajanja,wanazila,halafu nyingine kiduchu,wanatuzugia kuzifanyia kazi lengwa,ujinga kabisa huu.
 
Back
Top Bottom