Kishimba ni mmoja wa matajiri wakubwa Botswana

Kishimba ni mmoja wa matajiri wakubwa Botswana

Acha kudanganya watu hapa JF.

Hao matajiri wanakuwa hawalipi kodi miaka nenda, miaka rudi kwa sababu ya kuhonga watu wa TRA.

Kuna wafanyabiashara wako clean na wanaichachafya serikali kila siku lakini wanaendelea kufanya biashara zao bila tatizo lolote.

Kishimba alikuwa anafanya biashara nyingi tu za chini ya meza huku polisi na TRA wakijifanya hawaoni.

... hadi alipokataa kutoa mchango.
 
Ni kweli kuwa Jumanne Kishimba alishahamishia biashara zake Botswana nae anaishi huko, aliihama nchi yake ya kuzaliwa kwa mizengwe mikubwa aliyoandamwa ktk biashara zake wakati wa serikali ya awamu ya tatu.
Napata tu hofu juu ya source yako ipelekeayo kuwa Kishimba ni miongoni mwa matajiri wakubwa Botswana.
hapa ndio huwa nachoka na habari zetu. Mimi binafsi namfahamu Kishimba yuko hapa dar anakaa masaki na alikuwa anasimamia ule ujenzi wa majengo yake karibu na ubalozi wa kenya kuna fremu nyingi za maduka na kuna sanamu ya samaki mkubwa huwa anatoa maji amesimama mbele. amesimamia ujenzi toka unaanza mpaka unaisha na alikuwa na ofisi mle ndani. kama huamini waulize wale wapangaji.

Pili, Kishimba aliwekeza zimbabwe ila kwa botswana sina uhakika kama mnavyosema. Na alikwenda kule kwa sababu alipata matatizo wakati meli yake ya mizigo ilipozama na kuuwa wakati haikuwa na bima. ila kwa sababu ya fedha kesi ilishaisha.
kuhusu utajiri kuna mambo mengi huwa yanaweza kuonyesha wingi wa utajiri wa mtu kodi ikiwa mojawapo. ila kigezo cha kulipa kodi nyingi si kwamba ndio tajiri namba moja, labda nifafanue hapa kwetu kuna bidhaa zinatozwa kodi nyingi kama mafuta, nguo, magari. na kuna bidhaa nyingine inatozwa kodi kidogo au hakuna kabisa kama vyakula. sasa unaweza ukafanya biashara ya tshs. 10 milioni ya magari ukalipa kodi kubwa zaidi ya mfanyabiashara ya chakula ya tshs. 50 milioni. ukienda kwenye kodi utaonekana umelipa nyingi ila ukija kibiashara wa chakula ndio mfanyabiashara mkubwa.
hata apa kwetu Konyagi mwaka jana wamelipa kodi kubwa kuliko barrick kwa sababu ya msamaha wa kodi ila si kwamba konyagi ni kampuni kubwa au tajiri kuliko barrick.
 
Back
Top Bottom